Kukufuru Mwenyezi Mungu

Kukufuru Mwenyezi Mungu

La shaka ALLAH ni Mwingi wa msamaha,
PIA JUA MAANA YA KUFURU NA SHIRKI KISHA UJE UPINGE KWA HOJA NA DALILI
Lakin nasaha zangu kwako, ISOME DINI YAKO.


وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلنَّارِۖ هُمۡ فِيهَا خَٰلِدُونَ

Na wenye kukufuru na kuzikanusha ishara zetu, hao ndio watakao kuwa watu wa Motoni, humo watadumu.

Al Baqara 39

Nyingine hii

👇👇👇👇

قُل لِّلَّذِينَ كَفَرُواْ سَتُغۡلَبُونَ وَتُحۡشَرُونَ إِلَىٰ جَهَنَّمَۖ وَبِئۡسَ ٱلۡمِهَادُ


Waambie walio kufuru: Karibuni mtashindwa na mtakusanywa, mtiwe kwenye Jahannam; nako huko ni makao mabaya kabisa.

Al Imran, aya 12.

Nyingine
👇👇👇👇
وَٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَكَذَّبُواْ بِـَٔايَٰتِنَآ أُوْلَٰٓئِكَ أَصۡحَٰبُ ٱلۡجَحِيمِ

Na wale walio kufuru na wakakanusha Ishara zetu, hao ndio watu wa Motoni.

Al-Ma'idah 10.

Ziada

إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ مِنۡ أَهۡلِ ٱلۡكِتَٰبِ وَٱلۡمُشۡرِكِينَ فِي نَارِ جَهَنَّمَ خَٰلِدِينَ فِيهَآۚ أُوْلَٰٓئِكَ هُمۡ شَرُّ ٱلۡبَرِيَّةِ

Hakika walio kufuru miongoni mwa Watu wa Kitabu na washirikina wataingia katika Moto wa Jahannamu wadumu milele humo. Hao ndio viumbe waovu kabisa.

Al-Bayyinah, Ayah 6

Sasa ndg yangu je baada ya hizi dalili je waweza kutupa faida nasisi juu ya dalili ya ALLAH kuwasamehe MAKAFIRI NA WASHIRIKINA?
Baarakallah feeyka



Mkuu mimi ninakubaliana kabisa na hizo aya za Qur'an, ila mimi sikubaliani na maneno yako yanayopinga baadhi ya aya za Qur'an pale uliposema:-

"Allah hasamehi yoyote atakayekufuru ila tu kama atafikwa na mauti akiwa katika ukafiri"

Neno "YOYOTE" uliloandika ndilo linaloleta mushkeli, kwani ukisoma katika 18:58, inasema:- "Na Mola wako ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa huruma, kama angaliwashika kwa yale waliyochuma basi angaliharakisha adhabu kwao, lakini wanao muda maalumu ambamo hawatakimbia."

Hapo katika hiyo aya Mungu anajaribu kwanza kuonyesha msamaha na huruma yake kwa wakosefu kabla ya kuwaadhibu, na kuna aya kadhaa zinataja kwamba Allah ni mwingi wa huruma 6:147, 18:58 nk.

Kwakuwa kusamehe na huruma ni sifa za Allah basi wapo makafiri atakaowasamehe na wapo atakao waadhibu kwa sababu kuadhibu ni moja ya sifa yake pia na ndiyo maana napinga matumizi ya neno kafiri "YOYOTE".

Ukisoma katika 5:118, Nabii Isa (as) anasema/atasema siku ya kiyama juu ya watu wake waliokufuru kwamba:- "In tua'dhibtum fainnahum i'baaduka wa in faghfirlahum fainnaka anta al aziizul hakiim"


Yaani; kama utawaadhibu wao ni watumishi wako na kama utawasamehe Wewe ni mwenye nguvu mwenye hekima"


Ukiangalia tafsiri yako ya ukafiri uliyoitoa mwanzoni mwa uzi wako (ambayo ninaikubali), hapo hao wafuasi wa Nabii Isa (as) nao ni makafiri na Nabii Isa (as) anataja sifa ya kusamehe ya Allah ili kama akipenda aitekeleze juu ya wafuasi wake siku ya kiyama, hivyo pia katika siku ya hukumu (kiama) Allah atawasamehe baadhi ya makafiri atakapopenda na siyo kafiri YOYOTE ataadhibiwa, kwahiyo nafasi ya watu (makafiri) kusamehewa na ALLAH ipo.
 
