Kulaumu ndiyo suluhisho ya matatizo yako?

Ibrahimeliza

Member
Nov 25, 2020
37
26
Kulaumu ndiyo suluhisho ya matatizo yako?

Au kifichio cha kutokufanikiwa katika mambo yako?

Acha kulaumu ndugu yangu acha lawama, acha kuwalaumu wazazi wako kwakila kitu unachokipitia, kuna mtu humu akipata ugumu au changamoto kidogo tu, baba angenifanyia hivi nisingekuwa na maisha haya au mama angenifunza jambo fulani ningeweza kuishi na watu vizuri, acha lawama ndugu, acha kuwalaumu waliokuzunguka.

Anza kuishi maisha ambayo unatamani wazazi wako wangekupatia badala ya kulaumu yaishi maisha ambayo unatamani ungepatiwa na wazazi wako au waliokuzunguka, yaishi sasa kwani mtu siyuleyule si ndo wewe, ni wewe wewe wewe tu

Kuwa makini na wewe usije kulaumiwa na wanao
 
Back
Top Bottom