Elections 2010 Kujumlisha matokeo kunatushinda, tuweze nini duniani?

Nikupateje

JF-Expert Member
Dec 22, 2009
1,334
988
Wakuu,

Naona watanzania tumeamua kutumbukiza akili yetu kwenye imani moja ya ajabu. Imani kwamba matokeo ya vituoni yatatangazwa na kubandikwa vituoni lakini matokeo ya jumla Tume ndiyo yenye haki ya kuyatangaza.

Hii lugha mimi inashindwa kuingia akilini kwani kutangazwa kwa kitu ni kukiweka wazi ili kila mmoja akione ama kwa mdomo au kwa maandishi. Kituoni yametangazwa kwa maandishi. Tanzania ina vituo zaidi ya 50,0000.

Binafsi nikitembea ninaweza kuishia kuona vituo vine tu. Mwenye pikipiki au gari anaweza kuona hata 20.

Tume itaona matokeo yote kwani karatasi zilizoandika matokeo zinapelekwa huko zote. Mimi sintaona yote kwani uwezo wangu ni kutembea vituo vichache.

Ninachojua ni kwamba kila wakala anapewa kopi ya voucher ya matokeo ya kila chama na voucher hiyo imesainiwa na vyama vyote.

Baada ya hapo ukweli kinachofuata si kutangaza bali ni kujumlisha matokeo yaliyotangazwa tayari vituoni.

Haki ya kujumlisha na kupata jibu sahihi ni ya kila mmoja duniani. Kumbe matokeo ya jimbo mtu angeweza kupata idadi ya kila kituo halafu yeye hata asisumbuke kuyajumlisha na badala yake akampa motto wake aliye darasa la nne amjumlishie na hata darasa la tau au la pili.

Tumeona magazeti yakifukua ufisadi mwingi serikalini huku yakionyesha photocopy ya documents zilizosaini ufisadi huo. Leo magazeti kwenda kwenye chama kinachodhani kitadhulumiwa na kuomba photocopy ya voucher za matokeo ya kila kituo halafu yajumlishe yenyewe.

Hakuna haja ya kuweka gazetini photocopy za voucher zile kwani jimbo linaweza kuwa na vituo 400. Lakini kama kweli gazeti limekusanya copy zote hizo basi ni kiasi cha kusema gazeti lao limeweka matokeo ya jibo zima na lina ushahidi wa karatasi za matokeo yaliyosainiwa kituoni, na anayebisha aende mahakamani!

Labda nimezembea lakini sijaona gazeti au website . Magazeti wameweza kufanya hivyo kwa matokeo ya mitihani lakini sijui wameshindwa nini kwenye hili la matokeo ya vituo vyote majimboni.
Gazeti likitangaza idadi katika vuto basi likijitahidi ni vituo 20 tu wakati jimbo lina vituo zaidi ya 100. Ulitegemea walau gazet liwe na toleo maalumu kwa ajili ya matokeo kwani vituo ni vingi.

Ndiyo sababu tunapata taabu hii ya sasa. Mtu anasema “mgombea fulani sasa anapumulia mashine”. Ukiulizwa lete data ya zinaanza porojo nyingi wakati hapo ndipo chance ya kutuonyesha anavyopumulia mashine kwa kutaja matokeo ya kila kituo!

Ok. Tusema tuna wasiwasi tume inachakachua. Sijashiriki siasa. Mlioshiriki hebu tufundisheni miujiza inayofanyika kuwa tume-saini matokeo vituoni, gazete limeorodheshaa vituo vyote jimboni likiwa na ushahidi wa photocopy zile.

Pale kwenye majumuisho, mmejulisha vyote na wananchi wamejumlisha. Hesabu ya kujumlisha haileti majibu tofauti hata ingefanywa na genious wa dunia hii au ifanywe na mwanafunzi wa darasa la nne.

Kuchakachua pekee kulikobaki ni kutangaza jumla tofauti, tena tofauti nay a kituoni, tofauti nay ale yenye signature za voucher kituoni na hivyo tofauti na popote pale photocopy za voucher zilipoenda

Hadi sasa na hata humu JF hatuna hata jimbo rekodi ya jimbo inayoonyesha kituo kwa kituo. Badala yake tunapokea matokea kwa walau kwa ngazi ya kata lakini mengi kwa ngazi ya jimbo.

