Kujitoa kwa Mwapachu CCM, Sababu hizi hapa

Kujitoa kwa Mwapachu CCM, Sababu hizi hapa

Ndugu Wanabodi,

Suala la kujitoa kwa ndugu Mwapachu CCM na kudai Kuwa ati CCM siyo mamake, siyo suala geni. Wafukunyungu kama sisi tulilifahamu hili sikunyingi na tulisubiria litokee. Wengine bado wapo an watafuata siku si nyingi!

Kama alivyoeleza yeye binafsi, Mwapachu alikuwa ni TeamLowassa , Lowaasa akiwa bado yuko CCM. Mwapachu ni miongoni mwa makada wa CCM waliokuwa wakigawa fedha za Lowassa pale DODOMA. Mwapachu alikuwa ni miongoni mwa walioratibu msafara wa vijana waendesha bodaboda walioendesha pikipiki hadi Dodoma kumuomba EL agombee Urais. Ni Mwapachu huyu huyu aliandaa (kwa kushirikiana na Team Lowassa) CV za watakaowekwa katika nafasi mbalimbali mara EL atakapotinga Ikulu kupitia CCM.

kubwa zaidi na kilichofanya ajitoe CCM, Balozi Mwapachu ameahidiwa na aliahidiwa nafasi ya UWAZIRI WA MAMBO ya NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA. Tunalifahamu hili na list nzima ya Walioahidiwa Ukuu wa Mikoa, Wilaya, Wizara, Ubalozi, na Ukatibu Mkuu ipo.

Ninachotaka kuwaambia ni kuwa hao wanaotoka CCM siyo kwa sababu wanataka MABADILIKO YA KWELI in kwa sababu wanafuata maslahi. Wanaotaka mabadiliko ha kweli walikuwa CDM tangu hata kabla ya uchaguzi mkuu kuanza. Kuweni makini mnaposhabikia wanaojiondoa CCM muda huu wa kampeni Zambia lala salama!

nawasilisha.
Yeamlowassa iliyokuwa ndani ya Ccm imulikwe!
 
Acha kutapatapa ulikuwa wapi kuyasema hayo kabla. Haya embu tuambie watakaofata ni nani na nani na kwa sababu zipi.
 
Condition za kumwaga shuzi nimezitoa,sasa kama mnaweza hoja zijibiwe hayo mengine ni utovu wako wa adabu !

Ralph Tyler amekujibu uzuri sana, tena amerefer watu wazito kwenye post nzito kama Sepp Blatter wa FIFA, na kama iyo haitoshi kingunge huyo huyo alijitosa kumpigia debe Lowasa live live, tena kwa kujua kuwa anakiuka taratibu za chama alizozisimamia yeye kwa miaka isiyopungua 50 ila kwa vile Lowasa amemuahidi kitu akajikuta anazivua nguo zote hadharani bila kujali kuna vijukuu sebuleni. Sasa kama hizo zote kwako si hoja na kuona ni utovu wa adabu kajambe ili utimize ile ahadi yako ya kublack out Zenj yote na kwa hili nachelea kuamini utakuwa una combination ya Bachani, Kisisimizi, Arafati and the likes , so watch out usije ukaunguza vifaa vya watu vya umeme kwa hilo mega watt lako.
 
Ninachotaka kuwaambia ni kuwa hao wanaotoka CCM siyo kwa sababu wanataka MABADILIKO YA KWELI in kwa sababu wanafuata maslahi. Wanaotaka mabadiliko ha kweli walikuwa CDM tangu hata kabla ya uchaguzi mkuu kuanza. Kuweni makini mnaposhabikia wanaojiondoa CCM muda huu wa kampeni Zambia lala salama!
nawasilisha.

Sasa kama hawa wataharakisha hayo mabadiliko, ushauri wako nini? Kwani kwa sasa ilani watakazotekeza ni za ccm? Je wangejiunga na CHADEMA kabla ya kuanza harakati za uchaguzi wangekuwa watu tofauti na ilivyo sasa?

Ukiwa mkristo ukikubali kuwa muislamu sharti utiwe maji, kadhalika kwa muislamu kwenda ukristo sharti abatizwe (atiwe maji). Sasa wote hawa wametiwa maji, sasa tuseme je?
 
