Nafsi ni zile zile, kasoro maumbile ya kibaiolojia tu, kwamba huyu ni "me", huyu ni "ke", lakini udhaifu wa tamaa ni ule ule.
Mwanzoni wanamke unamtamani, ni mzuri kwa sura na ana mvuto kwenye macho yako, unamchumbia na kumuoa, hatimaye mnapata watoto nk nk.
Mnazoeana na hatimaye kumuona wa kawaida sana, miaka inasonga.
Baadae ule mvuto unatokomea na kumuona kama dada'ko mtoto wa baba yako.
Wakati huo wenzio wanamuona mrembo na anavutia. Na kwa wanawake ni hivyohivyo jinsi wanavyowaona waume zao baada ya kuishi miaka nenda rudi, mivuto husinyaa.
Kwa hiyo mautundu na mambo mengine ya awali mliyoanza nayo hutokomea menyewe. Hapo kupepesa macho kwingine ni jambo lisilozuilika, ni maisha, ni ubinadamu.