SI KWELI Kuku ana sumu kali kuliko Nyoka?

SI KWELI Kuku ana sumu kali kuliko Nyoka?

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Kuna kipande cha video huko Insa nimekiona jamaa anaelezea kuwa kuku wana nyoka kali kuliko ya nyoka. Hili Limekaaje wakuu?

1790578164286.png
 
Tunachokijua
Kuku ni ndege wa kufugwa anayetumika kwa ajili ya biashara, kitoweo na mayai. Kitendo cha kuku kulalia mayai ni kitendo cha kawaida cha kuendelea kuongeza kizazi chake ambapo hufanya hivyo mara baada ya kumaliza kutaga. Kuku hulalia kwa muda wa siku 21 na baada ya hapo vifaranga hujiangua kutoka kwenye mayai.

Miongoni mwa sifa anazokuwa nazo kuku anayelalia ni kuwa mkali kwa lengo la kulinda mayai yake, hivyo anaweza kushambulia ikiwa utatakakuyagusa ama kuyahamisha mayai yake.

JamiiCheck imepitia makala mbalimbali kuhusu kuku na kubaini kuwa hakuna chanzo kinachomtaja kuku kama kiumbe chenye kuzalisha sumu na badala yake hutumia njia mbalimbali kujilinda ambazo hazihusiani na kuzalisha sumu. Njia hizo ni pamoja na;

  • Kuvimbisha manyoya yake ili kuonekana mkubwa zaidi.
  • Kutanua mabawa yake wazi.
  • Kumrukia, kumdonoa, au kumkwaruza mshambuliaji.
  • Kutoa sauti ya kuzomea au kunguruma, hasa kuku wanaolalia.

Kituo cha kuzia na kupambana na magonjwa cha Marekani kinaeleza kuwa kuku hawana meno lakini midomo yao inaweza kusababisha majeraha makubwa wanapokuuma au kukudonoa.

Vimelea vya magonjwa vinaweza kuenea kupitia kuumwa, kudonolewa au kukwaruzwa na kuku, hata kama jeraha linaonekana kuwa dogo au si kubwa.

Kwa hiyo, epuka kuumwa, kudonolewa au kukwaruzwa na kuku na ndege wa majini unaowafuga nyumbani.

Ni muhimu kufahamu kuwa kuku wanaweza kuwa na vimelea vya magonjwa kwenye kinyesi chao na kwenye miili yao, ikiwemo manyoya, miguu na midomo, hata kama wanaonekana kuwa na afya na safi.

Nawa mikono kwa sabuni na maji mara baada ya kumshika kuku au kugusa maeneo wanamoishi na kutembea. Watu wazima wanapaswa kuhakikisha watoto wadogo wanaosha mikono vizuri.
Back
Top Bottom