Kuitwa kazini | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuitwa kazini

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by zema21, Jul 18, 2012.

 1. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Wakuu,
  Juzi jumatatu nimetumiwa sms ikinielekeza nikacheki kwenye email yangu kuna mail nimetumiwa inayohusu maelekezo ya ajira katika kampuni ya GBM (GLOBAL BUSNESS MACHINE) niliingia kwenye email yangu nikakuta maelekezo yaliyoonyesha kuwa katika kikao walichokaa "tulipo hotel" nimekuwa miongoni mwa watu waliochaguliwa kupata ajira katika kampuni hiyo..Hivyo jumatatu ya tar 23.7.2012 natakiwa kufika eneo la mikocheni karibu na chuo cha bima zilipo ofisi za kampuni hiyo kwa ajili ya certificate verification. Ikaongeza kuwa nifike na academic transcript, cheti cha kuzaliwa, na work permit kama mim sio mtanzania. Pia mahitaji mengine ni kulipa sh 30,000/= kwa ajili ya training itakayofanyika baada ya certificate verification (itafanyikia kcc Nairobi). Malipo yalitakiwa yafanyika kabla ya tar 18.7.2012 kupitia mpesa(wakaweka na namba za malipo) Wakuu nilifurahi nikasema Mungu amejibu maombi yangu ya kupata ajira. Nikafunga safari kuelekea mikocheni kutafuta ofisi za kampuni bila mafanikio kwani hakuna aliwahi kuisikia kampuni hiyo pale. Nilimpigia huyo aliyenitumia sms mara kadhaa haikupokelewa, baada ya masaa mawili alinipigia, nikajitambulisha akaniuliza nipo wapi nikamjibu mwenge. Akaniambia kuwa ofs zao zipo mwanza. Nikamwuliza mbona walisema ofisi zao zipo dar? Akanambia dar wana representative wao. Nikamwomba namba ya simu ya huyo repr akanipa nikajaribu kupiga siku nzima hazipatikani...nimejaribu kumpigia yule jamaa ili nimwambie namba alizonipa hazipatikani lakn hapatikan pia nayeye kutwa nzima!
  Wakuu nishaurini nilipie hizo 30,000/= manake jioni ndo deadline..!?
   
 2. Doyi

  Doyi JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Dec 4, 2011
  Messages: 747
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 60
  kaka usilipe hao ni matapeli walishaliza watu wengi sana.hyo hela kama vip katoe sadaka au fanya mambo yako mengine
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Kama hyo elfu 30 umeiokota watumie,ila kama umeivujia jasho ucfanye hvo.
   
 4. Mwanawalwa

  Mwanawalwa JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: May 28, 2012
  Messages: 1,015
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  one for the lord
   
 5. C

  CAY JF-Expert Member

  #5
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Kama unahamu ya kutapeliwa tuma.Kuanzia lini watu wanalipia training ya kazi ambayo wanaenda kumfanyia mwajiri?Akili kichwani ndg yangu!
   
 6. M

  MR.LEO Senior Member

  #6
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 129
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mdau,hii dunia imeshaharibika kabisa,mimi yamenitokea juzi nilitaka kutapeliwa laki mbili tena walikua wanamtumia mdada!
  Kilichosaidia ni huduma ya mteja ya M-PESA!
   
 7. Aggrey86

  Aggrey86 JF-Expert Member

  #7
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 856
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Wapuuzi hao Matapeli achana nao!
   
 8. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #8
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Duuh! Wakuu nawashukuru kwa msaada wenu wa kimawazo!
  Nilipata wasiwasi ndiyo maana nikaamua kutafuta ofisi zao pasipo mafanikio!
   
 9. happiness win

  happiness win JF-Expert Member

  #9
  Jul 18, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 2,478
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Hiyo 30,000 kanunue kuku mzuriiiiiii kisha mrosti na umle kwa raha zako ili akupe nguvu ya kupiga magoti na kumuomba Mungu akupe kazi ya uhakika. Achana na Matapeli.
   
 10. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #10
  Jul 18, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  asante
   
 11. p

  panadol JF-Expert Member

  #11
  Jul 18, 2012
  Joined: Feb 11, 2012
  Messages: 352
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Kaka matapeli hao usijejaribu kutuma pesa,wameshaliza sana watu!
   
 12. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #12
  Jul 19, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Bwana Mangushi nakupa pole sana.
   
 13. UKWELIWANGU

  UKWELIWANGU Member

  #13
  Jul 19, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  achana na hawo jamaa matapeli hawafai
   
 14. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #14
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  Wizi ushakua ajira in DSM
   
 15. webondo

  webondo JF-Expert Member

  #15
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 29, 2012
  Messages: 1,724
  Likes Received: 110
  Trophy Points: 160
  Pole sana, ni matapeli wakubwa hao, bora ukatoe sadaka hiyo 30,000/=
   
 16. ITEGAMATWI

  ITEGAMATWI JF-Expert Member

  #16
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 4,222
  Likes Received: 1,065
  Trophy Points: 280
  Kama unahamu ya kuitoa hiyo 30,000/=Tsh nakushauri bora uwapoze wafiwa na majeruhi wa Ajali ya Boti.
   
 17. m

  mummyjimmy Member

  #17
  Jul 19, 2012
  Joined: May 13, 2011
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hao we ni wezi kakangu usilipe mi yashanikuta hayo .

   
 18. BAGAH

  BAGAH JF-Expert Member

  #18
  Jul 19, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 4,523
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  sa kama ndio unatafta kazi elfu 30 unatoa wap?
   
 19. zema21

  zema21 JF-Expert Member

  #19
  Jul 19, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 619
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  wao wanataka ulipe hawajui utakapoipata cha msingi uwalipe!
  Hakuna dhambi kubwa kama hii ya ku-take advantage kwa shida ya mwenzio ili kunufaika
   
 20. Gwangambo

  Gwangambo JF-Expert Member

  #20
  Jul 19, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 3,655
  Likes Received: 85
  Trophy Points: 145
  Liwalo na liwe, fanya maamuzi magumu.
   
Loading...