Kukataliwa na wanawake wazuri

Kukataliwa na wanawake wazuri

EMMYGUY

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2015
Posts
11,115
Reaction score
25,415
Heshima kwenu wakuu,

Nimekuwa nikisumbuliwa na kasumba moja ili mbaya sana, maana kila mwanamke mwenye kuweza kutimiza haja zangu kila nikimtongoza lazima anikatae. Kwa mda sasa nimekuwa nikichagua machaguo yasiyo halali yangu na kuishia kuachana maana ninayempenda hanipendi mimi. Sasa najiuliza sijui ndo hii sura yangu iliyo na ukakasi wa kukataliwa ama sijui ni kitu gani.

Naombeni ushauri wenu maana imefikia mda nimechoka sasa, wanawake wanaonipenda mimi kwangu nawaona hawana mvuto kabisa, ila ninaemhitaji/kumpenda ndo kwanza hata salamu tu hataki.
 
siku zote binaadamu hawapendi vitu ambavyo ni too common kwao

hao wanawake wazuri wanakuona 'too common'

body language yako inaonesha tu 'unababaika' mno ukiwaona hao warembo

anza kujifunza kuwachukulia kawaida
Asante Mkuu The Boss kwa ushauri. Ngoja nianze kuwaona wa kawaida na kuwachukulia powa labda ninaweza kurudisha heshima.
 
Hapo ndo penye ugumu. Lakini ligi yangu si ya kitoto ujue.
. Watoto wazuri wanapenda (vitu vizuri) mboi ambae yupo ligi soo.
1. Muonekano upo bro?
2. pesa ipo?
3. Uvaaji vipi?
4. Ongea yako vipi?..sio unakua mlugaluga...ropokaropoka..poyoyo..mpayukaji...
5. Kwenye crue yako unatitle gani? Au wewe ndo kilaza

Watoto wazuri wanapenda vitu vizuri brother.
 
. Watoto wazuri wanapenda (vitu vizuri) mboi ambae yupo ligi soo.
1. Muonekano upo bro?
2. pesa ipo?
3. Uvaaji vipi?
4. Ongea yako vipi?..sio unakua mlugaluga...ropokaropoka..poyoyo..mpayukaji...
5. Kwenye crue yako unatitle gani? Au wewe ndo ******

Watoto wazuri wanapenda vitu vizuri brother.
Mkuu. Ngoja nianze upya kwa kuangalia kila sekta then nione itakavyokuwa.
 
Heshima kwenu wakuu,

Nimekuwa nikisumbuliwa na kasumba moja ili mbaya sana, maana kila mwanamke mwenye kuweza kutimiza haja zangu kila nikimtongoza lazima anikatae. Kwa mda sasa nimekuwa nikichagua machaguo yasiyo halali yangu na kuishia kuachana maana ninayempenda hanipendi mimi. Sasa najiuliza sijui ndo hii sura yangu iliyo na ukakasi wa kukataliwa ama sijui ni kitu gani.

Naombeni ushauri wenu maana imefikia mda nimechoka sasa, wanawake wanaonipenda mimi kwangu nawaona hawana mvuto kabisa, ila ninaemhitaji/kumpenda ndo kwanza hata salamu tu hataki.
ligi yako ni ya mchangani bado ujapanda jaraja ukipanda tu utawapata tu..kwa sasa cheza hukohuko mchangani..hahaha
 
Mkuu. Ngoja nianze upya kwa kuangalia kila sekta then nione itakavyokuwa.

umeshafeli

watoto wazuri wanapenda mtu ambae anaweza kuwa ignore
ukiwa nao jifanye kama huoni huo uzuri wao..
wakikupa namba usipige..kaa kimya kama wiki hivi
halafu ukipiga ni mara chache sana huku unaongea cha maana
sio kupiga kusalimia tu
 
Sampo yako inakuja kua na subira, labda nikulize unataka mwanamke wa Aina gan au awe na vigezo gan? Mana unasema usiowapenda ndio wanskungangania
 
Back
Top Bottom