Ndugu wanabodi,
Tokana na juhudi zetu za kumwaga ama kuanika uchafu unaofanywa na viongozi wetu katika serikali ya Tanzania, tumewezesha kulazimisha Baraza la mawaziri kuvunjwa.
Lakini kiini kikubwa cha kuvunjwa kwa baraza hilo ni Ufisadi.
Swali langu ni kwamba je adhabu ya kujiuzulu ama kuachishwa kazi inatosha?. Mapesa yetu yaliyochukuliwa yatarudishwa vipi, lini, na wapi?.
Kwanini wahusika na ufisadi wasichukuliwe hatua kama vile kuwekwa ndani na kufunguliwa mashitaka?.
Ni katika Tanzania hiyo hiyo mwizi wa kuku ama mwizi wa mifukoni akishikwa tunampiga na kumchoma moto, sasa hawa wezi wakubwa na wakutisha kwanini tunawaangalia tu?. Kwa misingi hii ndugu wana JF hamwoni kama wizi ama tabia ya ufisadi haitaisha Tanzania?, kwani kila atakayepata mwanya atafanya kweli akijua kwamba akijulikana ataachishwa kazi tu lakini maisha kwake yatakuwa poa tu. Je adhabu inatoshaaaaaaa???????