Habari wapendwa,
Poleni na majukumu ya maisha. Wandugu nisiwachoshe mwenzenu kuna mkasa umenipata yaani nashindwa kufanya maamuzi.
Stori inaanza hivi, mimi niliolewa na nikajaaliwa kupata watoto watatu wawili ni twins, mume wangu ni mkristo mimi muislamu.
Sasa wakati mume wangu ananioa nimemkuta na mtoto alizaa na mdada flani hivi muigizaji wa Bongo Movie.
Huyo dada hakumuoa alizaa nae tu wakaachana na mtoto huyo nimemlea mimi mpaka sasa yupo darasa la2.
Mwaka juzi nilipata mkasa mzito sintosahau, nilipakaziwa kitu ambacho sijafanya ikawa ndo sababu na nikaachika kwa talaka kabisa.
Ni kwamba kuna mtu inasemekana alipiga simu kwa wakwe zangu na kujitambulisha kwamba yeye ni rafiki yangu na tupo kwa mganga kwa lengo la kumroga mume wangu nimuue ili nirithi mali zake.
Muda wote huo me skujua kwanini mama mkwe ananichukia ghafla wakati mwanzo alinipenda kama amenizaa.
Mwisho wa siku nikapewa talaka nikarudi kwetu nikiwa na mimba ya mtoto mwingine, nimehangaika peke yangu mpaka nimejifungua.
Nikarudi chuo nimemaliza chuo mume wangu amenifuata kuniomba msamaha turudiane tulee watoto wetu.
Kibinadamu nikamsamehe lakini Mungu hamfichi mnafiki siku ikafika nikagundua aliefanya huo mchezo ni yule mwanamke aliezaa nae lengo lake arudi yeye.
Lakini kisicho riziki hakiliki pamoja na kufanya hayo bado mume wangu hakumrudia.
Akapata bwana mwingne ni askari akazaa nae mtoto mmoja, huyo bwana aliona picha yangu Instagram akanitafuta,yeye hakujua na hajui kama namjua.
So amekua mpenzi wangu kwa muda kidogo, mimi nilikua nafanya kwa kumkomoa yule mwanamke alieniharibia kwangu.
Sasa jamaa huyu ndo amenogewa anataka ndoa nampa tarehe tu kila siku yani nimedata tu hapa.
Nampenda sana na ananipenda hivi keshokutwa anataka kunipeleka kwao Usukumani kunitambulisha.
Mume wangu wa kwanza huyo ni mkristo, huyu ni mkristo but yupo tayari kubadili dini hata leo.
Nampenda ni mstaarabu, muwazi, mkweli, ana huruma, anajua mapenzi tofauti na wa mwanzo.
Sasa nawaza je, akija kujua kama mimi nilikua nalipiza kisasi atanichukuliaje?
Atanipenda? Haya nitamuachaje yule niliezaa nae watoto watatu wakati ameshaomb radhi?
Ushauri please