Tungekuwa na matokeo ya kila kituo sanasana utani hapa JF ingekuwa kuchekana “fulani hajui kujumlisha, mpe chekechea akusaidie”.

Mimi ninaliona tatizo hili si dogo. Kama watanzania tunashindwa biashara ndogo ya kujumlisha kituo kwa kituo ni biashara gani tutaiweza. Majuzi tumebisha demographic data kwamba haiwezekani Tanzania iwe na watu kiasi fulani kutoka sense iliyopita.

Kweli hatujafanya sense hivi karibuni lakini kutetea hoja za sasa ni lazima uwe umefanya mesabu makali yaitwayo “extraporlation”. Yapo mengine yana vitu initwa Permutation, Combination na mengine huitwa exponential.

Kama tuliweza kubisha kwa vitu vyenye mahesabu magumu yale ni maajabu gani tusibishane kwa hesabu rahisi ya kujumlisha ambayo unaweza kumpa mtoto akufanyie.

Sijaona chama hata kimoja chenye website inayotoa live update kwa kila kituo.

Niko wazi naipenda CHADEMA na nimepekua website yao hii {www.chadema.or.tz}. Ndugu zangu hawa wanapata kopi ya kila kituo lakini sioni page yoyote kuhusu hata matokeo ya jumla achilia mbali matokeo ya jimbo na kitaifa.

Pia nimetembelea website ya CCM {www.cms.ccmtz.org}. Eti hawa CCM tumejikuta tumewapa hadhi ya u-professa wa uchakachuaji hapa duniani wakiwazidi wengine wote duniani. Hivy naweza kusema website yao hawataweka matokeo live ya kituo kwa kituo ili wachakachue vizuri.

Nimenunu gazet la TANZANIA Daima la jana nikamefurahi kuona matokeo ya IRINGA MJINI kituo kwa kituo. Lakini furaha yangu haikuenda mbali kwani haikuzidi vituo 20 tena vyote ni vile ambavyo tulivijadili humu JF usiku wakati yanaendelea kutoka vituoni.

Nikaambiwa MWANANCHI wanatoa update kwenye website yao. Kumbe hata huko inatoka kuanzia level ya jimbo tena majimbo mengi hukuti idadi bali unaona pie chart inayoonyesha KIKWETE anaongoza kwa 64% hadi jana.

Nilileta sheet inayojumlisha kila kitu kwenye thread hii { https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/81684-matokeo-ya-uchaguzi-yawekwe-hapa.html}, wewe unaingiza data tu. Hatuitumii.

Hebu wazoefu wanisaidie kimawazo maana naamini tuko wengi tunaojiuliza hivi. Narudia, ninaipenda CHADEMA, sitaki idhulumiwe lakini hebu nifundisheni wenye uzoefu, ni nini kinatokea pale majumuishoni hadi tuambukizne wasiwasi.
 
Unajua Watanzania tumekuwa tunalea ujinga kwa muda mrefuu. Sasa tunalea upumbavu. Unajua umasikini wa fikra ni umasikini mkubwa kuliko wote. Brazil yenye watu 200 milioni wamepiga kura jana na le wanajua Rais wao. Sisi jimbo tu mbinde. Huu ni upumbavu. Halafu tunakuja kutisha watu na vi-degree na vi-Phd vya kina Jakaya. Mi Doctor, Mi Doctor, ujinga tu. Wasomi Tanzania wengi hawajaelimika. Mbali na Permutation na Combination za Probability kuna mengi zaidi ya hayo katika dunia. Watanzania wanadanganywa na viongozi wa dini kwa visingizio vya amani lakini viongozi wa dini hawashinikizi CCM na serikali kuweka mazingira ya Haki. Usishangae kesho viongozi wa dini wamealikwa kwenye "Chakula cha Mchana." Hawa watu ni wanafiki tu. kwa kupitia watu kama hawa CCM inachakachua halafu wao wanalainisha vijana. Huu upumbavu hautakubalika. Nakubali watu watofautiane na mimi, ila mimi binafsi sitakubali kusaidiwa kufikiri nitafikiri kwa akili ya ngu mwenyewe. Mungu ibariki Tanzania.
 
