'kuishi kwa dada'

Lazima mume awe na uwezo eh?
BTW sakapal salama??

Salama SnowBall
yeah coz kama mume hana uwezo atakaye kuja kaa hapo kwa shemejiye wa kubangaiza atakuwa anatafuta kugombanisha ndoa ya dada yake tu au labda mume hana uwezo ila dada yake kazikamata na hapa ni shida coz atajidai mali za sister, kwa wali wanawake waliofundwa hapa wataambia ndugu zao hz mali za mwanume sio zangu ili kuweka heshima kwa mumewe asionekane choka mbaya, na ufanye hivo halafu mwanaume mwenyewe akutende looh kazi kweli utakuwa unafanya wema then unaishia hungoji shukrani kweli yataka moyo...
 
SnowBall acha hiyo habari hata kijana kukaa kwa kaka mtu mawifi huwa wanawatesa sana mimi nina kaka yangu anasoma hapo udsm alikuwa akifunga chuo anajiegesha kwa kaka yangu lo alikuwa anafanyiwa visa mpaka eeehu basi mimi mdogo wake nikamwambia isiwe shida njoo kaa kwanguuuu ila mbona haokuwa shda inategemea sana huyo mme wa dadayak akoje ukikuta ndio kamwokota baa basi atawanyanyasa wote

Amsterdam Nimelileta hili kwa sababu inakuwa kama vile kukaa kwa dadaako ni laana..
Nafahamu kila mtu anatakiwa awe na maisha yake in future..lakini ikumbukwe pia tunakaa kwa ndugu zetu wakati tukiwa bado tunajitafutiza..Kwa nini wanaokaa kwa dadazao kipindi hiki cha mpito waonekane 'hawana maana'!!
 
Last edited by a moderator:
Mr Rocky Is this the reason?..Na je kama kama yupo kaka au mdogo wa mume?..is it acceptable?

Nakubaliana na mawazo ya gfsonwin na ya kwako SnowBall
Kwa vyovyote vile najua ugumu wa wewe kijana kama mwanachuo unahitaji usave ili upambane na maisha
Au ni wewe mwanafunzi wa sekondari unatakiwa ujibane ili upate sehem ya kukaa na kusoma
Kwa malengo hapo nakubaliana na wengi kuwa kuna muda kweli hali hairuhusu inabidi ujibane kwa sister ili kukidhi lengo na huku ukifanya fanya na vikazi vya pale home kusaidia
Ila sasa inapofikia ni kijana wa kiume umri umeenda sio kwa malengo ya kumaliza shule uondoke zako ila unakaa kwa sister bila mpango wowote
Awe ndugu wa mume au wa mke unapojikuta katika mazingira ya kuishi kwa dada yako huna mpango wowote umekaa kaa tuu khasara hapo tena huna cha kujitetea
Unawanyima watu uhuru wao ambao wanautaka
 
Last edited by a moderator:
Tatizo kubwa naloona ni watu kukosa UPENDO, na hii huanza toka tukiwa wadogo...ni jinsi gani tuko connected na ndugu zetu.

Hata ile kuona mtu kama Masanja anatania wanaokaa kwa dada zao ni kuwa anaona hajabu kwa kuwa yeye hana feelings za kuona hawezi ku enjoy maisha wakati ndugu zake wanashindia mlo mmoja...na yeye anakula na kumwaga vyakula. Watoto wengi wanazaliwa na mzazi mmoja lakini bado unakuta ni paka na chui.

Mi nawaonea wivu kabisa wanaoishi na wadogo zao/kaka zao wa kiume kwa kuwa najua wanatoka kwenye familia ambayo iko blessed.

Kuna dada nilisoma nae o'level na A 'level. Wazazi wake ni wako fresh sana..mama na baba wote ni maboss wakubwa. Wadogo wa mama yao na wadogo wa baba yao wote walilelewa na wazazi wa huyu dada. Na wakati tuko boarding huyu dada alikuwa anapokea EMO za kumwaga toka kwa aunties and uncles wake; wanalipa fadhila ingawa wazazi wake bado walikuwa wako fresh kipesa.

Ukoo wote umeendelea sasa kwa sababu mama na baba yake hawakuwa selfish.

