Elections 2010 Kukatishwa Kwa Matangazo Jangwani: Tido Mhando Alonga

Ha ha ha ama kweli CHADEMA ni wageni wa siasa za CCM ,yaani matangazo yamekatwa kidogo mnapiga makelele ,sizani kama mtaiweza mizengwe na mikakati ya Chama Tawala ? Mambo ndio kwanza ata CCM awajafungulia majibwa yao !!:lol:
Sasa unachoshangilia nini? Hamuwezi kushinda bila kuwabana wenzenu?
 
Mara ya kwanza Johnson Mbwambo alimchambua udhaifu wake wa kumuuliza kikwete maswali ya kishkaji nikadhani ana,wonea, sasa nimeanza kuona udhaifu wake laivu. Ni matusi yapi aliyotamka marando? alichofanya marando ni kutukumbusha tu ambayo tunayafahamu.

Huyu bwana huwezi kuamini kama ni mtu ambaye amefanya kazi BBC alikuwa akijionea mwenyewe jinsi David Cameron na Godon brown walivyokuwa wakichambuana , hakuna anayemsifia mwingine eti "kampeni ya kistaarabu" Kusema ukweli ndo kutokuwa mstaarabu?
 
Najua CCM Wasingependa neno Ufisadi likitamkwa hasa na wapinzania...Nilisikia Marando akizungumzia EPA sijui aliongelea na nini kingine maana TBC walifanya kazi yao..au Meremeta, Richmond ....
 

Tido Dunstan Mhando umjuaye wewe na mimi miaka ile kabla haja ondoka Tanzania kwenda Sauti ya Kenya Nairobi na hatimaye kujijengea jina kubwa kwenye anga za Kimataifa na kuwa mpaka Mkuu wa idhaa ya BBC siyo yeye yule wa leo. Tido Dunstan Mhando wa leo amelewa togwa la kifisisadi, kwani anazungumza kama wao na na anafanya kila kitu kama wao. Tido Dunstan Mhando wa leo amekubali kuwa kibaraka wa siasa kandamizi. Tido Dunstan Mhando wa leo ameamua kuisaliti taaluma. Sasa amekuwa kundi moja na mafisadi wengine waliokwisha jivunjia heshima za taaluma zao kama akina Salva Rweyemamu na wapuuzi wengine on the list.
 
Wana jamii kwani hamjui kuwa ni Jakaya Kikwete ndiye aliyempa kazi TIDO??? Jakaya amemsaidia TIDO kutoka kuishi ughaibuni UK, kwa hiyo ni lazima atii amri ya BOSS wake, tena siyo BOSS tu ni kuwa kamsaidia kampa kazi.
Naamini kuwa TIDO alipigiwa simu au aliamurishwaa na CCM azime TV haraka sanaaaaaaa, of course TIDO kama TIDO angetaka na angependa sana watanzania wajuwe jinsi CCM wanavyoibaaaaaa mahela yao, na mambo ya KISHENZI wanayofanya CCM, TIDO angetaka watanzania wafahamu, lakini hao majambazi wanaogopaa sana.
Watanzania wasikatishwe tamaa na ujinga na michezo ya kuigiza inayofanywa na CCM, iko siku kitaeleweka tuuu, kama siyo kwa KURA basi kwa BUNDUKI, maana CCM wameigeuza hii nchi ya kwao wanafanya wanachokitaka.
Mapambano yanaendelea mpaka kieleweke!!!
 

Nasikitika sikuwepo make ninge samasoti nikamramba teke, make kodi yangu ndo inaendesha TBC, iweje iwe ya watu fulani?
 
Kama mambo yenyewe ndo haya basi haina hata maana ya kwenda kupiga kura kwa sababu zitaibiwa tu na ntakuwa nimepoteza kura yangu.Vyombo vyote na tume zinaonekana zipo upande wa CCM.
 

Mkuu sana MMMJ,
JK aliwaita wapinzani kuwa ni FOTOKOPI na CCM ndio ORIJINO....Hili sio tusi?....na Mungu akamlaani kwa kutukana huku kafunga....Pwa akaanguka.....AISEE
 
Kwa akili na tafsiri ya TIDO na TBC1 mtu mstarabu ni yule anayeisifia CCM pamoja wa JK na kuwaponda wengine
 
Kilicho muharibia Tido Muhando ni kutumiliwa na CCM. Na unapotumiliwa mara zote huwa huna mwisho mwema. Ni kheri angebakia kule kule BBC ambako alikuwa tayari amesha jijengea. Alianza na kuziba harakati za CUF na 2005 na alidiriki hata kumuondosha Ally Saleh kutooka Zanzibr na kumleta Dar, kituu ambacho ni kinyume nyume kabisa. Ally Saleh amekuwa na BBC kwa muda mrefu na mtu ambaye anaeleweka zaidi Zanzibar na ni muandhishi pekee ambaye hana woga katika kazi yake. Sasa kumuondosha kwa siku za uchaguzi hapo kunatia mashaka!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…