Kula-kulala wanapowindana usiku na mchana….!

Baba, hujajua ni nini kilichokufikisha hapo ulipo? Umepata medali gani hadi sasa? Kuwasaidia ndugu sio tatizo, tatizo ni kuwalea kama mayai! Nawajengea mazingira ya kujitegemea, msaidie ndugu apate kazi aondoke. Aibu gani mtu anafukuzwa kazi ama anakufa familia nzima mnatafuta pa kutawanyikia? Mbona sie tumetoka kwako kila mtu anajitegemea hadi Cantalasia?
He! mwanangu ndivyo nilivyokufundisha hivyo, kutowajali ndugu zako wa damu na ndugu wa mumeo! mimi sijakufundisha tabia hiyo na najiuliza sijui umeipata wapi. wakati ule kabla sijakubinafsisha kwa mumeo si uliona jinsi nyumba yetu ilivyosheheni ndugu wa pande mbili wa mama yenu na ndugu zangu, kwani hujui hiyo ni mila yetu. sasa kwa nini uache mila?
 
Da, AshaDii, unaweza kuhusishwa bila wewe mwenyewe kupenda, yanaweza kuporomoshwa matusi na ukatajwa, au unaweza kusingiziwa umefanya jambo ambalo hata hukuwaza na hili linaweza kutamkwa katikati ya matusi................. unaweza kufunga mkwiji au kibwebwe na kuingia uwanjani mwenyewe bila kupenda............... si unajua ugomvi huwa haunogi kama mlengwa hakuhusishwa?

Mtambuzi mie nikipigana na mtu atanipiga tu! Sijawahi pigana maishani mwangu... hivo hizo techniques sizijui... Ugomvi siku zooote huja as a result ya kutaka fuatiliana saana na kujuana kwa undani na pia kushindana. Sasa kama mimi nawapuuza ndugu wa mume wangu kwa vituko vyao - kwanini ndugu upande wangu waingilie kwa vitimbi? Unless otherwise hao wanandugu wa mume waje wanivamie nyumbani na kunitundika mangumi (sijui wataanzia wapi lakini); hapa kweli ndugu najua waweza inglia kutaka leta ugomvi ju! Siwezi tukanana pia.... Walau kwa maandishi naweza tukana.... But sio ile nabishana na mtu kwa matusi... Lazima tu atanitukana atanimaliza na kuniadhiri na kunianika hapo..... Kuepusha hilo akija mtu kunitukana nitamuangalia tu.... mpaka pale atapomaliza.... na nitamuuliza kama kakaukiwa maji nimpe..... (najua ndo njia pekee nitamuongeza hasira ambazo kapania kunipatia....
 
Mkuu halafu shuhudia itokee baba kafariki,shemeji atavamiwa chumbani hakuna cha faragha wala nini breki ya kwanza ni briefcase ya marehemu maana wanawahi cheque books,halafu itokee bahati mbaya shemeji hakuzaa ndo kabisaaa wanapata na kisingizio.jamani kinababa kuandika wosia/will muhimu jamani!

Na kama walikuwa wamekabidhiwa baadhi ya miradi waisimamie, wanajigawia mirathi
 
Nakubaliana na extended family, maana wengi wetu ni matunda ya extended families, lakini watu kugeuza nyumba yangu kuwa sehemu ya malumbano ysiyo na tija kamwe sikubaliani nalo ...

Wakitaka ugomvi, wakafanyie huko kwaoooo ...

Ukicheka na nyani utavuna mabua ....!
 
Mtambuzi mie nikipigana na mtu atanipiga tu! Sijawahi pigana maishani mwangu... hivo hizo techniques sizijui... Ugomvi siku zooote huja as a result ya kutaka fuatiliana saana na kujuana kwa undani na pia kushindana. Sasa kama mimi nawapuuza ndugu wa mume wangu kwa vituko vyao - kwanini ndugu upande wangu waingilie kwa vitimbi? Unless otherwise hao wanandugu wa mume waje wanivamie nyumbani na kunitundika mangumi (sijui wataanzia wapi lakini); hapa kweli ndugu najua waweza inglia kutaka leta ugomvi ju! Siwezi tukanana pia.... Walau kwa maandishi naweza tukana.... But sio ile nabishana na mtu kwa matusi... Lazima tu atanitukana atanimaliza na kuniadhiri na kunianika hapo..... Kuepusha hilo akija mtu kunitukana nitamuangalia tu.... mpaka pale atapomaliza.... na nitamuuliza kama kakaukiwa maji nimpe..... (najua ndo njia pekee nitamuongeza hasira ambazo kapania kunipatia....

Wewe ni mwerevu................ Hongera kwa msimamo wako!
 
Bora wagombane kuliko ije ile aibu ya kupeana mimba!

Sauala kubwa hapa ni kuto-entertain ndugu wa pande zote kukaa hapo kwa namna yoyote ile!
 
Ukiona kula - kulala wanapigana au kuleta ugomvi hiyo familia haina baba
Bora ku-outsource tu

Kuna mashamba, ngombe wa kuchunga, mbuzi, palizi, kuvuna, fuga kuku, name it
Wapate wapi huo muda wa kupigana???
 
Ngumu sana kuishi Nuclear family
Labda kama umetoka familia bora
Lakini hizi third world families
Its inevitable
Ila ni kuwa na rules and principles zilizo wazi
Anayeshindwa basi akatafute kwingine

Hujawahi jiegesha kwa watu hata mwezi
Ili kujipanga tayari kwa kutoka?

