Kuingilia ugomvi huo haifai Mkuu!Kukaa kwa shemeji..........!
Huo nimtihani mkubwa sana, maana siku akishushiwa kipondo sijui unaingilia kuamulia au au unaugulia pembeni dada akipigwa....!
Wakuu!
Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.
Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!
OK...OK...OK...!
Tufanye basi mume ameondoka, je wadogo zake wataondoka nao?...kwanini?
(Japo hapa najua unapigania ku-retain heshima ya eneo maarufu la huko China-Beijing)
Du!
Inasikitisha sana hii na moyo umeniuma!
Kwahiyo dada ku'behave vyema chumbani kule ni salama ya watu wengi sana huko nje!..du!
Mkubwa,Ukiwa unaishi kwa shemeji tafsiri yake ni kwamba na wewe unakuwa umeolewa
Mkuu,Ni ngumu kutoa jibu la haraka haraka. Nafikiri busara kwa wahusika inahitaji zaidi ya kutumia formula ya kwamba ukigombana na mwenza na mashem pia wanatakiwa kula kona. Swali la kujiuliza ni kuwa hao wanahusikaje na mgogoro wenu? Madhara ni nini baada ya kuondoka nyumbani hapo? Kama ulikuwa ukiwahudumia kwa shule/vyuo, hatma yao ni nini? Ni vzr kuwa na ubinaadamu zaidi ....
Hii ni sawa kabisa na kabila fulani ambalo ukioa binti kwao wanafanya fasta kuwapa sehemu ya kujenga, na baadaye wanachochea mgogoro kati yenu, ili mwanaume uondoke zako na kuiacha nyumba!mi nafikiri kibinadamu wanaweza kubaki, hebu imagine ni wanafunzi.. Wakiondoka itakuwaje? Halafu vipi kama mke na mume wakarudiana, inamaana walioondoka watarudi tena!
Kwa heshima ya beijing inabindi nijenge kibanda changu kabla sijaolewa na huyo mwanaume aje akae kwangu. Tukitibuana anaondoka yeye.
Kukaa kwa shemeji..........!
Huo nimtihani mkubwa sana, maana siku akishushiwa kipondo sijui unaingilia kuamulia au au unaugulia pembeni dada akipigwa....!
haiko clear sana hii mada yako Mkuu, kuna vitu vingi sana unatakiwa kuvifafanua unapozungumzia kufungasha viragoWakuu!
Kwa familia za kiAfrika tuna tabia za ndugu wa kutoka kwa mke na kwa mume kuishi na familia fulani, hasa wanapokuwa katika hali ya kutafuta misaada au kuugua.
Je inakuwaje pale mke na mume wanapokorofishana na kufikia hatua ya mke kufunga virago kurudi kwao...Je ndugu wa upande wa kike wanaondoka au hubaki?..chukulia kuwa hao ndugu si sehemu ya mgogoro wa familia husika, na hawajawahi kushabikia upande wowote!
Mkuu,
Chukulia ugomvi ni serious kidogo, mfano kufumania. Je kama ulikuwa unaishi nao na kuwalipia karo mashemegi zako utasitisha zoezi hilo?
Mkubwa,Umenikumbusha jirani yetu .. kuna jamaa alikuwa anaishi na Shemeji yake (dada yake alikuwa ameolewa hapo). Kuna siku dada yake alikuwa anapigwa ja jamaa (mumewe) huku jamaa kafunga mlango wa chumba.
Jamaa (mdogo mtu) akaenda kwa dirishani akasema kwa sauti kubwa "Shemeji! ... Shemeji! ... ukimuwuwa dada na wewe utawuwawa!"
Majirani tuliokuwepo hapo nje kuamulia ugomvi tulijikuta tunaangusha vicheko kwa namna jamaa alivyokuwa anaongea Lafudhi yake ... katokea Bush na bado alikuwa na Ushamba flani.
Tokea siku hiyo jamaa amekuwa anataniwa na watu wake walio-karibu nae huwa wanamuambia "Shemeji! ... Shemeji! ... ukimuwuwa dada na wewe utawuwawa!"