Na pia kwa kauli yako hiyo hapo juu (rangi nyekundu) kukanusha ile aya niliyoiweka
Unayajua madhara ya kuikataa Aya au sunnah?
Kama wewe ni Muislam na hujui kawaulize wajuzi walo jiran na wewe na unaowaamin.
Kisha uione hukmu yake


Mimi sipingi aya za Allah, na ninamuomba Allah (swt) anilinde na kadhia hiyo na anipe ufahamu wa kujua sana maana za maneno ya Qur'an.

Mimi napinga maneno yako kwamba kafiri "YOYOTE" ataingia motoni, wapo watakaoingia motoni lakini kuna wengine atawasamehe kulingana na huruma yake. YEYE NI MSAHEMEVU NA MWENYE HURUMA SANA, sasa niambie ni nani anayetakiwa kusamehewa na Allah kati ya kafiri na muumini ili sifa ya Allah ya kusamehe ifanye kazi??, Zingatia kwamba dhambi isiyosameheka siku ya kiama ni Shirk tu, hivyo zingine zote zinaweza kusameheka Allah atakapopenda.
 
Mkuu mimi ninakubaliana kabisa na hizo aya za Qur'an, ila mimi sikubaliani na maneno yako yanayopinga baadhi ya aya za Qur'an pale uliposema:-

"Allah hasamehi yoyote atakayekufuru ila tu kama atafikwa na mauti akiwa katika ukafiri"

Neno "YOYOTE" uliloandika ndilo linaloleta mushkeli, kwani ukisoma katika 18:58, inasema:- "Na Mola wako ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa huruma, kama angaliwashika kwa yale waliyochuma basi angaliharakisha adhabu kwao, lakini wanao muda maalumu ambamo hawatakimbia."

Hapo katika hiyo aya Mungu anajaribu kwanza kuonyesha msamaha na huruma yake kwa wakosefu kabla ya kuwaadhibu, na kuna aya kadhaa zinataja kwamba Allah ni mwingi wa huruma 6:147, 18:58 nk.

Kwakuwa kusamehe na huruma ni sifa za Allah basi wapo makafiri atakaowasamehe na wapo atakao waadhibu kwa sababu kuadhibu ni moja ya sifa yake pia na ndiyo maana napinga matumizi ya neno kafiri "YOYOTE".

Ukisoma katika 5:118, Nabii Isa (as) anasema/atasema siku ya kiyama juu ya watu wake waliokufuru kwamba:- "In tua'dhibtum fainnahum i'baaduka wa in faghfirlahum fainnaka anta al aziizul hakiim"


Yaani; kama utawaadhibu wao ni watumishi wako na kama utawasamehe Wewe ni mwenye nguvu mwenye hekima"


Ukiangalia tafsiri yako ya ukafiri uliyoitoa mwanzoni mwa uzi wako (ambayo ninaikubali), hapo hao wafuasi wa Nabii Isa (as) nao ni makafiri na Nabii Isa (as) anataja sifa ya kusamehe ya Allah ili kama akipenda aitekeleze juu ya wafuasi wake siku ya kiyama, hivyo pia katika siku ya hukumu (kiama) Allah atawasamehe baadhi ya makafiri atakapopenda na siyo kafiri YOYOTE ataadhibiwa, kwahiyo nafasi ya watu (makafiri) kusamehewa na ALLAH ipo.



Nakiri ALLAH NI MWINGI WA MSAMAHA NA HUMSAMEHE AMTAKAYE LAAKIN YEYE ALLAH NDIYE ALIYESEMA HASAMEHE KUSHIRIKISHWA,


إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا


Hakika ALLAH hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha ALLAH basi hakika amezua dhambi kubwa.

An-Nisa'a Ayah 48
👇👇👇👇👇👇


إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَظَلَمُواْ لَمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ طَرِيقًا


Hakika wale walio kufuru na wakadhulumu hawi ALLAH wa kuwasamehe wala kuwaongoa njia.

An-Nisa'a, Ayah 168.

👇👇👇👇👇👇

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا


Hakika ALLAH hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha MOLA MLEZI basi huyo amepotea upotovu wa mbali.

An-Nisa'a, Ayah 116
Ndg yangu naomba kwanza jua maana ya Kufuru kisha jua shirki ni Nini maana Kufuru na shirki Baba na mama yao ni mmoja.
Na kama shirk huijui utaipukaje? Si huenda ukawa ushatumbukia?
 
Mimi sipingi aya za Allah, na ninamuomba Allah (swt) anilinde na kadhia hiyo na anipe ufahamu wa kujua sana maana za maneno ya Qur'an.