Bora wagombane kuliko ije ile aibu ya kupeana mimba!

Sauala kubwa hapa ni kuto-entertain ndugu wa pande zote kukaa hapo kwa namna yoyote ile!
 
There u go! Una akili kama mchwa wa kizungu!
Unawapa ugali washibe, waangalie tv tu, nguvu za ziada watazipeleka wapi! Hawasomi, hawalimi!
Ukiona kula - kulala wanapigana au kuleta ugomvi hiyo familia haina baba
Bora ku-outsource tu

Kuna mashamba, ngombe wa kuchunga, mbuzi, palizi, kuvuna, fuga kuku, name it
Wapate wapi huo muda wa kupigana???
 
Hivi umeshawahi kuona ndoa ambapo zinafumuka ngumi kati ya ndugu wa mke na wale wa mume, humohumo kwenye nyumba ya wanandoa? Kama hujawahi, una bahati mbaya tu, kwani ni nyingi za kutosha ndoa za aina hiyo.

Ni ndoa ambazo, ndugu wa mume wanatafutana usiku na mchana na wale wa mke. Kila upande unajaribu kutafuta ushindi ili ndiyo uwe unashikilia nyumba kimamlaka. Hawa ndugu wa mume au mke, mara nyingi ni wale wanaoitwa kula-kulala. Au ni wale wanaoamini kwamba, mradi fulani ni ndugu yake anayo haki ya kuvaa nguo yake ya ndani muda wowote akishikwa na hamu ya kufanya hivyo.

Lakini bila shaka ufa ambao umejengwa na wanandoa wenyewe, ndiyo unaoruhusu hali kama hii. Hawa ndugu wanatumia udhaifu huo kupata kile wanachohitaji, siyo kwamba ni kweli wanawapenda hao ndugu zao. Ingekuwa wanapenda, wangewasaidia kuwaunganisha kwa njia mbalimbali.Kwenye nyumba nyingi, ugomvi au mvutano kati ya ndugu wa mume na wale wa mke ni wa chinichini sana, lakini unasaidia kwa nguvu ileile kuvunja uhusiano wa wawili ambao waliapa kwamba, kifo ndicho kitawatengenisha.

Hatimaye kinachowatenganisha siyo kifo, bali ndugu. Mtu unajiuliza, ni kwa faida ya nani na kwa nini ni lazima iwe hivyo.
Ndoa inaweza kuwa na matatizo, lakini kuwepo kwa matatizo hakuna maana ya ndugu kuruhusiwa kuiingilia na kuwafanya wanandoa kama wanasesere. Sina maana kwamba, ndugu wasipokuwepo ndoa ndiyo itakuwa nzuri, hapana. Lakini, ninachosema ni kwamba, ndoa ni zao la watu wawili ambao waliamua kwa hiyari yao kulizalisha. Wanapoamua zao hilo liwe ni kondoo na mbwa mwitu wanaonesha ni kwa kiasi gani uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

Kama watu bado wanaishi pamoja, bila kujali wanapigana kutwa mara ngapi, wana haki ya kulinda ndoa yao isiingiliwe na watu wengine. Tukumbuke kwamba, kuna watu ambao wako tayari kuuwa mtu ili wapate wanachotaka kutoka kwetu sisi ndugu zao au watoto wao. Kwa sababu hiyo, kwa ushabiki wao, tunaweza kujikuta tukiwauwa wapenzi wetu na hivyo kubadili kabisa historia ya maisha yetu.

Kama tunagombana sana au kama hatuna mawasiliano, tusifanye udhaifu huo ukaonesha ujinga wetu kwa ndugu na jamaa zetu. tugombane, tushindwe kuwasiliana, lakini iwe ni siri yetu.

This happened to me guys!wanandoa be wise
 
tatizo la kukosa vitu vya kufanya ndo husababisha watu wabadilike kitabia na kufanya vitu ambavyo kibinadamu haviko sahihi .. kula kulala siku zote anatakiwa awe na malengo ya kujikwamua na si kuharibu alipo au kuharibu utaratibu wa watu kimaisha
 
Ikiwezekana ndugu msaidie kule kule alipo, mambo ya kuishi na ndugu yana matatizo yake, kama kuna uwezekano wa kumsaidia alipo msaidie kule kule, na mie wanisaidie huku niliko la sivyo.............................
 
Baba, hujajua ni nini kilichokufikisha hapo ulipo? Umepata medali gani hadi sasa? Kuwasaidia ndugu sio tatizo, tatizo ni kuwalea kama mayai! Nawajengea mazingira ya kujitegemea, msaidie ndugu apate kazi aondoke. Aibu gani mtu anafukuzwa kazi ama anakufa familia nzima mnatafuta pa kutawanyikia? Mbona sie tumetoka kwako kila mtu anajitegemea hadi Cantalasia?

Halafu nyie wanangu wawili yaani wewe na Cantalisa, umoja wenu unaninyima usingizi...................... mkipanga njama, lazima nione cha mtema kuni. natafuta mbinu ya kuwafarakanisha wallahi
 
Suala hili sidhani kama lina ukanda, kwa sasa imekuwa ni kutoka pande zote za nchi hii.Kikubwa zaidi hapa ni kwamba tuwapokee kwa muda maalumu kwa lengo maalum na likishakamilika warudi makwao.
 
Back
Top Bottom