Kujifungua | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujifungua

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Nov 10, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Unafaa kuzijua dalili uchungu wa kuzaa. Unafaa kujua pia chagui za kujifungua. Inafaa usikie umetosheka na chaguo lako.  Katika sehemu ifuatayo utajifunza kuhushu uchungu wa kuzaa (labour) na kujifungwa. Jifunze vile unavuofaa kutosheka na jinsi unavostajili kuchukulia maumivu haya. Jifunze jinsi ya kujitunza baada ya kujifungua na pia utapata ujumbe kuhusu majonzi baada ya kuzaa.

  Baada ya kujifungua


  Wakati huu, baada ya kujifungua, huitwa ‘post partum period’. Huu ni wakati utakapokuwa na mabadiliko mengi sana maishani kwa sabababu una mtoto wa kutunza. Ni vizuri kufuata maagizo yale daktari wako atakupa na ujitunze wewe na mtoto wako.
  Haya ni baadhi ya mambo unayoweza kufanya ili kuufanya wakati huu rahisi.

  • Pata pumziko la kutosha- Hili ni jambo moja muhimu sana unafaa kuzingatia siku za kwanza baada ya kujifungua. Jilaze chini ili kupata usingizi kila wakati mwanao anapolala.
  • Usifanye kazi nyingi punde sana- Uliza usaidizi kutoka kwa marafiki na familia ili wakusaidia kionya, kupika na shughuli zingine za kila siku.
  • Fanya mazoezi rahisi rahisi- Unaweza taka moili wako urudie umbo/ukubwa wake kabla ya kupata mimba. Yaweza kuchukua muda mrefu ili misuli ya tumbo iliyokuwa imekunjuka kurudia hali yake ya awali, lakini mazoezi rahisi yanaweza saidia. Anza kufanya mazoezi taratibu na kasha kuongezea mazoezi polepole. Kama unanyonyesha, hakikisha umenwona daktari wako kabla ya kuanza zoezi lolote.
  • Tambua kwamba mwili wako bado unabadilika- Mwili wako utaendelea kubadilika jinsi unavyoendelea kupona tangu kujifungua. Siku za kwanza utakosa starehe. Tumbo la mama huanza kujikuja na linaporudia ukubwa wake wa kawaida, matiti yaki yatajaa na kuuma,na mguu yako inaweza kuanza kufura. Pia utapata majimaji yakitoka ukeni yaitwayo ‘lochia’. Huwa damu na tabaka la tumbo la uzazi. Pia haya huwa ya kawaida na hukoma baada na ya siku kadhaa.
  • Kula chakula kilicho na afya na unywi maji mengi. Kama unanyonyesha ongea na daktari wako kuhusu chakula unachotaka kula.

  Kama utaona mabadilika yafuatayo, mwite daktari wako haraka iwezekanavyo:

  • Joto ya juu ya 38oc
  • Uchefuchefu na kutapika
  • Uchugu unapokonjoa, kuchomeka unaponjoa au haja ya kukonjoa kwa ghafla.
  • Damu ya hedhi nyingi kuliko kawaida na huendelea siku nyingi kuliko 1on2.
  • Uchugu, kufura au miguu yako kuwa miororo
  • Uchugu kwa kifua na homa
  • Matiti moto na nyororo
  • Uchugu kati ya uke na huendelea kuwa mkali.
   
 2. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #2
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Jinsi ya kuufanya uchungu wa kujifungua ustahimilike


  Labda unawaza kuhusa uchungu utakaopata wakati wa kujifungua. Kuna mambo unayoweza kufanya ili uchungu huu ustahimilike.

  • Kutumia njia za kujipumzisha na kuvuta hewa
  • Dawa za kudungwa mishipani
  • Sindano itakayopunguza uchungu upande wa chini wa mwilio
  • Dawa ya kupunguza maumivu (anaesthesia) hasa unapotumia kibanio
  • ‘Pudenal Block’ itakayo maliza hisi kwa uke na mwaranda.

  Kujifungua/uchungu wa kujifungua


  Katika wiki zako za mwisho za mimba, mji wako mimba (uterus) utaanza kurudiana kujikunja. Hii huita Braxton-Hicks Contractions (au uchungu wa kujifungua usio wa kweli) na huwa wa kawaida. Kwa sana hili hutokea ukikaribia kujifungua, ni vigumu kwa wanawake wengi kujua kama ni uchungu wa kweli au usio wa kweli.

