Kukataliwa kwa Mkapa Burundi: Je, ni mwisho wa "ushawishi" wa TZ katika Siasa za Afrika?

barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Messages
6,394
Likes
27,425
Points
280
barafu

barafu

JF-Expert Member
Joined Apr 28, 2013
6,394 27,425 280
Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi.Bila shaka alikuwa Burundi kwa ajili ya kusuruhisha ule mgogoro wa Nkurunzinza na wenzake.Bahati mbaya safari hii Warundi wamemgomea na amerudi mikono mitupu.Hivyo kutokuwepo kwake katika sherehe za kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru si kwa sabbu "alisusia" bali alikuwa anatekeleza majukumu ya Tanzania katika siasa za Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu.

JK hakuwepo,naye alikuwa na safari nje ya nchi,msafara wake jana jioni ulitusimamisha wengi barabarani wakati akipita kurudi nyumbani.

Kutokuwepo kwao hakumaanishi lolote baya,zaidi ya wao kama marais wastaafu kutumikia jumuiya ya kimataifa kwa kutumia uzoefu wao wa uongozi katika kutatua mizozo na migogoro pamoja na kuhudumia Afrika ktk masuala mtambuka ya kidiplomasia.

Licha ya mapungufu yetu kama Taifa,licha ya kuwa na watu kama Jecha kule Znz na Lubuva huku Bara.Bado Tanzania nje ya mipaka ya nchi tuna heshima yetu.Hata baada ya nusu karne,ushawishi wetu ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere unavuka mlima Kilimanjaro na Ziwa Tanganyika,fukwe za Tanganyika na kando ya pili ya Ziwa Nyasa.Hii si kazi ya siku moja,ni juhudi za nusu karne,na walioipigania si wote wangali hai.

Ushawishi huu ulisimikwa na Julius;huyu hata baada ya kuondoka Ikulu aliogopeka ndani na nje ya nchi.Masaa kadhaa kwenye gereza la Kemwela-Kabwe Zambia,akiwa na sharubati ya chungwa (Orange juice)na biscuit,Nyerere alimfanya Kaunda kuacha kugoma kula na kunywa na kufungua "mfungo" wake alioufanya gerezani baada ya kuswekwa rumande na Chiluba.Wakati Nyerere akipanda ndege Lusaka kurudi Butiama,huku nyuma Chiluba alimfungulia Kaunda na kumtoa gerezani na kurudi nyumbani.Huu ni ushawishi unaovuka mipaka.Tuliaminiwa Burundi na Rwanda kuwaweka pamoja baada ya mauwaji ya kimbari.

Sasa tunakoelekea,tunaweza kuzalisha viongozi ambao hata "ushawishi" wao hauvuki kisiwa cha Chumbe ktk moja ya kina cha bahari ya Hindi, ushawishi usiovuka Ziwa Tanganyika kuelekea maziwa makuu.

Tutakosa watu wenye nguvu za ushawishi kuvuka Ziwa Nyasa na Pwani ya Afrika Mashariki.Nyakati hizo tulisimika Marais ktk nchi jirani na wakawa "vibaraka" wa Ikulu ya Dsm; kuanzia Ikulu ya Nakasere Uganda mpaka Bujumbura,Ututsi mpaka Moroni,eneo la Nampula mpaka Maputo ya Msumbiji.Tuliambaambaa kuanzia Lusaka mpaka Salisbury ya Zimbabwe na Windhoek.Wote hawa walikuwa "vijana" wetu tuliowakuza na kuwalea.

Leo kuna mtu kakataliwa huko Bujumbura;sababu anakosa "moral Authority" ya kukemea yale wanayotenda wengine sbb na yeye ana harufu ya yanayotendwa na yule anayelalamikiwa.Habari ya mtu anayeitwa Jecha inaweza kuwa na matokeo hasi ya muda mrefu katika ushawishi wetu wa siasa za kimataifa ndani na nje ya mipaka ya Afrika.

Unawezaje kumkemea Museveni kwa matendo yake kwa Kiiza Besigye wakati na wewe unayabariki kama hayo kwa wapinzani ndani ya nchi yako?Utamuwekaje meza moja Nkurunzinza na wapinzani wake wakati kwako hao wapinzani unaonekana kwenye youtube ukiwaita "mal.ofa na uchwara".

Huwezi kuwa na sauti kama ktk nchi yako wapinzani wa Serikali wananyimwa nafasi ya mikutano ya kisiasa na uhuru wa kutoa habari unadhibitiwa kwa sheria zilizotungwa na bunge (A law which is not just,is a useless law) na wewe umekaa kimya.

Wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Nyerere,upinzani wa Tanzania ulikuwa mikononi mwa Augustine Mrema na NCCR-Mageuzi,siku ya msiba ule pale Butiama na Mrema alifika,katika watu wa kuweka mashada ya mauwa,watu wa protokoli walimkacha Mrema wakidhani watamfurahisha Mwalimu,kwa ajabu Mwalimu alichukua shada moja na kumpelekea Mrema ili kuweka katika kaburi la Mama yake.Wale wote waliomkacha Mrema wakapatwa na aibu kubwa.

Wakati wa kupeana pole,Mrema alifika alipokaa Mwalimu na kumshika mkono wa pole,na baadae akahamia kwa aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Dr Alli Juma,na wakati wakiongea hili na lile,marehemu Dr Alli akajisemesha;"Huyu Augustino alikuwa rafiki yangu sana wakati akiwa serikalini",na Mwalimu akamuuliza Dr Alli;kwani sasa imekuwaje?Dr akajibu "Aa toka aende upinzani sina hamu nae tena"...Basi Mwalimu akamwambi "Aaa basi huyo hakuwa rafiki yako;angekuwa rafiki hata leo ungeendelea kumuona ni rafiki tu"

Katazo la Bujumbura si ishara njema kwa sisi kama Taifa;hata kama laweza kuwa katazo la "muda" tu,lakini ni taa ya tahadhari kuwa sasa ule "ushawishi" tuliokuwa nao enzi za Mwalimu na baada ya Mwalimu unaweza kuwa ktk eneo la mwisho wa enzi...Ni wapi tulipotereza??
 
jme

jme

JF-Expert Member
Joined
Aug 4, 2013
Messages
4,207
Likes
1,551
Points
280
jme

jme

JF-Expert Member
Joined Aug 4, 2013
4,207 1,551 280
Viongozi karibu wote wamepoteza ushawishi au legitimacy ndan na nje ya nchi
Jiulize ili uwe msuluhishi lazima na wewe uwe msafi jiulize ni nan kat yao ni msafi mwenye moral authority ya kuwaweka watu pamoja?
Angalia swala la zanzibar wangekuwa na hiyo credilibility wangeanza na hilo kwanza kabla ya kufikiri kusuluhisha mambo ya wengine
 
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2013
Messages
8,070
Likes
18,432
Points
280
M

MENGELENI KWETU

JF-Expert Member
Joined Oct 23, 2013
8,070 18,432 280
Na hawa wengine je?
Ni kama Wahuni tu.

Mkapa ni kati ya waliobariki uharamia aliofanya Jecha kwenye Uchaguzi wa Zbar.

Anapata wapi legality ya kwenda kusuluhisha mgogoro wa Burundi??

Mwl Nyerere wote hawa wenye matendo ya namna hii alikuwa anawaita WAHUNI.
 
Oxx

Oxx

JF-Expert Member
Joined
Jul 12, 2015
Messages
576
Likes
968
Points
180
Oxx

Oxx

JF-Expert Member
Joined Jul 12, 2015
576 968 180
Labda tungekua na Mfalme au Chama kimoja aya yote yasingetokea.
 
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Messages
57,943
Likes
54,912
Points
280
Erythrocyte

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined Nov 6, 2012
57,943 54,912 280
Adui yetu mkubwa ni yule aliyemteua Mkapa kuwa msuluhishi , alilenga kutudhalilisha .

Ni hivi , Tanzania kama nchi haina uwezo wa kusuluhisha migogoro ya kisiasa hata kwenye ngazi ya kata , achilia mbali nje ya nchi , bali kuna watu wawili tu ndani ya nchi hii wenye uwezo wa kuwa wasuluhishi , wote ni wazanzibar , nadhani kwa vile wote ni machotara .

