Kula-kulala wanapowindana usiku na mchana….! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kula-kulala wanapowindana usiku na mchana….!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Jan 3, 2012.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Hivi umeshawahi kuona ndoa ambapo zinafumuka ngumi kati ya ndugu wa mke na wale wa mume, humohumo kwenye nyumba ya wanandoa? Kama hujawahi, una bahati mbaya tu, kwani ni nyingi za kutosha ndoa za aina hiyo.

  Ni ndoa ambazo, ndugu wa mume wanatafutana usiku na mchana na wale wa mke. Kila upande unajaribu kutafuta ushindi ili ndiyo uwe unashikilia nyumba kimamlaka. Hawa ndugu wa mume au mke, mara nyingi ni wale wanaoitwa kula-kulala. Au ni wale wanaoamini kwamba, mradi fulani ni ndugu yake anayo haki ya kuvaa nguo yake ya ndani muda wowote akishikwa na hamu ya kufanya hivyo.

  Lakini bila shaka ufa ambao umejengwa na wanandoa wenyewe, ndiyo unaoruhusu hali kama hii. Hawa ndugu wanatumia udhaifu huo kupata kile wanachohitaji, siyo kwamba ni kweli wanawapenda hao ndugu zao. Ingekuwa wanapenda, wangewasaidia kuwaunganisha kwa njia mbalimbali.Kwenye nyumba nyingi, ugomvi au mvutano kati ya ndugu wa mume na wale wa mke ni wa chinichini sana, lakini unasaidia kwa nguvu ileile kuvunja uhusiano wa wawili ambao waliapa kwamba, kifo ndicho kitawatengenisha.

  Hatimaye kinachowatenganisha siyo kifo, bali ndugu. Mtu unajiuliza, ni kwa faida ya nani na kwa nini ni lazima iwe hivyo.
  Ndoa inaweza kuwa na matatizo, lakini kuwepo kwa matatizo hakuna maana ya ndugu kuruhusiwa kuiingilia na kuwafanya wanandoa kama wanasesere. Sina maana kwamba, ndugu wasipokuwepo ndoa ndiyo itakuwa nzuri, hapana. Lakini, ninachosema ni kwamba, ndoa ni zao la watu wawili ambao waliamua kwa hiyari yao kulizalisha. Wanapoamua zao hilo liwe ni kondoo na mbwa mwitu wanaonesha ni kwa kiasi gani uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sana.

  Kama watu bado wanaishi pamoja, bila kujali wanapigana kutwa mara ngapi, wana haki ya kulinda ndoa yao isiingiliwe na watu wengine. Tukumbuke kwamba, kuna watu ambao wako tayari kuuwa mtu ili wapate wanachotaka kutoka kwetu sisi ndugu zao au watoto wao. Kwa sababu hiyo, kwa ushabiki wao, tunaweza kujikuta tukiwauwa wapenzi wetu na hivyo kubadili kabisa historia ya maisha yetu.

  Kama tunagombana sana au kama hatuna mawasiliano, tusifanye udhaifu huo ukaonesha ujinga wetu kwa ndugu na jamaa zetu. tugombane, tushindwe kuwasiliana, lakini iwe ni siri yetu.
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kweli kabisa utaliona ji mwanaume zima lina lala nakuamka hazi hataki kisa kaka yake ana uwezo na bila haya anataka ajifanye na yeye anapanga sheria hata haya haoni, kwao hataki kwenda utadhani kazaliwa na kaka yake anajitia mapenzi tele kwa kakake kumbe fisadi, mpenda dezo....
   
 3. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #3
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Walisema ndugu wakipewa nafasi huvunja ndoa au uhusiano hawakukosea kabisa......................
   
 4. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  mostlu unakuta ndugu wa kike wa pande zote
  vidume sio saana
   
 5. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #5
  Jan 3, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Nikiwa kama mama mwenye nyumba na mke humo ndani.... Sitaingilia ndugu zangu na mume wangu wakigombana.... Kwa sharti moja tu.... Watoke ndani ya nyumba na himaya yetu wapeleke ugomvi wao mbele!
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kwa nini ufuge mimama na mibaba mizima kwenye nyumba yako?
  Baadae hata chupi zao zikichakaa utakuja ombwa pesa ya kwenda kununua
   