  Ongea na daktari wako kama:

  • Unapata mikunjano hii (contractions) baada ya sekunde 30-70, inaendelea bila kukoma na inaendelea kuwa mikali zaidi.
  • Unaumwa na sehemu ya chini ya mgongo na uchungu huu haukomi.
  • Hata kama uchungu wa kujifungua huwa tofauti, huwa na awamu tatu kwa kawaida.

  Awamu ya kwanza
  Hiki kipindi ndicho hukoa sana. Huanza wakati mlago wa uzazi huanza kuwa mwembamba na kufunguka. Ule ulio na damu huanza kutoka ukeni (‘show’). Karibu na mwisho wa awamu hii mikunjano huu huana mikali zaidi na huchukua muda mrefu pia.

  Awamu ya pili
  Mlango wa uzazi hufunguka kabisa na mtoto anahitaji usaidizi ili atoke. Utahitajika kumsukuma mtoto ili atoke wakati wa mkunjano hadi mtoto atakapotoka. Awamu hii inaweza kukaa hata masaa mawili au zaidi hasa kama ni mara yako ya kwanza.

  Awamu ya tatu
  Baada ya kujifungua utaendelea kupata mikunjano ili kito ‘placenta’. Mikunjano hii huja ikikaribiana zaidi kuliko ile ya kabla hujajifungra lakini haina uchungu kama ya awali. Awamu hii inaweza kukaa kwa dakika chache na kukaa kwa dakika 15-20.

  Baada ya kujifungua utachungwa kwa uangalifu mwingi ili kuhakikisha hauna matatizo yoyote. Joto la mwili wako, mpigo wa moyo, kupumua na mwendo wa damu zitachunguzwa mara kwa mara. Katika wakati huu, unaweza kuanza kumjua mtoto wako. Kama ulikuwa umepanga kumnyonyesha mwanao unaweza kuanza wakati huu.


  Daktari wako atakusaidi kuchagua ni njia ipi nakufaa zaidi.
   
 3. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Majonzi baada ya kuzaa


  Wiki moja baada ya kujifungua unaweza kuanza kupata mabadiliko ya tabia (furaha na hasira) yanayo sababishwa na mabadiliko ya ‘Hormone’, uchovu na mahangaiko kwa sababu ya mtoto wako kukufanya ukasirike. Haya ni matukio ya kawaida na hutoweka baada ya wiki chache.

  Kwa matukio mengine, wanawake huhuzunika hata wanashindwa kujitunza na kutunza watoto wao. Haya majonzi huitwa ‘Post natal’ au ‘Post partum depression’. Kama kukasirika huku kutaendelea kwa zaidi ya wiki mbili au kama una yafuatayo, hakikisha umemwona daktari wako:

  • Haupati usingizi au unakasirika haraka
  • Una huzuni, umekasirika na unakaa ukilialia
  • Hauna nguvu
  • Unaumwa na kichwa na kifua unapumua harakaharaka, moyo wako unapiga kwa kasi au unasikia kama moyo unaruka midundo Fulani.
  • Haukuli au unakula sana
  • Haufikirii vizuri, haukubuki mambo au hauwezi kufanya uchaguzi
  • Hauna hamu tena ya uliokuea unapenda kama kufanya mapenzi
  • Haupati shughuli na mtoto wako
  • Unajisikia kama hauna maana tena na unajihurumia
  • Unaogopa utamuumiza mtoto au utajiumiza

  Njia zingine za kukusaidia unapojifungua

  Wanawake wengi hujifungua kupitia kwa mlango wa uzazi, lakini wakati mwingine njia zingine huhitaji ili kisaidia kujifungua.

  • Kibanio (forceps) - Kifaa hiki hukaa kama vijiki viwili. Daktari hukiweka kwenye uke kasha anakishikisha kwenye kichwa cha mtoto na kumvuta mtoto kwa utaratibu ili atoke.

  • ‘Vacuum’- Kikombe cha plastiki huwekelewa kwenye kichwa cha mtoto kwa kutumia bomba la ‘vacuum’ mtoto anavutwa taratibu baadaye.

  • Upasuliwaji - Mama mtoto hukatwa tumbo na mji wa mimba ili kumtoa mtoto (caesarean section)
   
 4. M

  Malolella JF-Expert Member

  #4
  Jun 3, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 367
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hili ni bonge la darasa.
   
 5. nilkarish

  nilkarish Member

  #5
  Jun 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  shukran sana mzizimkavu.. i wish ningeisoma hii topic before sijaingia exam yangu, kuna question zilitoka kwenye exam hapa ndo nimekuta majibu yake.
  namba kukuliza post partum depression umesema inakuwa kw 2 weeks, kma ikizidi hapo inakuwa normal depression or major depression?
   
 6. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #6
  Jun 4, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @nilkarish Post partum Depression kwa kawaida inakuwa ni wiki mbili ikizidi hapo inakuwa ni Major depression itabidi umuone Daktari wako haraka iwezekanavyo akupe tiba na ushauri wa kufanya au ikitokea moja kati ya dalili hizi hapa chini itabidi umuone pia Dakatari wako.

  Haupati usingizi au unakasirika haraka
  Una huzuni, umekasirika na unakaa ukilialia
  Hauna nguvu
  Unaumwa na kichwa na kifua unapumua harakaharaka, moyo wako unapiga kwa kasi au unasikia kama moyo unaruka midundo Fulani.
  Haukuli au unakula sana
  Haufikirii vizuri, haukubuki mambo au hauwezi kufanya uchaguzi
  Hauna hamu tena ya uliokuea unapenda kama kufanya mapenzi
  Haupati shughuli na mtoto wako
  Unajisikia kama hauna maana tena na unajihurumia
  Unaogopa utamuumiza mtoto au utajiumiza
   
 7. nilkarish

  nilkarish Member

  #7
  Jun 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ok . ila siumwi depression thnx GOD.. hili suali tuliulizwa kwenye mtihani. asante kw kunipatia jibu
   
 8. Latifaa

  Latifaa JF-Expert Member

  #8
  Jun 4, 2012
  Joined: Jan 18, 2012
  Messages: 474
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  thank you mzizi mkavu! Niko njiani kupata mtoto somo zuri na limenifaa sana.
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @Latifaa Mwenyeezi Mungu akupe mtoto mwenye kheri na wewe inshallah.
   
 10. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #10
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #11
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Vipi Mwalimu wangu hujambo lakini?
   
 12. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #12
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  sijambo kabisa daktari wangi MziziMkavu. niliamka mapema kuandaa somo wanangu wanaanza mitihani ya mock tarehe 23/7 so chemia inanipeleka kwani nilikuwa maternity.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin pole sana kwa hiyo unawasaidia wanangu ili waweze kupasi hiyo mitihani? Na mimi Mwangu yupo hapo chuo kikuu DAr anafanya Mitihani yake ya Semster ya IT. Wewe kwani upo mji gani Dar au Arusha?
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  ndiyo nawasaidia wanangu manake wote wanaopitia kwangu huwa nawaita wanangu. nawapenda sana hawa vijana sijui kwanin. Mimi niko Dar of course. wewe mwenzangu umesha kuza huyo chuo wala hakupi shida
   
 15. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #15
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Hanipi shida? unasema wewe mtoto wa miaka 25 si unajuwa vijana wa siku hizi kwa kupenda mambo ya ujana, kulewa,kuvuta sigara uvutaji wa bangi uvutaji wa madawa ya kulevya na mengineyo mengi tu.

  Na mimi sipo nae karibu napigizana nae kelele tukiwa kwenye chat ya Skype yeye huniambia baba mimi ninataka kuja kwako nipande ndege nampigia kelele upande ndege? soma umalize ndio waweza kupanda ndege nikiwa kwenye chat nae nakuwa

  mkali kama nusu saa kisha nakuwa mchangafu namchekesha kama rafiki yangu si unajuwa ukiwa ana mtoto wa kiume anakuwa kama ni rafiki yako wa karibu baba yake ungelikuwa unajuwa mambo ya IT ungemsaidia mwanangu. Au sivyo bibie?
   
 16. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #16
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  unajua MziziMkavu, malezi ya ujana ni magumu sana, kuwa rafiki lakini pia uwe very strict usipende awe mzembe. Hawa ninaowafundisha ni vijana wa miaka 20-24 ni rafiki yao sana na huwa tnapendana na kuheshimiana sana lakin wakikosea nawalima mikwaju au hata kuwakaripia. But wako wazuri sana huwaga nawapasha livu hasa juu ya tabia za ujana manake wanaolala shule n vijana wa a level tu day ni o-level halafu kuna wadada wa o-level so yaani niko makini kwel na tabia zao za kiujana.

  ila najiskia raha sana ninapoona wako vyuo wengine, na wengine wamemaliza degree dah! halafu bado wananiita mama ni raha sana kuliko hata ningelipwa milion halafu nikose hii heshima.

  Ningekuwa najua ningemsaidia sana tu. si unajua tena mm na wewe?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Ninajitahidi ingawa nipo mbali na yeye na yeye mwanangu anakaa kwa mjomba wake si unajuwa mtoto wako akikaa kwa kaka yako ataweza

  kumuangalia kama unavyomuangalia wewe mwenyewe? Waswahili husema Fimbo ya mbali haiuwi nyoka mama yake ni mgonjwa wa moyo basi kazi ninayo mimi mjomba wake hamshughulikii chochote yeye humwambia tu mwanangu baba

  yako si yupo ulaya? ndio atakaye kuangalia wewe mimi sina wakati, shemeji yangu ana matatizo na yeye huyo mjomba wake yaani shemeji yangu alikuwa Mwalimu kama wewe lakini amekwisha acha kufundisha kwa sababu ya uzee lakini wewe bado unafundisha ndio vizuri wachunge sana vijana ujana wao ni wa taabu tupu mitihani ya dunia ni mingi sana.
   
 18. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #18
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  kwa ulivyosema nimepata picha moja kuwa huenda mwanao akawa muhanga tabia za kuiga kwasababu ya kukosa uangalizi wa karibu. Lakini pia nikutie moyo dont look at what uncle is doing to his niece ila wewe mweleze maisha anayotafuta ni yakwake binafsi wala hataish na mtu so aki messup ameharibu yote aliyoyatafuta kwa bidii for 2 and a half decades. na akiwin hapa basi atavuna aivyovitunza kwa muda wote huo.

  ukitaka kumueleza usimpe alternative soln katika maisha like usimwambie soma ukifeli nitakuchukua uje huku urudie, au tutafanya hivi. Mwambie kabisa ukeli kuwa akifeli ni basi so aamue moja kusuka au kunyoa.

  pole sana ka kuugulliwa na bimkubwa Mungu ata muafu tu. mimi nafanya kazi ya kanisa tu hainaga malipo hii nasubiria kuurith uzima wa milele tu, manake hakuna return kwenye misha ya kuwa mwaalim kwa hapa kwetu. But sijutii sana kwangu ni poa tu.
   
 19. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #19
  Jun 6, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Ni kweli uyasemayo anapenda sana kuangalia marafiki zake ni nini wanachofanya lakini ninashukuru Mungu haigi marafiki zake na pia anayo akili havuti,sigara wala hana ulevi wa aina

  yoyote ile iwe ulevi wa wanawake au pombe au madawa ya kulevya ninashukuru mimi huwa namwambia umeona Rais Obama alivyokuwa amejitahidi kusoma mpaka kawa Rais wa Amerika na Dunia nzima inamuangalia yeye Rais Obama.

  Soma na wewe uwe kama Mzee Obama, ananiitikia sawa baba lakini kazi kweli ninayo kubwa sana. Huwa Mwanangu ananiambia kuwa Wenzake wakienda chuoni wakiwa Walimu wao hawapo Darasani Marafiki zake huwa wanafunguwa internet kwenye facebook na kuanza ku chat na marafiki.

  Yeye mwanangu huwa anajisomea masomo na ikifika kwenye mitihani wana feli hao wanaofunguwa Facebook wakiwa shuleni basi napata hope kidogo kuwa anayo akili ya kusoma ingawa nipo nae mbali Namuomba Mwenyeezi Mungu amsaidie si unajuwa elimu ndio ufunguo wa maisha ya binadamu.
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Jun 6, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,838
  Trophy Points: 280
  mzizi mkavu atleast huyu anaelewa nini maana ya shule wewe mwombee tu ila naskitika maisha anayokulia siyo mazuri sana. Hakuna kitu ibaya kama ukose mtu unayemwamni kumwambia shida yako. but jitahd tu atatoka tu so far bado kijana mdogo kabisa.
   
Loading...