Mbege
Member
- Oct 27, 2013
- 61
- 32
Wana JF, ushauri unahitajika. Nimeoa kwa muda wa miaka 7 sasa mke wangu ni kutoka kanda ya ziwa, kwamuda wote huo sikuwahi kukaa na ndugu wa mke wangu hata mmoja zaidi ya mimi kuwatembelea wao kuko kwao na kurudi. Hivi karibuni amekuja mdogo wa mke wangu mwanaume yeye hajaoa na hana kazi.
Ni muda wa miezi mitatu sasa yuko kwangu na nilitegemea kuja kwake ni kwa muda tu kusalimia na kuondoka. Hivi sasa nimekuwa nikikwazika sana hasa baada ya kuzoea hapa nyumbani kwangu, kwanza nirudipo nyumbani namkuta yuko jikoni na dada yake wanapiga stori muda wote hata siku nikiwa sijaenda kwenye misele kutwa ni yeye na dada yake tu.
Pili mke wangu amekuwa akifanya mambo mengi naye bila kunishirikisha kabisa mfano, amemtafutia kibarua mahali bila mimi kujua, na shemeji mwenyewe hayawahi kuniambia, tatu anaweza akaondoka kwenda kwa jamaa zake wengine wa kutoka kwao waliopo mji ninaoishi na kulala huko bila hata ya kuniaga mimi ni dada yake tu. Nne amekuwa akitoa amri hata kwa watoto wangu na dada wa kazi kwa kuwakoromea.
Mke wangu kwa sasa hana mda na mimi kabisa ni yeye na mdogo wake tu, hata chakula anaweza akapewa yeye kabla hata ya watoto na hata mimi pia. Jamani hiii imekaaje, au ni mimi mwenye tatizo? Ninampango wa kumwambia huyu shemeji aende zake alikotoka.
Semeni waungwana