Imekuwa ni kawaida sana katika mitaa mingi hapa Dar es salaam kuanzisha Bar zinazopiga muziki kwa sauti ya juu. Mimi sio mtalaamu wa sauti lakini kitendo cha "mabar" yaliyo karibu na makaazi ya watu kupiga muziki kwa sauti kubwa bila kujari usumbufu wanaosababisha HAIKUBALIKI.
Naomba kuchukua fursa hii kumuomba Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam pamoja idara ya afya katika kata zetu kuingilia kati. Makele na miungurumo ya muziki ni kero mno.
Nafahamu watu wa "mabar" wanatumia njia ya kupiga muziki wa sauti kubwa kama njia ya kuwavuta wateja wao. Lakini wanashindwa kufahamu kwamba muziki wa sauti kubwa ni kero kubwa kwenye makaazi ya watu wanaozunguka. Kama mwenye bar anataka kupiga muziki kwa sauti kubwa ni jukumu lake kutengeneza utaratibu wa kuhakikisha sauti ya muziki wake haiwi kero kwa majirani zake.
Nimechukua njia hii ya kufikisha ujumbe kwa idara zinazohusika kwa sababu wananchi wengi wanashindwa kulalamika kwa kuongopa nguvu za wenye "mabar".
Kama njia ya dharura, nichukue fursa hii kumuomba IGP Siro kutumia vijana wake wa patrols kuwachukulia hatua mabar yote yanayopiga muziki kwa sauti kubwa kwenye makaazi ya watu.