Kuisifia serikali ya awamu ya nne, ni sawa na kusifia kuzikwa kwa mchakato wa KATIBA MPYA.

Muwindaji

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
245
250
Habari zenu wanabodi,
Natumai weekend inakwenda vizuri popote pale mlipo.

Binafsi nikikumbuka swala la katiba mpya moyo wangu unafadhaika sana.

Nakumbuka jinsi tume ya kukusanya maoni ilivyoendesha mchakato ule kwa usahihi na uamimifu mkubwa na wananchi wa kawaida tulipata nafasi ya kutoa maoni pia.

Mchakato ulienda vizuri mpaka kufika hatua ya kukamilika kwa rasimu ya katiba, rasimu ambayo ilikua na mageuzi makubwa sana ndani yake.

Ikumbukwe kua mchakato huu uliendeshwa kwa bajeti, alafu licha ya bajeti mchakato huu ulikua ndio landmark ya maisha ya kidemokrasia hapa Tanzania.

Mwisho wa siku mchakato huo ulifanyiwa mambo ya ajabu mpaka matumaini ya watanzania yakayeyuka kabisa.

YAPI YALIKUA MATEGEMEP YETU KUTOKA KWA RAISI JAKAYA KIKWETE?

mheshimiwa raisi kikwete alikua anaelekea kuandika historia ya kipekee kwa kuikabidhi Tanzania katiba ambayo ilikua inamaliza matatizo yote.

Pesa zilizotumika, pamoja na umuhimu wa swala lenyewe, kushindikana kutimizwa kwake baada ya kulianzisha kulikua ni sawa usaliti mkubwa.

Hata uhuru wa kuongea ulioshamiri kipindi chake ulikua hauna maana kama mawazo hayo yangeshindwa kutekelezwa na kuwekwa Katika mambo muhimu ya kikatiba.

Raisi kikwete alikua ni msaliti wa matumaini ya watanzania, hii ipo wazi na haihitaji kupepesa macho.

IWEJE MSALITI WA MATUMAINI YA WATANZANIA KWA KUWANYIMA KATIBA MPYA AONEKANE SHUJAA WA LEO?

Katika hali ambayo sio ya kawaida, baadhi ya watanzania, kwa kujitoa ufahamu, wamekua wakieleza wazi wazi kua wanamkumbuka raisi huyu msaliti wa matumaini ya watanzania.

Wapinzani pia, kwenye matamko mengi, tamko moja wapo likiwa la mwenyekiti wa chama kikuu cha upinzani Tanzania CHADEMA ndugu FREEMAN MBOWE anaeleza wazi kua wanamkumbuka raisi huyu msaliti wa mioyo ya watanzania.

Hii inamaanisha nini?
Hii inamaanisha kwamba upinzani umejikitika kwenye siasa za kinadharia zaidi, siasa ambazo utaongea tu bila kua na uwezo wa kubadili chochote.

Siasa ambazo unapewa uhuru wa kuzungumza bila uwezo wa kufanya mabadiliko.

Mazuri yote ya serikali ya awamu ya nne yangekamilika kwa dhati kama nchi yetu ingejipatia katiba mpya. Katiba ambayo ingekua chachu ya mabadiliko ya aina yoyote yale hapa nchini.

MSIMAMO WA WANANCHI WAPENDA MABADILIKO.

ni dhahiri kwamba uzito wa swala la katiba mpya hauwezi ukaondolewa kwa tendo jepesi la kumkumba mtu alitukwamisha kama taifa na kutufikisha hapo tulipo.

Kwamba, kitendo cha wapinzani kumkumbuka na kumsifia mtu aliyekwamisha mchakato huu muhimu kinaathiri maslahi ya kimabadiliko ambayo ndio chanzo cha maendeleo ya nchi yoyote.

Kwamba, ni ngumu kuililia katiba mpya kwa kumsifia mtu aliyesababisha tukose katiba hiyo.

Mungu Ibariki Afrika,
Mungu Ibariki Tanzania.

Naomba kuwasilisha.
 

Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,861
2,000
mheshimiwa raisi kikwete alikua anaelekea kuandika historia ya kipekee kwa kuikabidhi Tanzania katiba ambayo ilikua inamaliza matatizo yote.
Hapa ndipo panapojionyesha kuwa mh Kikwete alikuwa hana matatizo yoyote na kuleta katiba mpya na hapa ndipo wapinzani wanapomuona kuwa alikuwa safi,pia alisha wahi kuwambia wanaccm wenzake kuwa wajiandae kisaikolojia kupokea mabadiliko ya serekali 3 kama mapendekezo ya wananchi yaliokuwepo kwenye mapendekezo ya katiba.

Shetani mkubwa ambaye alikuja kumpindua Kikwete mpaka akawasaliti wananchi yuko ndani ya CCM,shetani huyo alifanikiwa kumpindua pia Waryoba,Polepole,Butiku na kuwafanya kuwa kinyume kabisa na wananchi.

Utafikiri siyo wale waliokubaliana na maoni ya wananchi kabla hawajabadilishwa na shetaniccm.
 

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
16,059
2,000
umesema upinzani nao wanasiasa za kinadharia! kwahiyo hatuna viongozi bora tuna bora viongozi..? nilikuja kuhuzunika pale walipoimba tunaimani na kikwete! sijui hata niwaweke kundi gani..!
 

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
9,021
2,000
Awamu ya NNE nchi ilikuwa likizo ya kiuongozi. Nikikumbuka yafuatayo;-
-mgomo wa madaktari.
-kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi
-kauli yake juu ya fedha za escrow
-alivyoanzisha na kuvuruga mchakato wa katiba mpya.

...napata kichefuchefu nikimfikiria aliyekuwa rais wa awamu hiyo, maana alikuwa anaishi ikulu tu na haongozi nchi.

.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom