Kulalamikia matokeo ya tabia mbaya ni kuihalalisha! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kulalamikia matokeo ya tabia mbaya ni kuihalalisha!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by IsangulaKG, Sep 19, 2011.

 1. IsangulaKG

  IsangulaKG Verified User

  #1
  Sep 19, 2011
  Joined: Oct 14, 2010
  Messages: 702
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 45
  Nakwazika sana tena saaaaaaana ninapoona watu wenye akili timamu (kwa kuwa wameweza kuandika ina maana wana akili timamu) wakilaumu vitendo vya wafuasi wa CHADEMA kwa Mama Fatuma huko Igunga.

  Siku Zote mimi huangalia tatizo kwa jicho jingine
  Kwa mfano, kuhoji kwa nini wananchi wanamuadhibu mwizi badala ya kujiuliza kama kuiba ilikuwa halali maana kama mwizi asingeiba kwa kuwa anajua kuiba ni kosa yasingemfika ya kumfika.
  Naamini mama Fatuma ana akili timamu ndiyo maana alipewa ukuu wa Wilaya, sipendi kuamini kuwa alipewa nafasi hyo kwa kupendelewa na kama imani yangu ni sahihi inamaanisha alikuwa anajua anachokifanya au yatakayo mfika kama anavunja taratibu. Mwizi anapoiba anajua kuna kukamatwa akaadhibiwa au akatoka salama. Kwa mama Fatuma ,kwa mfano wa Mwizi alikamatwa na akaadhibiwa stahili yake, kwa nini ulalamike???? Ooh mara kadhalilishwa, kwani walimfuata Ofisini au Nyumbani kwake wakamvuta vuta au kumvua Hijabu?

  Nasikitika sana kuona bado Tanzania ina watu wavivu wa kufikiri wanaolaumu laumu malipo ya Dhambi! Unapofikiria kuwa wanachadema hawajatenda haki , fikiria kuwa je mama Fatuma alitenda haki? Alitumia akili yake ipasavyo? Kwa nini asifanye kazi siku zote mpaka asubiri mkutano wa CHADEMA? Ukiuliza hayo na kupata majibu huna sababu ya kuwalaumu makomandoo wa Chadema, hawakumfuata mama nyumbani kwake , Kimsingi naona Mama huyu Hakustahili hata kupewa nafasi aliyonayo!

  Na wote wanaoshabikia na KUMSUPPORT kwa upuuzi wake pia wapuuzi tu! au Vibaraka wa CCM!
   
Loading...