Na Kingunge kwa umri wa zaidi ya miaka 82 aliahidiwa nini?

wakati mwingine muwe mnatumia na akili zenu sio mnakalia mihemuko tu! kwani siku zote walikuwa wapi hadi wamsubiri LOWASA ndo watangaze kujitoa!? inamaana hawana akili za kuyajua mabadiliko hadi LOWASA awaongoze!? mimi nasema hao wote ni wanafiki wanakuja kuvizia vizia ulaji tu hawana jipya!!
 
wametiwa maji wapi au wamebatizwa wapi wakati wengine ndo kama wamesababishwa Mbowe na Lissu kupata kigugumiza cha ghafla juu ya Ufisadi na mambo mengine lukuki! Ni ujinga kuamini kuwa kweli hadi Sumaye nae eti anahubiri mabadiliko..............yetu macho ngoja huu upepo upite tuone kama baada ya uchaguzi watabaki salama......nachohisi mimi, endapo LOWASA atashinda LAZIMA mtifuano wa kugombea vyeo kwa hawa wanaokuja utokee na asiposhinda hautawaona wala kuwaskia tena wakihubiri hayo mabadiliko!
 
Kwa vyovyote vile kuna faida zake na hasara zake. Lowasa akishinda kuna faida zake kubwa kuliko inavyoweza kuelezeka. Faida moja kubwa ni kuwa siasa za Tanzania zitakuwa zimebadilika kwa ujumla wake, na mfumo uliojengeka kwa miaka mingi wa chama tawala utakuwa umevunjika rasmi. Kwangu mimi hili ni kubwa kuliko yote.
 
wakati mwingine muwe mnatumia na akili zenu sio mnakalia mihemuko tu! kwani siku zote walikuwa wapi hadi wamsubiri LOWASA ndo watangaze kujitoa!? inamaana hawana akili za kuyajua mabadiliko hadi LOWASA awaongoze!? mimi nasema hao wote ni wanafiki wanakuja kuvizia vizia ulaji tu hawana jipya!!
nitajie mwanasiasa mmoja asiyevizia ulaji?
 
Ninyi watu wa CCM mnashangaza sana.Hivi inaweza kuwa kweli kwamba kila anayeondoka CCM ndiye mwenye matatizo.Siamini kabisa.Mtu muungwana yanapotokea matatatizo kama hayo, anajichunguza yeye mwenyewe kwanza.Na hakuna mtu aliyekamilika,kila mtu ana kasoro.Vivyo hivyo CCM nayo haijakamilika,CCM ina kasoro,tena kubwa,ndio maana hata waasisi wa chama wanaondoka.Ni vema CCM ikatambua hilo na ikajirekebisha.Kuendelea kuamini kwamba wanaondoka ndio wenye matatizo na kumbe sio kweli ni kujifariji.Tabia hii itaendelea kukididimiza na kukibomoa chama.

Kwa hiyo kuondoka kwa Dr Slaa na Lipumba tatizo sio wao tatizo ni limfumo la chadema na ukawa. Hapa nimekuelewa sana mkuu.
 
Hata ungekuwa wewe ungefata maslahi. Siasa ni kazi kama kazi ingine yoyote ndo wanasiasa wanapopata chakula chao. Funguka
 
Jamani Mzee ni cha pombe hana kazi anayoiweza ni katika kubebana tu ndio alipatiwa nafasi ile,tunasonga mbele kungoja Rais wetu Dr John akiapishwa hivi vizee viende tuu mbona tuna wazee wengi tu tena walikuwa mabosi wao
 
Chadema msishangilie ujio wa hawa wanamtandao mnapokea matatizo chamani kwenu huku wamesumbua sana... toka enzi za Baba wa T. Labda huko watakuwa watulivu.
 
Na Kingunge kwa umri wa zaidi ya miaka 82 aliahidiwa nini?

Kingunge hajakosana na JK leo.., wengi kwa kuwa mlikuwa makinda hamuwezi kujua au kukumbuka..,

www.joe-tznews.blogspot.com: Kingunge, Sumaye out of Central Committee

Kama Lowassa aliwadanganya mmelamba dume mlifanya makosa, mlitakiwa mfanye due diligence yenu mapema kujua influence na weight ya makada mnaowaokota. As it stands many were none factor and outside the inner core for as long as 3/4 of JK presidency.
 
nitajie mwanasiasa mmoja asiyevizia ulaji?

mkuu, naongelea hao wanao tanga tanga! hata ndani ya UKAWA wapo wengi wanaovizia madaraka lakini hao naweza kuwaita hao ni watoto wa nyumbani ambao kupewa chakula ni haki na halali kwao sababu walitumwa na baba yao (chama) kufagia nyumba wakafagia, walitumwa kuchota maji wakachota, kadhalika hata kudeki choo walideki, sasa kwanini wakose matunda ya baba kutajirika kisa watoto wa jirani waliothubutu hata kuwakebehi wakati wanadeki choo kwa amri ya baba yao!? yaani leo mtoto wa kambo awe na thamani zaidi ya mtoto wa ndani!!?
 
Back
Top Bottom