Watu wengi wa Kanda ya Ziwa sio wastaarabu wakati wa kula, wanatia kinyaa!

Nominee

JF-Expert Member
Sep 5, 2017
459
1,240
Picha linaanza, nimeenda ukweni kanda ya ziwa kulipa mahari. Siku hiyo walichinja Ng'ombe na msosi ulikuwa wa kutosha. Muda wa kula nakumbuka sisi tuliwekwa sehemu moja na wenyeji wetu wawili ili tusiwe wapweke, daah walivyokuwa wanalamba vidole wale mabwana hadi nikaghairi kula. Wenyewe wanasema kuwa haitakiwi mkono ubaki na mabaki ya chakula, kwahiyo wanalamba mikono haswa ili kuisafisha huku wanaendelea kula, pia hawajui kula sehemu moja. Muda huu atamega tonge upande huu, ila tonge la pili litamegwa upande ule na tonge la tatu litamegwa katikati. Nikamtumia meseji waif afanye mchakato aniletee chakula cha peke yangu, kweli kikaletwa nikala. Japo maneno ya chinichini yaliongeleka kuwa sipendi kula sahani moja na wenyeji.

Baada ya kuwa mwenyeji hii kanda kwa takribani miaka minne ndio nimegundua kuwa ile siku ya mahari haikuwa bahati mbaya, watu wengi huku kuanzia Simiyu, Shinyanga, Mwanza hadi mara wapo hivyo. Kukuta mtu anakula huku anajichokonoa meno kwa vidole mbele za watu ni kawaida, kula na kukibehulia chakula ni kawaida, kula huku analamba vidole vyote vitano ni kawaida sana, Kula chakula bila kuchagua upande ndio kabisa hawa jamaa ni mafundi, wanadonoa chakula kama kuku. Inatia hasira sana na inakera kushuhudia watu wa namna hii.

Angalau kidogo kwa waliosoma soma na wale wenye exposure ya kusafiri sehemu mbalimbali ndio wanaunafuu.

USHAURI: Wazazi wa kanda ya ziwa wafundisheni vijana wenu ustaarabu wakati wa kula.

Kuna mashemeji zangu walikuja kunitembelea ila nikawaambia waziwazi kuwa sipendi kumuona mtu anakula hovyo kama mbwa hapa nyumbani kwangu. Walienda kusimulia huko walipotoka kuwa nina roho mbaya ila mimi sijali.
 
Pana Lile kabila ugali wa moto unaliwa kwenye sufuria kubwa pamoja na sufuria ya mboga Kama camp hivi.
Ukikata tonge ukaachia kisa unaungua mwenzako anapita na tonge lako wao mikono Yao imekomaa.
Usipokuwa makini utaambulia maji ya kunawa tu.
Ugali moto mboga moto.
 
Mimi nikisemaga kuwa wasukuma ni watu wa hovyo huwa naonekana mbaguzi, hao watu waanzishiwe kule Mwanza chuo cha ustaarabu kuwe na kozi za namna ya kuongea, kula, kuvaa na namna ya kuishi na jamii zingine. Wasukuma ni watu wa hovyo sana bora masai
 
Back
Top Bottom