Kichankuli
JF-Expert Member
- Dec 18, 2008
- 887
- 189
Wakati nikikua, kule kwetu, kucheua kwa nguvu iliashiria shibe. Na kila ilipotokea inalazimu wenzio waliopo karipu wa kufagilie; kama ni mkeo atakwambia "Njiko/Nkabako yani"-ikimaanisha mume wangu, akicheua mwanamke huambiwa "Kibayi yito"-Ikimaanisha ng'ombe jike anayetoa maziwa mengi. Aidha mtu akipiga chafya shurti wenzie wamumwitikie kwa kumwambia "kusa-ikimaanisha fuka. Matendo yote mawili yamekuwa yakifanyika kwa sauti pasibo kulazimika kuwataka radhi wenzio. Lakini pia japokuwa kule kwetu kujamba miongoni mwa kundi la wenzio haikuwa inakubalika bil kujali ushuzi umetolewa kwa sauti kubwa au kimyakimya, kumekuwa na maelezo kwa watu waliowahi kuishi karibu na Wadosi/Wahindi kwamba wao kujamba ni suala la kawaida tu (sina uhakika na hili).
Ambacho ningependa Dr. JF na wadau wengine wa Weledi ya Afya ni kunijulisha:
1) Iwapo kuna madhara yoyote yanayoweza kusababishwa na mtu kubania kutoa ushuzi, chafya au kucheua;
2) Ni ipi njia sahihi na bora kiafya (siyo kiustaarabu) ya kujamba, kucheua na kupiga chafya ati ya kwa sauti au kwa kubania?