 7. obsesd

  obsesd JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 23, 2011
  Messages: 1,226
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  kweli kbs yan, afu inaboa hii hali mmh.
  mm kamwe sina entertain wandugu jaman ni waharibufu 2 wa nyumba za wa2.
  njoo unitembelee uondoke mambo ya kutaka kulala tena jaman akuuu, especially mawifi wawe wanatulia makwao jaman mmh. kucha kwa kaka zao loh.
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Da, AshaDii, unaweza kuhusishwa bila wewe mwenyewe kupenda, yanaweza kuporomoshwa matusi na ukatajwa, au unaweza kusingiziwa umefanya jambo ambalo hata hukuwaza na hili linaweza kutamkwa katikati ya matusi................. unaweza kufunga mkwiji au kibwebwe na kuingia uwanjani mwenyewe bila kupenda............... si unajua ugomvi huwa haunogi kama mlengwa hakuhusishwa?
   
 9. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #9
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  The Boss, kwa taarifa yako bado kuna wanaume wanaishi kwa dada zao walioolewa....................
   
 10. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #10
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  kaka hali ya uchumi na mila na desturi zetu bado zinaamini katika extended family, ukikataa kukaa na ndugu zako utatengwa na kupewa majina mabaya na kashfa chungu mzima.
   
 11. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #11
  Jan 3, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Ni dhambi na nahisi Mungu hapendi kuwa-entertain ndugu wa pande zote mbili kuwa tegemezi. Kama hawataki kufanya kitu kitakachowatoa nyumbani kwangu (kusoma, ama kujishughulisha/kutoa ushirikiano kupata kazi) kwa kweli I will denounce them. Kama hawana wazazi ntawataftia shamba niwaanzishie kijiji cha ujamaa. Humo watajenga na miti na udongo, watalima (nawapa mfuko wa mbegu), nikienda kuwatembelea narudi na viroba vya mboga. Si ndo maana ya undugu kufaana?
   
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  sijapinga hilo
  nimepinga tabia ya kugombana gombana mostly ni wadada...
   
 13. P

  Pure nomaa JF-Expert Member

  #13
  Jan 3, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 1,049
  Likes Received: 1,073
  Trophy Points: 280
  Ni kweli hao kula kulala huwa na matatizo sana kwenye ndoa ya kaka au dada yake.na mara nyingi sana hurudi nyumbani muda wa msosi tu,utawasikia wakiuliza shemeji msosi bado?afadhali kula-kuamka hawana matatizo sana
   
 14. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #14
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Hizi tabia wanazo wagogo toka Dom na watu wa Musoma huko kuhamia ukoo mzima kwa ndugu waliopo mjini.
  Lakini inategemea wewe unawachekea vp maana unaweza filisika au ukaishi kwa hofu kwa kuogopa kutengwa.
   
 15. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #15
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  He! mwanangu ndivyo nilivyokufundisha hivyo, kutowajali ndugu zako wa damu na ndugu wa mumeo! mimi sijakufundisha tabia hiyo na najiuliza sijui umeipata wapi. wakati ule kabla sijakubinafsisha kwa mumeo si uliona jinsi nyumba yetu ilivyosheheni ndugu wa pande mbili wa mama yenu na ndugu zangu, kwani hujui hiyo ni mila yetu. sasa kwa nini uache mila?
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jan 3, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Labda tubadilishe mfumo wa maisha kutoka huu wa extended family ndio tutaondokana na tatizo hili.
   
 17. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #17
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Haya mawani yangu yame-expire, hawa Lions Club sijui wataanza lini ile kampeni yao ya kutoa mawani bure pale Mnazi Mmoja. Nimekuelewa The Boss, nilikuwa sijaona hilo neno "Mostly"

   
 18. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #18
  Jan 3, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Kwa nini usiwanunulie jembe la mkono na uwape mbegu warudi kijijini wakalime kuliko kuwafuga kama mbwa nyumbani kwako?
   
 19. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #19
  Jan 3, 2012
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,795
  Likes Received: 1,247
  Trophy Points: 280
  Katavi, nani aanze....................!? naogopa kutaja makabila, lakini kuna makabila, ukikataa kukaa na ndugu zako, watakuloga............LOL
   
 20. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #20
  Jan 3, 2012
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  Mkuu halafu shuhudia itokee baba kafariki,shemeji atavamiwa chumbani hakuna cha faragha wala nini breki ya kwanza ni briefcase ya marehemu maana wanawahi cheque books,halafu itokee bahati mbaya shemeji hakuzaa ndo kabisaaa wanapata na kisingizio.jamani kinababa kuandika wosia/will muhimu jamani!
   
Loading...