lukelo sakafu
JF-Expert Member
- Feb 19, 2015
- 2,938
- 517
wakuu hama kweli duniani kuna mambo,hii imetokea leo mchana hapa dar, leo niliingia kwenye mgahawa moja maeneo ya mnazi moja nikaagiza ugali na samaki, mara akaingia jamaa moja yupo smart sana, akaagiza chakula, chips mayai na kuku, lakini alipoletewa chakula chake kulikua kuna kisu na uma katika sahani kwa maana anatakiwa kula chakula chote kwa kutumia kisu na uma tu na sio mikono,mara baada ya chakula kuwekwa mezani yule jamaa akawa anaongea peke yake kwa lugha ya kichaga, mara nikaona jasho likimtoka taratibu, akashika uma na kisu na kuanza kula ghafla akadondosha uma chini ya meza,jamaa akaangalia kushoto na kulia kisha akaendelea kula tena akadondosha kisu nacho akakiokota akaangalia tena kulia na kushoto akaendelea kula, alipokua anakula kuku ndipo mambo yakaharibika zaidi kwani alishindwa jinsi ya kumkata mara kuku wote akadondoka chini mara nikasikia"yerewiii hii short babangu walah vile sikuachi my chiken" jamaa akamuokota than akaweka pembeni uma na kisu akaenda kunawa mikono na kuendelea kula