Kukamatwa, kupigwa risasi Lissu: Chama cha Wanasheria Uingereza chamlima barua Rais Magufuli

Waambieni hao mabwana wa Uingereza Lissu haitaji barua Lissu anahitaji matibabu wangemchukua wakampa matibabu ya uhakika huko uingereza watakua wamesaidia sio hizi ngonjera
Kwani waliompiga Risasi mbona haujawaambia kumtibu,Apigwe Risasi na wengine matibabu uhusishe wengine.
Waliompiga risasi wanakula bata hapo wengine wanazurura kule Arusha mbona hauwatolei mimacho?
 
Upuuzi mtupu nimeanza amini Hii ni vita ya kiuchumi lakini kwa upuuzi huu ndio utatufanya tuwe imara zaidi na kubuni mbinu nzuri zaidi za kupaa kiuchumi
Lazima uwe taahira hasa kuamini kuwa unaweza kupaa kiuchumi kwa kwenda kinyume na Dunia. Kati ya mambo yanayoweza kukufanya uonekane hopeless kabisa ni pale unaposhindwa kutekeleza hata uliyoyaahidi mwenyewe.

Sisi kama nchi tumetia saini mikataba mbalimbali inayohusiana na maisha ya binadamu, halafu bila aibu tunakiuka. Tunapokumbushwa, kwa wendawazimu mkubwa tunajifanya vichwa maji. Kama nchi tunatakiwa kujitafakari, na kuchukua hatua, ambazo kiuhalisia zinatusaidia sisi wenyewe.

Kwa sasa Tanzania haiwezi kushinda vita yoyote kwa sababu wananchi wamegawanyika. Wapo wanaoshabikia siasa na uongozi wa kibabe na wale wanaounga mkono utawala wa kistaarabu, unaolinda misingi ya utu wa binadamu. Hawa wawili hawawezi kushikamana.
 
Informer mambo mengine muwe mnatusaidia sisi Kayumba bwanaa....na ukayumba wangu nimefikiri hii imeandaliwa tuu na watu fulani...eti nimeangalia imeandikwa "FROM THE PRESIDENT" Halafu ikaandikwa adress ya presidaa wa TZ, Sasa kwa ukilaza wangu nimefikiri imetoka KWA PRESIDAA WA TZ,KULIA NI ADRESS YAO WAZUNGU Nilikuwa eti najua kushoto ni adress yetu kwa hivyo wataandika "TO THE TZ PRESIDENT...Huu ujinga wangu huu nahitaji kufundishwa...
 
wazungu ni wanafiki sana. kesho utasikia uingereza yatoa misaada kwa tanzania. kama wanaume wapige marufuku kiongozi yeyote wa serikali kukanyaga ulaya.
Rwanda kila Siku Watu wanapigwa Chuma wakileta U maku maku, Kenya kapigwa Chuma Mkuu wa ICT wa Tume
Kama vikwazo angeanza kuwekewa Kagame!

Ethiopia kuanzia ya Meles Zenawi mpaka ya Sasa Watu wanapigwa Vyuma vya kichwa wakileta Udwanzi the same to Eritrea lakin Maisha yanaendelea!

Huko Africa ya Kati ndio usiseme kwa Ubabe, Wazungu wanajua haya Mambo kwa Africa ni ya kawaida sana sana
 
Waambieni hao mabwana wa Uingereza Lissu haitaji barua Lissu anahitaji matibabu wangemchukua wakampa matibabu ya uhakika huko uingereza watakua wamesaidia sio hizi ngonjera
Mnaonywa kwani mnaleta kiburi kwa misaada yao, unapoona Mwingireza ameongea, ujue nchi zoote za Ulaya nazo hazitaenda kinyume naye, na Usa lazima naye atatia neno.
Hii siyo dalili njema, mkumbuke Wazungu hutafuta sababu ya kukuletea vikwazo, so hili silo la kubeza labda mpumbavu pekee
 
Back
Top Bottom