Kukataliwa na wanawake wazuri

Kukataliwa na wanawake wazuri

Heshima kwenu wakuu,

Nimekuwa nikisumbuliwa na kasumba moja ili mbaya sana, maana kila mwanamke mwenye kuweza kutimiza haja zangu kila nikimtongoza lazima anikatae. Kwa mda sasa nimekuwa nikichagua machaguo yasiyo halali yangu na kuishia kuachana maana ninayempenda hanipendi mimi. Sasa najiuliza sijui ndo hii sura yangu iliyo na ukakasi wa kukataliwa ama sijui ni kitu gani.

Naombeni ushauri wenu maana imefikia mda nimechoka sasa, wanawake wanaonipenda mimi kwangu nawaona hawana mvuto kabisa, ila ninaemhitaji/kumpenda ndo kwanza hata salamu tu hataki.
nilizani hupendwi....kumbe napendwa ila we huwapendi...na unaowapenda wao hawakupendi..kawaida sana...tafuta hela tu..mapenzi yapo tu ukiyaendekeza utaumia...ukitulia utapendwa na wengi hadi utashangaa
 
Back
Top Bottom