Ni kweli kabisa wakuu, unajua in simple terms ilitakiwa mfano kunakuwa na live update kwenye TV (Matokeo kutoka vituoni), Tv stations kushirikiana na vyama vya siasa. Kila kituo, kila jimbo, mkoa etc. Hii ni possible na wala hatuhitaji kusubiri nchi yetu ije kuwa kama Marekani kutekeleza hili. Pili Tume pia ilitakiwa iwe live on TV, hatua kwa hatua wakituonyesha nini wanafanya na nini kinaendelea. Lakini unakuta matokeo inakuwa kama ni siri ya usalama wa taifa it is just absurd.

As a learning curve hao wazee kwenye tume wangeondolewa, wawe kama advisors tu. They have failed us miserably and not one time.
 
Hivi unadhani kunatushinda? Hapo ndo wanapopatiaga kura za pembeni. Bila hivyo itakuwa ngumu kuoanisha maana utajikuta umeingiza nyingi kuliko so inabidi polepole ili kubalansisha. CCM bana mh.
 
Unajua Watanzania tumekuwa tunalea ujinga kwa muda mrefuu. Sasa tunalea upumbavu. Unajua umasikini wa fikra ni umasikini mkubwa kuliko wote. Brazil yenye watu 200 milioni wamepiga kura jana na le wanajua Rais wao. Sisi jimbo tu mbinde. Huu ni upumbavu. Halafu tunakuja kutisha watu na vi-degree na vi-Phd vya kina Jakaya. Mi Doctor, Mi Doctor, ujinga tu. Wasomi Tanzania wengi hawajaelimika. Mbali na Permutation na Combination za Probability kuna mengi zaidi ya hayo katika dunia. Watanzania wanadanganywa na viongozi wa dini kwa visingizio vya amani lakini viongozi wa dini hawashinikizi CCM na serikali kuweka mazingira ya Haki. Usishangae kesho viongozi wa dini wamealikwa kwenye "Chakula cha Mchana." Hawa watu ni wanafiki tu. kwa kupitia watu kama hawa CCM inachakachua halafu wao wanalainisha vijana. Huu upumbavu hautakubalika. Nakubali watu watofautiane na mimi, ila mimi binafsi sitakubali kusaidiwa kufikiri nitafikiri kwa akili ya ngu mwenyewe. Mungu ibariki Tanzania.

Nakubaliana na nikupateje kuwa vyombo vya habari navyo pia vimekosa ubunifu, kwa maana ya kuwa kutaja kura zilizohesabiwa vituoni si kutangaza mataokeo ni kuhabarisha.
Nyambala, ni kweli wasomi wetu nao wanasehemu yao, kwa sababu hali kama hii walitakiwa wawe wanaijua mapema na watafute njia mbadala wa kkukwepa ukiritimba wa habari. Wasomi wetu wengi wanatetea vitumbua vyao kuliko keki ya taifa, ndiyo maana Makamba anweza kuwaambia acheni mdahalo na wakafyata, si diwani, si mbunge au yoyote.
Kwa upande wa tume ya uchaguzi, ni vituko vitupu, mwenyekiti ambaye ni msomi yupo madarakani kwa miaka 5 akilipwa stahiki na marupurupu yote. Eti leo tume haijui ni kituo gani kina watu wangapi hadi washindwe kupeleka karatasi. Swali ni kuwa miaka 5 iliyopita walikuwa wanafanya kazi gani? Bila kuuma maneno uhuru wa tume hii ni wa kutilia mashaka, na hili ni jambo la kwanza wabunge wanapaswa kulishughulikia, tume huru isiyo na mwingiliano na jeshi kama alivyowahi kusema kiongozi mmoja wa jeshi kuwa wanashirikiana na tume.
Lakini usidhani ni wajinga, matokeo yanahakikiwa sehemu nyingi tu ili yalete matokeo mazuri. Bahati mbaya au nzuri wa TZ sasa wamefumbua macho, na tume inapata kigugumizi kutaja hata kura za udiwani.
 
Back
Top Bottom