Kulivyo Geita tofauti na mabilioni ya dhahabu yaliyopo

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Hii nchi sijui shida hipo wapi yani kuwepo kwa mgodi mkubwa hapo geita na kiwango cha dhahabu inayotoka ni tofauti na mkoa wenyewe hapa geita mjini.
nyumba za ovyo kwa wananchi,mazingira mabovu hakuna mipango miji na matukio yaliyopo huku hakuna toofauti na kongo kule goma.
nimefika ila mpaka naona aibu yani ni kama mgodi hupo porini hapa geita mjini. boresheni geita ijivunie kinacho toka
 
Mfumo wa kapu Moja la mgawanyo wa Rasilimali ndio shida.

Ndio maana hata Mbeya inachangia Pato la Taifa namba 3 ila Sasa kulivuo hakufananii na Trilioni 10 wanazotoa Kwa Taifa Kila mwaka.

Pesa zinachukuliwa na kujenga Dar,Arusha na Sasa Dom na Mwanza.

Kuna haja ya kuandika Upya kanuni ya mgawanyo wa Rasilimali za Taifa
 
Kwahiyo kila sehemu itumie chake sio? Serikali ya majimbo ndo suluhu, makusanyo yote yanakuja Dsm, then ndo kinaamuliwa kili kiende wapi!
Wala hakuna haja ya Majimbo,Kenya kuan Majimbo?

Hii hii Mikoa,ni kuweka tuu kanuni nzuri ya mgawanyo na wale wanaopungukiwa ndio wanajaziliziwa na Serikali kuu.

Kunawekwa kanuni ya kuchangia na kanuni ya kugawana.Ilivyo Sasa kanuni ni vile mkipata viongozi wengi kutoka kwenu ndio kidogo mtapata kaupendeleo.
 
Pesa zina enda kujenga dar,mwanza ,arusha na dodoma nyie mikoa mingine kuleni shisha tu na mlipekodi zenu zika jenge pengine..si mli kataa serikali ya majimbo.

Sema nazani serikali ni wakati sasa waache kuwekeza zaidi kujenga dar isha jaa
 
Inaudhi sana.Hata hicho kinachoitwa csr ni upuuzi wa Hali ya Juu.

Mnapewa csr kama sehemu ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri mkiweka Bajeti ya Nchi na hiyo inahesaniwa so hakuna Cha maana mnakuwa kuwa na Madini tofauti na wale ambao hawana
 
Pesa zina enda kujenga dar,mwanza ,arusha na dodoma nyie mikoa mingine kuleni shisha tu na mlipekodi zenu zika jenge pengine..si mli kataa serikali ya majimbo.

Sema nazani serikali ni wakati sasa waache kuwekeza zaidi kujenga dar isha jaa

Mhhh, hivi kuna watu bado wanaenda kujenga arusha! Bora ya Dar and Mwanza, àu dom na Morogoro
 
Mfumo wa kapu Moja la mgawanyo wa Rasilimali ndio shida.

Ndio maana hata Mbeya inachangia Pato la Taifa namba 3 ila Sasa kulivuo hakufananii na Trilioni 10 wanazotoa Kwa Taifa Kila mwaka.

Pesa zinachukuliwa na kujenga Dar,Arusha na Sasa Dom na Mwanza.

Kuna haja ya kuandika Upya kanuni ya mgawanyo wa Rasilimali za Taifa
Na kheri hali ya sasa, kuliko lilivyokuwepo jiji moja tu la Dar ndio maana watu wengi wakakimbilia huko.

Nadhani ni bora tuwe na majiji makubwa hata matano ili watu waweze kupata huduma wanazozitaka kuliko kufikiria kukimbilia dar

Japo unalolisema ni la muhimu sana, Kama kila mkoa utafaidika na makusanyo yake bhasi hata hawa viongozi wa mikoa na majimbo watachangamsha akili kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kuyajenga maeneo yao. Ila hii ya kuitegemea serikali kuu ndio mzizi haswa wa kutegemea vyama na kujikomba kwa viongozi wakubwa ili wapendelewe.

Bottom line, je, serikali kuu itakuwa tayari kuukata huo utegemezi ambao kwa kiasi kikubwa unawapa nguvu kubwa kisiasa, mimi sijui 🙏🏽
 
uwezi amini yani geita mjini mpaka fisi wapo
😁😁😁 uoto na ikolojia asili,

Nakuelewa mkuu, unless pawe pamebadilika ila lile vumbi na mji ulivyo na hadi kuingia huko katoro. Huwezi sema katika zile poor town centres kuna madini pale
 
Watu wake hawana ustaarabu(hawajitambui) unataka jipya gani wafanyiwe?
 
Na kheri hali ya sasa, kuliko lilivyokuwepo jiji moja tu la Dar ndio maana watu wengi wakakimbilia huko.

Nadhani ni bora tuwe na majiji makubwa hata matano ili watu waweze kupata huduma wanazozitaka kuliko kufikiria kukimbilia dar

Japo unalolisema ni la muhimu sana, Kama kila mkoa utafaidika na makusanyo yake bhasi hata hawa viongozi wa mikoa na majimbo watachangamsha akili kutafuta vyanzo vipya vya mapato ili kuyajenga maeneo yao. Ila hii ya kuitegemea serikali kuu ndio mzizi haswa wa kutegemea vyama na kujikomba kwa viongozi wakubwa ili wapendelewe.

Bottom line, je, serikali kuu itakuwa tayari kuukata huo utegemezi ambao kwa kiasi kikubwa unawapa nguvu kubwa kisiasa, mimi sijui 🙏🏽
Kama strategy ingekuwa kujenga Majiji makubwa Kila Kanda tungeyaona,badala yake Serikali inajenga Dar,Dom na Arusha tuu ila kwingine watajijua.

Huko Mwanza wanalazimika kujikongoja kujenga ni Kwa vile ni Kanda ya watu wengi vinginevyo kungeouuzwa tuu kama kwingine.

Watu wamepunguza Kwa kiasi kuhamia Dar Kwa vile walau Mikoani Huduma za msingi walizokuwa wanazifuata Dar wanaweza zipata huko huko au maeneo ya jirani.

Tuwe na kanuni ya mgawanyo wa Mali Kwa Mikoa kama ilivyo huko USA au Kenya.
 
Back
Top Bottom