Mimi napinga maneno yako kwamba kafiri "YOYOTE" ataingia motoni, wapo watakaoingia motoni lakini kuna wengine atawasamehe kulingana na huruma yake. YEYE NI MSAHEMEVU NA MWENYE HURUMA SANA, sasa niambie ni nani anayetakiwa kusamehewa na Allah kati ya kafiri na muumini ili sifa ya Allah ya kusamehe ifanye kazi??, Zingatia kwamba dhambi isiyosameheka siku ya kiama ni Shirk tu, hivyo zingine zote zinaweza kusameheka Allah atakapopenda.
Kufuru unaijua?
 
Nakiri ALLAH NI MWINGI WA MSAMAHA NA HUMSAMEHE AMTAKAYE LAAKIN YEYE ALLAH NDIYE ALIYESEMA HASAMEHE KUSHIRIKISHWA,


إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدِ ٱفۡتَرَىٰٓ إِثۡمًا عَظِيمًا


Hakika ALLAH hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha ALLAH basi hakika amezua dhambi kubwa.

An-Nisa'a Ayah 48
👇👇👇👇👇👇


إِنَّ ٱلَّذِينَ كَفَرُواْ وَظَلَمُواْ لَمۡ يَكُنِ ٱللَّهُ لِيَغۡفِرَ لَهُمۡ وَلَا لِيَهۡدِيَهُمۡ طَرِيقًا


Hakika wale walio kufuru na wakadhulumu hawi ALLAH wa kuwasamehe wala kuwaongoa njia.

An-Nisa'a, Ayah 168.

👇👇👇👇👇👇

إِنَّ ٱللَّهَ لَا يَغۡفِرُ أَن يُشۡرَكَ بِهِۦ وَيَغۡفِرُ مَا دُونَ ذَٰلِكَ لِمَن يَشَآءُۚ وَمَن يُشۡرِكۡ بِٱللَّهِ فَقَدۡ ضَلَّ ضَلَٰلَۢا بَعِيدًا


Hakika ALLAH hasamehi kushirikishwa na kitu. Lakini Yeye husamehe yasiyo kuwa hayo kwa amtakaye. Na anaye mshirikisha MOLA MLEZI basi huyo amepotea upotovu wa mbali.

An-Nisa'a, Ayah 116
Ndg yangu naomba kwanza jua maana ya Kufuru kisha jua shirki ni Nini maana Kufuru na shirki Baba na mama yao ni mmoja.
Na kama shirk huijui utaipukaje? Si huenda ukawa ushatumbukia?



Assalam aleykum wa rahmatullah wa barakatuhu.

Ndugu yangu, naona tunazunguka hapohapo tu.

Mimi nimesema kulingana na sifa ya Allah sifa ya kusamehe na huruma (الغفور و الرحيم) ni lazima sifa hiyo itende kazi kama jinsi sifa ya ukali katika kuadhibu inavyofanya kazi, kimsingi sifa yenye nguvu sana ni sifa ya kusamehe na huruma kuliko sifa ya kuadhibu.

Nilikupa aya ambamo Nabii Isa (as) atakapo sema siku ya kiama kwa ajili ya watu wake kumuambia Allah; " kama utawaadhibu hao ni watu wako na kama utawasamehe wewe ni mwenye nguvu mwenye hekima" (5:118).

👆🏻👆🏻Hapo utaona kuna options mbili ambazo Allah anaweza kutenda juu ya hao wafuasi wa nabii Isa (as) ambao walikufuru ama awaadhibu au awasamehe, sasa wewe unaposema YOYOTE aliyekufuru ataadhibiwa, je wewe huoni hiyo aya na aya zingine za aina hiyo ambamo msamaha umetajwa??


Ni Kufuru ya ushirikina tu ndiyo haiwezi kusameheka, sasa kama ni ushirikina tu ndio hausameheki ni dhahiri kuwa kufuru zingine zote zinaweza kusameheka pale Allah kwa uwezo na hekima zake atakapotaka.

Kukufuru maana yake ya asili ni "kupinga", katika masuala ya dini kufuru maana yake ni kupinga mafundisho ya Mungu, mfano Mungu hataki ushirikina (kumshirikisha) wewe unapofanya shirki hapo utakuwa umepinga mafundisho ya Mungu na kwa upande huo wewe unakuwa ni kafiri katika ushirikina.


Mungu kwanza ni msahemevu na mwenye huruma-----halafu ni mwenye kuadhibu na hata katika kuadhibu hiyo ni kutokana na huruma yake ya "kuwaponya" watu na makosa waliyotenda.

Kwa hiyo usimchore Allah katika sura ya kuadhibu tu na ukasahau ile sura yake nzuri ya kusamehe na huruma.
 
Back
Top Bottom