Kujiangalia kwenye madirisha au milango ya vioo

Kujiangalia kwenye madirisha au milango ya vioo

Sasa kama wanajua, kwanini wasimame dirisha ambalo nasi tunategemea mwanga ili tufanye kazi halafu wanaendelea na mambo yao kama wako washroom ?
Mnategemea mwanga sasa mliweka tint za nini?
 
iliwahi nikutia kipindi hicho nasoma secondari niliona gari ina tinted nikaenda kujiweka sawa kwnye kioo kilichofuataa aibu hata kuhadisia
 
Kwani uliambiwa wanaotumia vioo hivyo kujiremba hawajui kama wa ndani wanawaona?!!
Shangaa na wewe, km alikuwa hajui huwa tunajiangalia huku tukijua tunaonwa. Mi ofisini kwangu ht walishanizoea, maana kila mchana after lunch lazima nipite na nikipita lazima nisimame kidogo kujiangalia.
 
Kwa yeye kutokukuona wewe hali ya kuwa wewe unamuona si tatizo.
Binadamu ana hulka ya kujitengenezea UKWELI WAKE na kisha kuamini, japo si UKWELI HALISI.
 
Kuna dirisha la benk flan hv pale kwenye round about yenye sanamu ya askari mwenye bunduki miaka mitano nyuma Ilkua kila asubuhi watu wengi tuliokuwa tunapita pale Ilkua lazima usimame ukikuta mwenzio inabidi uzuge aondoke nawe uingie ilbidi wapige tofali pale ila saiz naona kuna kioo pembeni yake ila aking'ai kama kile cha miaka ile

Postal Bank...
 
Ahahahaha umenigusa
 
Mnaotumia baadhi ya majengo ya vioo vya maofisi ya watu kujiangalia na kujirekebisha vizuri mlivyovaa tambueni kuwa mnaonekana maana vioo vingi ni tinted. Hii kuona kuwa huwaoni walio ndani isikufanye udhani nao hawakuoni, tafuta kujua kabla hujajianika.

Unakuta mtu anajiremba katika dirisha la ofisi yako na baadae anajipiga selfie akidhani haonekani na mapozi yake kumbe daah. Take care

wengI wao wale wanaotembea na vitana kila muda kutaka kuchana nywele zao, ni Utumwa
 
😀hahaha...hii isue kunajamaa alikula makofi maana alikua anajitazama ulimi, sasa wa ndani wanaona kama wanazomewa😀
 
Malizia tu

Nilisogea karibu sana na kioo ila sijafikiria km kutakua na mtu au laa kwa bahat mbaya mwnyewe akafungua kioo na kuanza kunicheka mpk nikasikia aibu den akaonfosha gari lake na kwenda zake toka siku hy nikiona vioo ninavikwepea mbali nisije ingia tena aibu[emoji85]
 
Back
Top Bottom