Mmoja anaitwa Amani Karume na Mwingine anaitwa Salim Ahmed Salim , lakini hakuna mzee yeyote katika hawa wachumia tumbo na wanafiki waliojazana huko Tanganyika anayeweza kusuluhisha hata mgogoro wa ndoa , nadhani rangi nyeusi ni laana .
 
B

Babati

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Messages
31,760
Likes
25,214
Points
280
Age
33
B

Babati

JF-Expert Member
Joined Aug 7, 2014
31,760 25,214 280
Msuluhishi alikuwa Mandela wengine muuuuu
 
U

Undu

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2013
Messages
1,947
Likes
265
Points
180
U

Undu

JF-Expert Member
Joined May 18, 2013
1,947 265 180
Naona kwa hili sina hamu na Huyu bwana
 
lukindo

lukindo

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2010
Messages
8,167
Likes
6,620
Points
280
lukindo

lukindo

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2010
8,167 6,620 280
Nimesikitika sana nilivyosikia BBC Focus in Africa akiwaita wanaomkataa Nkurunzinza wapumbavu!
Kiukweli wanaweza wakawa wapumbavu lakini ndio walio wengi na kura zao zilikuwa nyingi pia kabla hazijapinduliwa. Ukienda mbele zaidi ni kwamba watu hawa hawa wamekubali kukaa meza moja kuyamaliza na wewe umeaminiwa kama msuluhisi hivyo huna budi kuwasikiliza badala ya kuwakatisha tamaa na kuwatukana. Naamini Nelson Mandela kukaa gerezani miaka 27 na baadae akatolewa huku idadi kubwa ya watu ikimuunga mkono kwenda Ikulu lazima watesaji wake walijua ni 'mkorofi' na 'mpumbavu'!
 
Mo-TOWN

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2010
Messages
1,735
Likes
229
Points
160
Mo-TOWN

Mo-TOWN

JF-Expert Member
Joined Oct 11, 2010
1,735 229 160
Benjamin Mkapa alikuwa nje ya nchi.Bila shaka alikuwa Burundi kwa ajili ya kusuruhisha ule mgogoro wa Nkurunzinza na wenzake.Bahati mbaya safari hii Warundi wamemgomea na amerudi mikono mitupu.Hivyo kutokuwepo kwake katika sherehe za kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru si kwa sabbu "alisusia" bali alikuwa anatekeleza majukumu ya Tanzania katika siasa za Afrika Mashariki na Nchi za Maziwa Makuu.

JK hakuwepo,naye alikuwa na safari nje ya nchi,msafara wake jana jioni ulitusimamisha wengi barabarani wakati akipita kurudi nyumbani.

Kutokuwepo kwao hakumaanishi lolote baya,zaidi ya wao kama marais wastaafu kutumikia jumuiya ya kimataifa kwa kutumia uzoefu wao wa uongozi katika kutatua mizozo na migogoro pamoja na kuhudumia Afrika ktk masuala mtambuka ya kidiplomasia.

Licha ya mapungufu yetu kama Taifa,licha ya kuwa na watu kama Jecha kule Znz na Lubuva huku Bara.Bado Tanzania nje ya mipaka ya nchi tuna heshima yetu.Hata baada ya nusu karne,ushawishi wetu ulioasisiwa na Mwalimu Nyerere unavuka mlima Kilimanjaro na Ziwa Tanganyika,fukwe za Tanganyika na kando ya pili ya Ziwa Nyasa.Hii si kazi ya siku moja,ni juhudi za nusu karne,na walioipigania si wote wangali hai.

Ushawishi huu ulisimikwa na Julius;huyu hata baada ya kuondoka Ikulu aliogopeka ndani na nje ya nchi.Masaa kadhaa kwenye gereza la Kemwela-Kabwe Zambia,akiwa na sharubati ya chungwa (Orange juice)na biscuit,Nyerere alimfanya Kaunda kuacha kugoma kula na kunywa na kufungua "mfungo" wake alioufanya gerezani baada ya kuswekwa rumande na Chiluba.Wakati Nyerere akipanda ndege Lusaka kurudi Butiama,huku nyuma Chiluba alimfungulia Kaunda na kumtoa gerezani na kurudi nyumbani.Huu ni ushawishi unaovuka mipaka.Tuliaminiwa Burundi na Rwanda kuwaweka pamoja baada ya mauwaji ya kimbari.

Sasa tunakoelekea,tunaweza kuzalisha viongozi ambao hata "ushawishi" wao hauvuki kisiwa cha Chumbe ktk moja ya kina cha bahari ya Hindi, ushawishi usiovuka Ziwa Tanganyika kuelekea maziwa makuu.

Tutakosa watu wenye nguvu za ushawishi kuvuka Ziwa Nyasa na Pwani ya Afrika Mashariki.Nyakati hizo tulisimika Marais ktk nchi jirani na wakawa "vibaraka" wa Ikulu ya Dsm; kuanzia Ikulu ya Nakasere Uganda mpaka Bujumbura,Ututsi mpaka Moroni,eneo la Nampula mpaka Maputo ya Msumbiji.Tuliambaambaa kuanzia Lusaka mpaka Salisbury ya Zimbabwe na Windhoek.Wote hawa walikuwa "vijana" wetu tuliowakuza na kuwalea.

Leo kuna mtu kakataliwa huko Bujumbura;sababu anakosa "moral Authority" ya kukemea yale wanayotenda wengine sbb na yeye ana harufu ya yanayotendwa na yule anayelalamikiwa.Habari ya mtu anayeitwa Jecha inaweza kuwa na matokeo hasi ya muda mrefu katika ushawishi wetu wa siasa za kimataifa ndani na nje ya mipaka ya Afrika.

Unawezaje kumkemea Museveni kwa matendo yake kwa Kiiza Besigye wakati na wewe unayabariki kama hayo kwa wapinzani ndani ya nchi yako?Utamuwekaje meza moja Nkurunzinza na wapinzani wake wakati kwako hao wapinzani unaonekana kwenye youtube ukiwaita "mal.ofa na uchwara".

Huwezi kuwa na sauti kama ktk nchi yako wapinzani wa Serikali wananyimwa nafasi ya mikutano ya kisiasa na uhuru wa kutoa habari unadhibitiwa kwa sheria zilizotungwa na bunge (A law which is not just,is a useless law) na wewe umekaa kimya.

Wakati wa msiba wa Mama Mzazi wa Nyerere,upinzani wa Tanzania ulikuwa mikononi mwa Augustine Mrema na NCCR-Mageuzi,siku ya msiba ule pale Butiama na Mrema alifika,katika watu wa kuweka mashada ya mauwa,watu wa protokoli walimkacha Mrema wakidhani watamfurahisha Mwalimu,kwa ajabu Mwalimu alichukua shada moja na kumpelekea Mrema ili kuweka katika kaburi la Mama yake.Wale wote waliomkacha Mrema wakapatwa na aibu kubwa.

Wakati wa kupeana pole,Mrema alifika alipokaa Mwalimu na kumshika mkono wa pole,na baadae akahamia kwa aliyekuwa Makamu wa Rais marehemu Dr Alli Juma,na wakati wakiongea hili na lile,marehemu Dr Alli akajisemesha;"Huyu Augustino alikuwa rafiki yangu sana wakati akiwa serikalini",na Mwalimu akamuuliza Dr Alli;kwani sasa imekuwaje?Dr akajibu "Aa toka aende upinzani sina hamu nae tena"...Basi Mwalimu akamwambi "Aaa basi huyo hakuwa rafiki yako;angekuwa rafiki hata leo ungeendelea kumuona ni rafiki tu"

Katazo la Bujumbura si ishara njema kwa sisi kama Taifa;hata kama laweza kuwa katazo la "muda" tu,lakini ni taa ya tahadhari kuwa sasa ule "ushawishi" tuliokuwa nao enzi za Mwalimu na baada ya Mwalimu unaweza kuwa ktk eneo la mwisho wa enzi...Ni wapi tulipotereza??
Mkapa yupi yule aliosema watanzania ni wapumbavu??? Ningeshangaa sana kukubalika Burundi....ingewezekana vipi mpumbavu kusuluisha mgogoro
 
Forum statistics

Threads 1,272,592
Members 490,036
Posts 30,454,577