kUJUA MUSIC SYSTEM NZURI | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

kUJUA MUSIC SYSTEM NZURI

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by MANAKE MKARI, Mar 16, 2011.

 1. M

  MANAKE MKARI Senior Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 25, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakuu nataka ninunue music system kwa ajili ya kuniliwa kidogo. Naombeni ushauri juu ya Watt na ukubwa wa sauti maana naona zinaandikwa 250W, 300W, nk. Ikiwa na 600W itakuwa na mdundo?Maana nataka mziki mnene!
   
 2. g

  gkipaka Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 11, 2011
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  tafuta sony atleast 3000w.apo mwanzo mwisho vol 10 tu unaweza pasua ukuta
   
 3. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 819
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Usije rusha roho majirani kwa taarab kama unaishi chumba cha kupanga ..hahahahaha . Mimi sio mtaalam ila nachojua nina sony home theatre inasema 1000 watts, ina dunda vizuri sana na na enjoy bass yake , umuhimu pia chukua cables nzuri ili upate sauti nzuri, kuna hizo cables zinaitwa Monster cable , hizo zina kuwezesha kuzikia kila chombo kwenye mziki na kukupa bass unalotaka.
   
 4. Masika

  Masika JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Sep 18, 2009
  Messages: 731
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ndio baba kipimo cha mziki ni kuangalia hizo namba 250watts,300 ...... Zinavyokuwa kubwa ndivyo mziki unavyokuwa mnene
  angalia tu ukuta wa nyumba usipate crack
   
 5. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  Nimecheka sana hizi Comments humu ndani. Wengi wanaliwa sana hela zao au kununua kitu la ovyo na kisa ni kuwa wameandika 1000W.

  Sijui kwanza uko wapi na sehemu na pesa yako ikoje.

  Ila kusema ukweli, dunia ya kuwa na likabati la Music System majumbani imekwisha. Watu sasa hivi wanatumia zaidi home theatre. Ni sauti tosha kabisa huku ukiwa hutowi usumbufu kwa majirani. Siku ukiwa na harusi, si unakodisha tu music? Sherehe kama hizi huwa binadamu wanazo chache sana hadi uje upige Vitofali vyote sauti Full. Kwa Disco pia hazifai maana utauwa Spiker bure.

  Wee nunua hizo Home Theatre na zaidi kwangu mie ningelikupendekeza ununua PANASONIC au SONY. Kama ukitaka tofali kama Home Theatre na MISPIKER yake mikubwa, basi nunua hao akina ONKYO, Sony, nk ila hawa bwana labda uwe na jumba lako sijui wapi na majirani wako mbali na chumba cha kuangalia Sinema ni kikubwa kama watu 50 hivi.

  Unaponunua Spiker, kwanza angalia bei na uzito wa Spiker. Ukiona Spiker kubwa, miwati kibao na ukilibeba ni mzigo wa Manyoya, basi ujuwe hilo bomu. Ukishaona ambayo ukubwa, bei na uzito vinzlingana, basi angalia sasa kitu kinaitwa Frequency na dB (Decibela) ingawa hii isikupe sana shida.

  Kwenye Frequency, utagundua kuwa Spiker nyingi zinaanzia kitu kama 60hz-20 000 Hz. Hizi mara nyingi kama ni kwenye HT basi zinakuwa ni zile ndogo na zinaweza kuanzia hata 100Hz au zaidi....... Pia inakuja kitu inaitwa Sub-Woofer ambacho kinakuwa Ki-Box kiJEBA na kina tundu kwa mbele. Hizi mara nyingi zinaanzia kwenye 20-40Hz na kwenda juu kidogo kama 200Hz.

  Mchezo uko hivi: Unaposhuka zaidi chini, ndiyo SAUTI NZITO ya BASS na unapopanda juu ndiyo ile MICHANGA (sikiliza wimbo wa Computer Love wa Rogers and Zapp utaisikia). Kuipata michanga ni kazi rahisi ila kupata BASS kubwa na nzuri ni kazi ngumu na inabidi utumie Materials nzito na aghali. Ndiyo maana namba za hizo Hz zinavyopungua, bei yake inakuwa ya kuotea mbali. Michanga mara nyingi wanaweka hadi 20 000Hz kwa sababu zaidi ya hapo, MASIKIO YA BINADAMU HAYASIKII KITU. Mbu anasikia kwenye Freq 60 000Hz, mhhh........ Sasa unakuta wanakuuzia Spiker au Headphone na wanaandika kuwa 10-30MHz. Sasa hapo ujuwe unaliwa hela heheheeee.....

  Ila kuna wengine wanadai kuwa Spiker ina uwezo wa kupiga hadi 20Hz ila bei yake ni kama Dola 150. Matokeo yake ukipiga unasikia sauti utafiri Spiker limechanika. Ndiyo maana bei, na uzito pekee vinaweza kukuambia kama kweli umenunua Spiker nzuri. Kuna Mzee miaka ya 90 nikiwa nchi za watu nilikutana naye akiwa kanunua Spiker za dola laki moja ili asikilize Jazz Music, wera wera !!!!!!

  Watu kama JBL, spiker zao ni nzuri sana. Boss na wao mhhh, mashine kali na safi ila sasa BEI!!!!! Ayii Ayiii........

  WATTS ni wizi mwingine huwa wanaufanya jamaa..... Fikiria Concert za watu kama Michael Jackson wanatumia Spiker za kama 10 000W. Concert za kwenye Maholi ya mziki inashuka hadi kwenye 3 000-4 000W. Ina maana mziki wa nyumbani haiwezekani uwe na 1000W kwa Spika. Ila hizo zinakuwa kwenye Amplifier yenyewe. Sasa ukizigawanya kwa 5 kwa namba ya Spiker, unakuta kuwa kwa Spiker kuna wastani wa 200Watts wakati wenzio akina The Rolling Stones, wanakuambia hizo ni Watts kwenye Spiker moja. Na mara nyingi kila Spiker inakuwa na Amplifier yake.....

  Hii ni sawa na Camera. Ukinunua imeandikwa Zoom 20 x, basi umeliwa maana ukweli hapo wamekuandikia na Digital Zoom ambazo ni kama kukuza ukubwa na si KUSOGEZA. Siku zote soma kitu waandika OPTICAL ZOOM maana huyo ndiyo mwenyewe.

  Nakuachia STAGE ya Rolling Stone na Spiker zao za JBL. Angalia urefu wake na urefu wa Binadamu. Hapo sasa ndiyo Watts wanakuhesabia kwenye Spiker na siyo Aplifiers..... Kama utakuwa na swali zaidi, basi usisite kuni-PM na ntakuja kuwajibu wote.

  [​IMG]
   
Loading...