Nikupateje
JF-Expert Member
- Dec 22, 2009
- 1,334
- 988
Wakuu,
Naona watanzania tumeamua kutumbukiza akili yetu kwenye imani moja ya ajabu. Imani kwamba matokeo ya vituoni yatatangazwa na kubandikwa vituoni lakini matokeo ya jumla Tume ndiyo yenye haki ya kuyatangaza.
Hii lugha mimi inashindwa kuingia akilini kwani kutangazwa kwa kitu ni kukiweka wazi ili kila mmoja akione ama kwa mdomo au kwa maandishi. Kituoni yametangazwa kwa maandishi. Tanzania ina vituo zaidi ya 50,0000.
Binafsi nikitembea ninaweza kuishia kuona vituo vine tu. Mwenye pikipiki au gari anaweza kuona hata 20.
Tume itaona matokeo yote kwani karatasi zilizoandika matokeo zinapelekwa huko zote. Mimi sintaona yote kwani uwezo wangu ni kutembea vituo vichache.
Ninachojua ni kwamba kila wakala anapewa kopi ya voucher ya matokeo ya kila chama na voucher hiyo imesainiwa na vyama vyote.
Baada ya hapo ukweli kinachofuata si kutangaza bali ni kujumlisha matokeo yaliyotangazwa tayari vituoni.
Haki ya kujumlisha na kupata jibu sahihi ni ya kila mmoja duniani. Kumbe matokeo ya jimbo mtu angeweza kupata idadi ya kila kituo halafu yeye hata asisumbuke kuyajumlisha na badala yake akampa motto wake aliye darasa la nne amjumlishie na hata darasa la tau au la pili.
Tumeona magazeti yakifukua ufisadi mwingi serikalini huku yakionyesha photocopy ya documents zilizosaini ufisadi huo. Leo magazeti kwenda kwenye chama kinachodhani kitadhulumiwa na kuomba photocopy ya voucher za matokeo ya kila kituo halafu yajumlishe yenyewe.
Hakuna haja ya kuweka gazetini photocopy za voucher zile kwani jimbo linaweza kuwa na vituo 400. Lakini kama kweli gazeti limekusanya copy zote hizo basi ni kiasi cha kusema gazeti lao limeweka matokeo ya jibo zima na lina ushahidi wa karatasi za matokeo yaliyosainiwa kituoni, na anayebisha aende mahakamani!
Labda nimezembea lakini sijaona gazeti au website . Magazeti wameweza kufanya hivyo kwa matokeo ya mitihani lakini sijui wameshindwa nini kwenye hili la matokeo ya vituo vyote majimboni.
Gazeti likitangaza idadi katika vuto basi likijitahidi ni vituo 20 tu wakati jimbo lina vituo zaidi ya 100. Ulitegemea walau gazet liwe na toleo maalumu kwa ajili ya matokeo kwani vituo ni vingi.
Ndiyo sababu tunapata taabu hii ya sasa. Mtu anasema mgombea fulani sasa anapumulia mashine. Ukiulizwa lete data ya zinaanza porojo nyingi wakati hapo ndipo chance ya kutuonyesha anavyopumulia mashine kwa kutaja matokeo ya kila kituo!
Ok. Tusema tuna wasiwasi tume inachakachua. Sijashiriki siasa. Mlioshiriki hebu tufundisheni miujiza inayofanyika kuwa tume-saini matokeo vituoni, gazete limeorodheshaa vituo vyote jimboni likiwa na ushahidi wa photocopy zile.
Pale kwenye majumuisho, mmejulisha vyote na wananchi wamejumlisha. Hesabu ya kujumlisha haileti majibu tofauti hata ingefanywa na genious wa dunia hii au ifanywe na mwanafunzi wa darasa la nne.
Kuchakachua pekee kulikobaki ni kutangaza jumla tofauti, tena tofauti nay a kituoni, tofauti nay ale yenye signature za voucher kituoni na hivyo tofauti na popote pale photocopy za voucher zilipoenda
Hadi sasa na hata humu JF hatuna hata jimbo rekodi ya jimbo inayoonyesha kituo kwa kituo. Badala yake tunapokea matokea kwa walau kwa ngazi ya kata lakini mengi kwa ngazi ya jimbo.
Tungekuwa na matokeo ya kila kituo sanasana utani hapa JF ingekuwa kuchekana fulani hajui kujumlisha, mpe chekechea akusaidie.
Mimi ninaliona tatizo hili si dogo. Kama watanzania tunashindwa biashara ndogo ya kujumlisha kituo kwa kituo ni biashara gani tutaiweza. Majuzi tumebisha demographic data kwamba haiwezekani Tanzania iwe na watu kiasi fulani kutoka sense iliyopita.
Kweli hatujafanya sense hivi karibuni lakini kutetea hoja za sasa ni lazima uwe umefanya mesabu makali yaitwayo extraporlation. Yapo mengine yana vitu initwa Permutation, Combination na mengine huitwa exponential.
Kama tuliweza kubisha kwa vitu vyenye mahesabu magumu yale ni maajabu gani tusibishane kwa hesabu rahisi ya kujumlisha ambayo unaweza kumpa mtoto akufanyie.
Sijaona chama hata kimoja chenye website inayotoa live update kwa kila kituo.
Niko wazi naipenda CHADEMA na nimepekua website yao hii {www.chadema.or.tz}. Ndugu zangu hawa wanapata kopi ya kila kituo lakini sioni page yoyote kuhusu hata matokeo ya jumla achilia mbali matokeo ya jimbo na kitaifa.
Pia nimetembelea website ya CCM {www.cms.ccmtz.org}. Eti hawa CCM tumejikuta tumewapa hadhi ya u-professa wa uchakachuaji hapa duniani wakiwazidi wengine wote duniani. Hivy naweza kusema website yao hawataweka matokeo live ya kituo kwa kituo ili wachakachue vizuri.
Nimenunu gazet la TANZANIA Daima la jana nikamefurahi kuona matokeo ya IRINGA MJINI kituo kwa kituo. Lakini furaha yangu haikuenda mbali kwani haikuzidi vituo 20 tena vyote ni vile ambavyo tulivijadili humu JF usiku wakati yanaendelea kutoka vituoni.
Nikaambiwa MWANANCHI wanatoa update kwenye website yao. Kumbe hata huko inatoka kuanzia level ya jimbo tena majimbo mengi hukuti idadi bali unaona pie chart inayoonyesha KIKWETE anaongoza kwa 64% hadi jana.
Nilileta sheet inayojumlisha kila kitu kwenye thread hii { https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/81684-matokeo-ya-uchaguzi-yawekwe-hapa.html}, wewe unaingiza data tu. Hatuitumii.
Hebu wazoefu wanisaidie kimawazo maana naamini tuko wengi tunaojiuliza hivi. Narudia, ninaipenda CHADEMA, sitaki idhulumiwe lakini hebu nifundisheni wenye uzoefu, ni nini kinatokea pale majumuishoni hadi tuambukizne wasiwasi.