Kulikoni bunge haliko live?

Kulikoni bunge haliko live?

Bangoo

JF-Expert Member
Joined
Nov 3, 2011
Posts
5,597
Reaction score
1,016
Ni kawaida kila mkutano wa bunge unapofunguliwa sisi tulioko nyumbani tunasubiria kwenye tv zetu kuangalia nini kinaendelea huko mjengoni dodoma, lakini leo hakuna hata tv moja inayoonyesha mkutano huo wa bunge. Je ni sababu gani zimefanya hata tbc ya serikali kuacha kuonyesha mkutano huo muhimu? Hata star tv haionyeshi! Hali hii siyo nzuri wanayotutendea serikali.

Kuna tetesi za chini chini kwamba kuna mkono wa serikali ambao umezuia vituo vya televisheni nchini kutorusha kipindi cha Bunge siku ya leo kutokana na uoga wa maccm kwamba cdm watajipatia uaarufu maana makamanda wamejipanga..tbccm nao eti mtambo haujakaa vizuri.
-Hizi ni fikra mgando sana...na ni ukatili kwa wananchi!!na wanaharakati wafuatiliaji.
-Uchaguzi wa maccm wiki chache zilizopita ulirushwa moja kwa moja na tbccm!!!!!!!lakini leo kwakuwa kila jicho la mtanzania wanajua lipo dodoma...wameona watukatili kwa kutuletea porojo zisizo na mantiki kwa umma.

>>YOU CAN FOOL ALL THE PEOPLE SOME OF TIME,AND SOME OF THE PEOPLE ALL THE TIME,BUT YOU CAN'T FOOL ALL THE PEOPE ALL THE TIME
 
Wanamwogopa Lema, wanataka kujua anaingia kwa style gani kwanza!!!
 
je ni hofu gani inayohofia serikali maana walianza kuzibiti star tv na sasa hata tbc? Hofu ni ni mbona watu wengi hawana ving'amuzi!
 
Uozo ni mwingi sasa wananchi wakiona inakuwa taabu!
Dawa nikuondoa ccm madarakani come 2015!
 
TBC wametoa sababu ya kijinga kabisa.... but kikubwa hapa ni ujio wa lema live hawataki kuuona ata star tv nayo imebuma.

But tutaona tu kwenye source nyingine makini.
 
Nakumbuka Spika wa Bunge Bi Anne makinda aliwahi kusema kwamba atapiga MARUFUKU bunge kuoneshwa LIVE, kwasababu eti sisi wapiga kura hatutakiwi kufahamu wanachoongoa bungeni kwasababu ni SIRI. Labda hiyo marufuku ndiyo imeanza kutekelezwa.
 
lema amewafanya wasionyeshe spika makinda ameagiza watumishi wa bunge wawasiliane na star tv pamoja na TBC kipindi cha leo kisirushwe kwanza kwani ni aibu kwao lema kurudi hasa ukizingatia hoja wa waziri mkuu muongo spika alisha iuwa na walizungumza na lema na kumsii awe mpole ila hawamwamini hivyo imewalazimu kuchukua tahadhari. Msihofu kesho bunge litakuwa live kama kawaida ingawa wanaweza kupiga marufuku vipindi vya bunge kurushwa ili kukabiliana na wimbi hili la mabadiliko. nawasilisha mkuu
 
CCM ni map..mb...
Sina maana hyo!namaanisha mapumba,kama ukijaza nafasi zilizo wazi!
 
si hawataki tuone maigizo yao ya ZE COMEDY!!!!shame on them.
 
Tbc1 wameibuka na gia kuwa mtambo wao wa kurusha matangazo ya moja kwa moja ya bunge umepata hitilafu na kuharibika.swali, je hawajafanya makusudi ili watu wasione ujio wa Lema bungeni leo?!iweje mtambo ukorofishe leo leo siku ya bunge?!natafakari
 
Hivi kwanini mungu asimchukue tu huyu bibi mkora.its our constitutional rights to be informed
 
Wanamwogopa Lema, wanataka kujua anaingia kwa style gani kwanza!!!

sasa wamesema hawataweza kuonyesha bunge eti wanaomba radhi! Hivi ingekuwa ni ishu kubwa na mna taarifa siku zote hizo mngesema hivyo! Upuuzi mtupu kwa tbccm
 
M4C hawana pesa imebaki ya kuanzisha TV ili watuonyeshe? Wafanye hivyo mbona nchi hadi sasa CCM wameishindwa!!!!
 
Back
Top Bottom