Kukopa na kutokulipa deni, Kama una tabia hii jitathimini sio nzuri kwani inapunguza uaminifu na kuvunja uhusiano pia

commm

JF-Expert Member
Sep 6, 2019
1,674
1,905
Mambo vipi wakuu

Kuna baadhi ya watu katika jamii tunayoishi, wengine ni ndugu, jamaa na rafiki zetu.

Huwa wanatabia ya kukopa na kutolipa deni kwa wakati au wengine kutolipa kabisa, na baada ya muda mtu anataka umkopeshe tena hali ya kuwa deni la mwanzo hajalipa.

Kiukweli hili jambo sio zuri kabisa, kwani mtu kutoa akiba yake kukupa wewe haimaanishi kwamba hana kazi nayo hiyo pesa bali ni roho ya utu na ubinadamu ndio maana akakukopesha wewe.

Sasa wewe tambua mpaka mtu inafikia hatua ya kukukopesha wewe jua na tambua kuwa amekuamini sana haijalishi ni ndugu yake au sio ndugu yake.

Kama una tabia hiyo acha mara moja.

Uzi tayari.
 
Watanzania Uaminifu ni tatizo kabisa.

Waliosema Uaminifu ni mtaji walikuwa sahihi 💯💯💯
 
Hali ya sasa ya uchumi imepelekea watu wengi kushindwa kurejesha madeni yao.
Hivyo wakopeshaji waendelee kuwa wavumilivu na staha.Vinginevyo watu watalogana na madeni hayatalipika
 
Back
Top Bottom