Kukopeshana kunasababisha tupoteze sana Marafiki

Kukopeshana kunasababisha tupoteze sana Marafiki

Kuna jamaa yanhu n mzee wa zile "nikopeshe kesho kuna dili linatiki nakulipa".
Kipindi cha nyuma ilikua unaeza mkopesha, then anakuja kukulipa bar. Mnalewaa, af mwishon anakwambia, oya ile hela nliokulipa embu nigei tulipie hii bili iliobaki af kesho mchongo unatiki chap nakutoa.
Nkaja kuona ntakuja nimtwange vifuti vya meno ayameze awe anapigia mswaki kwenye kinyero.
So akawa akija kukopa kwa mfano 10, nampa dasi namwambia io usinilipe, we nenda. Baadae akaacha kukopa kabisa.
 
Watu wanapenda kukopa kulipa hawataki. Hii ni tabia mbaya.
Wakati anakuja kukopa alikuwa mpole kinoma ila sasa hivi anadiriki kunidanganya waziwazi. Ni afadhali hata angeniambia tu ukweli mahali alipo, lakini kitendo cha kunidanganya hata alipo kimenifedhehesha sana.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Wakuu habarini za wakati huu...

Moja kwa moja kwenye mada. Nimegundua kwamba moja ya sababu kubwa inayotufanya tupoteze marafiki zetu ni hii tabia ya kukopeshana. Sasa hivi nimejiwekea misimamo kabisa kwamba sitamkopesha mshkaji kama sina uwezo wa kumsamehe asiponilipa.

Yaani ni afadhali akija kunikopa basi nisimkopeshe bali nimsaidie tu. Kwasababu ukimkopesha ukawa na matarajio kwamba atakulipa halafu asipokulipa basi ni lazima urafiki wenu utaharibika. Lakini ukimkopesha halafu ukajiwekea moyoni kwamba akikulipa sawa, asipokulipa pia sawa, walau unaweza ukaunusuru urafiki wenu ikitokea hajakulipa kwasababu utakuwa umeshajiandaa kisaikolojia.

Leo ni tarehe 01/07 na mshkaji aliniahidi atalipa pesa yangu tarehe 26 mshahara ukitoka ila yupo kimya mpaka sasa, tunakutana, tunapiga story ila anavunga kama hakuna kilichotokea!

Nimekuja kujipumzisha kwenye Bar moja hapa Mikocheni namuona anaagiza tu pombe na ma-slay queen 2, kwasababu hajaniona nikamtext, "wapi mwana?", amejibu hivi, "My G, nipo maghetoni nimejilaza najitafuta, vipi nipe code basi".

Hajui namuona hapa. Halafu hii ni mara ya pili nakutana na scenario za namna hii kwa marafiki 2 tofauti. Anyway, acha iendelee kunyesha tuone panapovuja.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Kamsalimie
 
Na kwa nini umukopeshe rafiki,kama MTU ni rafiki yako unampa tu au unamwazima unamwambia siku ukiwa vyema utanirudishia.
Kama MTU ni rafiki yako unamjua akikuambia nitakurudishia siku Fulani basis wewe kua free mweleze rudisha siku ukiwa nayo,mkianza kuwekeana muda asipotimiza ndio yanakuwa mengine.
 
Hapana.

Kuna mshkaji alikuja kunililia, akaomba mkopo.

Mshkaji wa kweli kabisa tumetoka mbali.

Nikampa hela.

Kabla hajalipa akarudi tena akanililia nimuongeze.

Nikamuingeza.

Akapotea mazima.

Hata salamu anaona noma.

Hiyo ndiyo double decker, unaunganishiwa juu kwa juu.
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂 Oyaaa weeee..
Alikua anakuchukuliaje huyo...??

Mbona kakuchukulia kinyonge sana 😂😂😂
Soon inakuja triple
 
Mm neno sina nilifundishwa na baba yangu mzazi japo alinikuza kwenye kusaidia na kutambua shida za watu ila alichonambia ni kutotoa hela kwa mtu unaetaka kuendelea kuwa nae. Na kingine hakuna tuzo wala faida unapata ukikopesha masela au rafiki na muda mwingine marafiki wapo kwenye maisha yetu kwaajili ya vitu fulani.
 
Kuna jamaa yanhu n mzee wa zile "nikopeshe kesho kuna dili linatiki nakulipa".
Kipindi cha nyuma ilikua unaeza mkopesha, then anakuja kukulipa bar. Mnalewaa, af mwishon anakwambia, oya ile hela nliokulipa embu nigei tulipie hii bili iliobaki af kesho mchongo unatiki chap nakutoa.
Nkaja kuona ntakuja nimtwange vifuti vya meno ayameze awe anapigia mswaki kwenye kinyero.
So akawa akija kukopa kwa mfano 10, nampa dasi namwambia io usinilipe, we nenda. Baadae akaacha kukopa kabisa.
oya ile hela nliokulipa embu nigei tulipie hii bili iliobaki af kesho mchongo unatiki chap nakutoa.

Anakulipa then unakopwa hiyo hiyo ela [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Wakati anakuja kukopa alikuwa mpole kinoma ila sasa hivi anadiriki kunidanganya waziwazi. Ni afadhali hata angeniambia tu ukweli mahali alipo, lakini kitendo cha kunidanganya hata alipo kimenifedhehesha sana.

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Hao ndio binadamu bora uwe mbaya tuu kwenye masuala ya pesa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom