Kujenga nyumba ni usumbufu sana

The golden

JF-Expert Member
Sep 11, 2018
1,381
2,553
Hii ni mara yangu ya pili kipitia msoto wa ujenzi.Nilipitia hali hii kwa mara kwanza mwaka 2014.

Ni kero sana. Ni kero sana kufanya kazi na mafundi ambao hawako smart. Huyu atakuharibia kazi, huyu atakuibia materials, yule ni muongo kachukua kazi halafu hafanyi. Yaaani kuna kila aina ya kero.

Nimechoka sana. Sasa naelewa kwa nini baadhi ya watu huamua kununua nyumba tu na kuhamia.

Mafundi wengi wanahitaji usimamizi, ukiondoka tu, umepigwa. Wengine huo muda hatuna.
 
Sitosahau Rafiki yangu baada ya Nyumba yake kuisha.... Mama Chanja wake akiosha Vyombo Maji hayaendi, wakienda Msalani kujisaidia Mzigo hauendi.... kuja kufatilia Bomba za Maji taka zote zimebanwa na Kifusi.... Bwana Fundi alifukia Bomba za Maji taka hata ukizibonyeza zinabonyea.... kazi ikaanza upya
 
Ukiona fundi anakuibia
Ukiona fundi anachelewesha kazi
Ukiona fundi anakudanganya au hafiki site
TAMBUA TATIZO NI WEWE. Wengi mnawanyonya Sana mafundi mnapopatana nao kazi. Boss anaelipa vizuri huwa haibiwi na fundi, boss anaelipa vizuri hawezi kuharibiwa kazi kwasababu fundi ana budget ya kutosha.
Kama unajali maslahi ya fundi Basi nae atajali kazi ya boss.
 
Ukiona fundi anakuibia,

Ila kuna wezi ambao ipo kwa damu Yao.

Tatizo Tanzanians wengi hawajali kukamilisha kazi na kupata nyingine

Wao kuiba, kuharibu etc

Utu umuweka mtu huru na mafanikio umfata bila kuumiza kichwa kwa kutenda dhambi.
 
Sitosahau Rafiki yangu baada ya Nyumba yake kuisha.... Mama Chanja wake akiosha Vyombo Maji hayaendi, wakienda Msalani kujisaidia Mzigo hauendi.... kuja kufatilia Bomba za Maji taka zote zimebanwa na Kifusi.... Bwana Fundi alifukia Bomba za Maji taka hata ukizibonyeza zinabonyea.... kazi ikaanza upya
Tatizo boss alinunua Bomba class A.
Ubahiri was boss ulimponza.

Class A tshs 18,000

Class B tshs 39000-45000

Yeye akapenda cheap
 
Tatizo boss alinunua Bomba class A.
Ubahiri was boss ulimponza.

Class A tshs 18,000

Class B tshs 39000-45000

Yeye akapenda cheap

Kwanini fundi asi shauri zinazofaa na kusema sababu?

Wezi wezi tu, fundi anaye jithamini hawezi kufanya kazi mbovu

Mwizi mwizi tu.. na kutokutumia akili za kujiwekea level ya juu kikazi

Kataeni kazi kwani lazima?
 
Kwanini ukubali kazi kama pesa haitoshi!?

Lazima fundi anakuwa na malengo, huu sio kitu Cha kujivunia

Muhimu kujiwekea level ambayo haikushishi kikazi.
Mafundi wengi wa mtaani Wana hali ngumu kimaisha. Anakubali kufanya kazi hata ambayo Haina maslahi.
Lakini kumbuka numbers haziongopi.
Mwishowasiku hela inakata kazi bado mbichi.

Epuka Sana cheap labour
 
Ukiona fundi anakuibia,
Ukiona fundi anachelewesha kazi
Ukiona fundi anakudanganya au hafiki site
TAMBUA TATIZO NI WEWE. Wengi mnawanyonya Sana mafundi mnapopatana nao kazi. Boss anaelipa vizuri huwa haibiwi na fundi, boss anaelipa vizuri hawezi kuharibiwa kazi kwasababu fundi ana budget ya kutosha.
Kama unajali maslahi ya fundi Basi nae atajali kazi ya boss.
NAKAZIA
Fundi ukimlipa vizuri hakuibii, na kazi inatoka vyema sana
wengi ni kubana bajeti kwa kumlalia fundi matokeo yake maumivu
 
Back
Top Bottom