Kulipia bima kubwa ya gari (Comprehensive) kupitia kampuni za simu

DENAMWE

JF-Expert Member
Dec 29, 2019
807
805
Naomba kufahamu manufaa na changamoto za kukata bima kubwa ya gari (Comprehensive) kwa kupitia mitandao ya simu kama vile Voda bima.

Utaratibu wao ukoje? Inawezezekana kulipa taratibu? Ukipata ajali unafidiwa kwa taratibu zipi?
 
Mimi nasema usijaribu. Kuna mtu huko analia voda bima ya afya wanagoma kumlipa.
 
BIMA kata kwa mawakala wakubwa, kwenye makampuni makubwa ie Icea Lion, BUMACO, ZIC, NIC, PHOENIX, SANLAM, CRDB INSURANCE, JUBILEE etc
 
Kulipia taratibu sijui ila nachojua unaweza kukata ya mwezi mmoja, miezi 3,6 ama mwaka.

Ongea nao huduma kwa wateja watakuelewesha kama kuna mikopo.

Bank ndio najua kuna kitu kama hicho. Unakata comprehensive labda 2m, wanakua wanakukata kwa mwezi labda laki 2 hadi inaisha.
 
Hakuna changamoto process iko wazi, ila ACHANA na takataka hizo! Yani ukate bima kubwa ya chombo chako online kwa nchi kama Tz, nenda kwa provider anayeeleweka Mkuu.

Ukikwama njoo inbox nitakupa maelekezo then utaamua wewe.


Narudia achana nao
 
Huku Naweza kAta ya miezi 6,,nilikuwa JUBILEE, imeisha ,Sasa nataka 3rd ,wananambia ni lazima iwe mwaka,
BIMA kata kwa mawakala wakubwa, kwenye makampuni makubwa ie Icea Lion, BUMACO, ZIC, NIC, PHOENIX, SANLAM, CRDB INSURANCE, JUBILEE etc
 
Back
Top Bottom