Kukosolewa. . . .

Dr Lizzy

Platinum Member
May 25, 2009
30,807
59,289
Kwanini kwenye jamii yetu watu hua wanapenda kuungwa mkono/kusifiwa hata pale wanachosema/fanya sio sahihi?

Nauliza kwasababu nimeona sana huku mitaani pia hapa JF. Yani mtu ukimkosoa anadhani/fikiri unamchukia, kwasababu tu hukubaliani na kile anachosema/amini. Je wewe mtu akikukosoa unachukia? Unadhani huyo mtu hakupendi?

Nasikitika kweli kuwa na watu wa aina hii kwenye jamii yetu maana kwa kutokua open minded and open to criticism wanapunguza wigo wa kujifunza. Mtu anapokukosoa/pinga unachojaribu kumweleza sio kwamba hakupendi bali anakupa wewe nafasi ya
kumcomvince/mweleza kwa undani kwanini unaamini
hicho unachosema hivyo chukua hiyo nafasi ya
kupanua uelewa wa huyo mtu mwingine from your point of view badala ya kununa.
 
BAdo una maumivu? Basi leo nakusamehe huendi twisheni angalia katuni na leo utakula chocolate.

Ndo ukubwa bado utagundua mengi, kuna siku nilikuambia "Kua uyaone"
 
Heeheh sawa mama. . .
Kuyaona kwenyewe ndo huku ehhh?Na kweli nimeyaona.
 
ni hulka tu nadhani. Wengine hujiona wao hawawezi kukosea na tena ndo ukute yule mwenye dharau, yaani yeye ana watu wake amesha waweka kwenye category ya maamuma, sasa subutu yako ukamkosoa utajuta!! (watu wa aina hii wao maoni yao tu ndo sahihi wanavodhani)

Kukataa kukosolewa ni upumbuvu, muungwana hupenda kukosolewa au hata kusikia maoni ya mwingine na huwezi jua utajifunza kitu.

BUT again Lizzy, kuna watu huwa wana tabia ya kukosoa kwa 'kukatisha tamaa', hao huwa hawana nia njema!
anyways, binafsi anayenikosoa naamini ananipenda na ananitakia mema...
 
Ha ha ha, zoea na jifunze kupotezea, zamani nilikuwa ivo kuja gundua ndo maisha yalivyo.
Nkapotezea, sasa ivi raha tupu, bado makazini ndo utakimbia kabisaa

Nimekusoma BHT. .
Kweli wanaokosea kwa nia ya kumkatisha mtu tamaa hata mimi sikubaliani nao. . . ila wanaonishangaza zaidi ni wale wasiotaka watu wengine watoe maoni yao ikiwa ni tofauti na yakwao.
 
Mie napenda kukosolewa manake naamini anaekukosoa anakupenda

lakini pia tusiwasahau wale wanaokosoa wenzao kwa kukatisha tamaa,au chuki binafsi. hii mara nyingi inachangiwa sana na wivu!
 
Ha ha ha, zoea na jifunze kupotezea, zamani nilikuwa ivo kuja gundua ndo maisha yalivyo.
Nkapotezea, sasa ivi raha tupu, bado makazini ndo utakimbia kabisaa
Sasa nipotezee kwa kutokukosoa na kukubaliana na kitu ambacho naona sio?Sidhani kama huo ni ujanja.Wao ndio wazoee kupingwa na kukosolewa bila kuchukulia personal.
 
Nimekusoma BHT. .
Kweli wanaokosea kwa nia ya kumkatisha mtu tamaa hata mimi sikubaliani nao. . . ila wanaonishangaza zaidi ni wale wasiotaka watu wengine watoe maoni yao ikiwa ni tofauti na yakwao.

watu wa hivo huwa 'hawakui', unaachana nao waendelee kuwa mbilikimo wa mawazo tu
 
Heeheh sawa mama. . .
Kuyaona kwenyewe ndo huku ehhh?Na kweli nimeyaona.

Lizzy we piga kitabu usiendekeze mambo ya hapa ambayo wakati mwingine yanaweza kabisa kukuacha mdomo wazi. Nakutakia mchana mwema katika kipande hicho cha dunia.
 
duuhh
Hivi bado tu hujazoea pole dadake
Hapa kuna watu ukiwasifia mtakuwa marafiki mpaka siku
ukimkosoa tena. :photo: copy na ku paste hii utaihitaji baadaye :bolt:
Kaaazi kweli kweli.
Nshaihifadhi hii for later use.
 
Nimekusoma BHT. .
Kweli wanaokosea kwa nia ya kumkatisha mtu tamaa hata mimi sikubaliani nao. . . ila wanaonishangaza zaidi ni wale wasiotaka watu wengine watoe maoni yao ikiwa ni tofauti na yakwao.
Hao Lizzy ndio tunawaeka kwenye kundi la malimbukeni manake wanaamini wako perfect kwenye kila kitu wakati hakuna aliye mkamilifu chini ya jua. Ukifahamu kuwa kila binadamu ameumbwa na madhaifu yake naamini kabisa hutachukia kukosolewa....manake hujakamilika!
 
Lizzy we piga kitabu usiendekeze mambo ya hapa ambayo wakati mwingine yanaweza kabisa kukuacha mdomo wazi. Nakutakia mchana mwema katika kipande hicho cha dunia.

Heheheheh asante BAK. . . ntapunguza kushangaa.
Na wewe nakutakia mwanzo mzuri wa siku.
 
Back
Top Bottom