Focus120
JF-Expert Member
- Nov 10, 2014
- 1,090
- 786
Hellow Learned brothers and sisters. Naomba mnifahamishe maana ya kukazia hukumu kisheria , nimekuwa nikilisikia hili neno Mara kwa mara lakini sijui maana yake.
Katika kesi za madai (tofautisha na kesi za jinai) mahakama huwasikiliza wadaawa (wenye kesi) na baada ya kuwasikiliza hutoa hukumu kulingana na ushaidi.
Aliyeshinda kesi hupata kitu kinaitwa DECREE. Kwa hiyo yeye nakuwa DECREE HOLDER, aliyeshindwa anakuwa JUDGMENT DEBTOR (utanishamehe sababu maneno haya siyafahamu katika lugha ya kiswahili. DECREE HOLDER ataluhusiwa kufungua shauli jingine la kukaza hukumu katika mahakama (Applicatin for Execution of Decree).
Kisheria hii hatua inatakiwa ifanyika mda wowote ule lakini usizidi miaka 12. Mahakama itamuita JUDGMENT DEBTOR ili ajieleze kwa nini amri za kwenye hukumu (ambazo zinakuwa zimeainishwa kwenye DECREE) zisitekelezwe.
Mahakama ikilizika kwamba hakuna Rufaa iliyokatwa kupinga hukumu basi mahakama itaamuru hukumu itekelezwe (kukaza hukumu). hapa sasa mdaiwa (JUDGEMENG DEBTOR) atazimishwa kulipa deni analodaiwa au kuondoka sehemu asiyotakiwa kuwepo.
Hapa sasa mahakama inaweza kuteua madalali au wafilisi ili kumlazimisha JUDGMENT DEBTOR atekeleze amri za mahakama. Hii ndio inaitwa kukaza hukumu.