Mimi mwenyewe siwezi sema familia yetu ina highest level ya Upendo ndo maana nasema nawaonea wivu familia ambazo zina umoja.
 
Hiyo ni kama social security kwa masikini...hata mtu akifa anajua watoto wake wataendelea ku enjoy maisha kama yuko hai kwa kuwa kuna ndugu ambao hawatawaona mzigo.
 
Mi nawaonea wivu kabisa wanaoishi na wadogo zao/kaka zao wa kiume kwa kuwa najua wanatoka kwenye familia ambayo iko blessed..

Well said nyumba kubwa ..
How do you consider issue ya time?
How long shall a person stay to his/her relatives..in this case kwa dada?
 
Last edited by a moderator:
Badala ya kusema ndugu yako amekaa kihasara kwa nini usimsaidie ili naye atoke???
Ni sahihi kumwambia aende anakokujua kwa kuwa hana dira ya maisha?? Akijiua utalia??

Unless huyo ndugu awe mvuta bangi ambaye nae anaweza kupata ushauri nasaa...badala ya kumdhiaki ndugu yako kuwa anakaa kula kulala unapaswa ufikirie ni jinsi gani ya kumsaidia ili nae ajitegemee. Hakuna anayependa kuwa tegemezi..kuna sababu kama kukosa capital au elimu.

Nakubaliana na mawazo ya gfsonwin na ya kwako SnowBall
Kwa vyovyote vile najua ugumu wa wewe kijana kama mwanachuo unahitaji usave ili upambane na maisha
Au ni wewe mwanafunzi wa sekondari unatakiwa ujibane ili upate sehem ya kukaa na kusoma
Kwa malengo hapo nakubaliana na wengi kuwa kuna muda kweli hali hairuhusu inabidi ujibane kwa sister ili kukidhi lengo na huku ukifanya fanya na vikazi vya pale home kusaidia
Ila sasa inapofikia ni kijana wa kiume umri umeenda sio kwa malengo ya kumaliza shule uondoke zako ila unakaa kwa sister bila mpango wowote
Awe ndugu wa mume au wa mke unapojikuta katika mazingira ya kuishi kwa dada yako huna mpango wowote umekaa kaa tuu khasara hapo tena huna cha kujitetea
Unawanyima watu uhuru wao ambao wanautaka
 
Kwenda kumsalimia kwa siku moja au mbili na kuondoka sio tatizo. Ila kuhamisha kabisa majeshi unakaa utadhani upo kwako haifai. Mwanaume lazima apambane kuwa na kwake siyo kuishi kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako. Kama dada ameolewa iko siku mtatukanwa ukoo wenu mzima na shemeji kisa kakorofishana na mkewe ambaye ni dada yako.
 
Badala ya kusema ndugu yako amekaa kihasara kwa nini usimsaidie ili naye atoke???
Ni sahihi kumwambia aende anakokujua kwa kuwa ana dira ya maisha?? Akijiua utalia??

Unless huyo ndugu awe mvuta bangi ambaye nae anaweza kupata ushauri nasaa...badala ya kumdhiaki ndugu yako kuwa anakaa kula kulala unapaswa ufikirie ni jinsi gani ya kumsaidia ili nae ajitegemee. Hakuna anayependa kuwa tegemezi..kuna sababu kama kukosa capital au elimu.

nyumba kubwa ngoja nikuambie kitu
Kuna watu ambao wanasaidiwa na hawajui thamani ya msada unaowapa
Kuna watu wanashauriwa ila hawajui thamani ya huo ushauri wala hawausikilizi
Kuna watu wanapewa hadi mitaji kwa ajili ya kujiendeleza au kupewa elimu ila bado anarudi kwako bila kuwa na lolote la kumsaidia maishani mwake
Sio kwamba watu hawapendi kukaa na ndugu ila mazingira yanayosababishwa na wale ambao hawajui thamani hiyo ndio yanayowafanya watu wadoubt
 
Last edited by a moderator:
Kwenda kumsalimia kwa siku moja au mbili na kuondoka sio tatizo. Ila kuhamisha kabisa majeshi unakaa utadhani upo kwako haifai. Mwanaume lazima apambane kuwa na kwake siyo kuishi kwa mtu mwingine hata kama ni dada yako. Kama dada ameolewa iko siku mtatukanwa ukoo wenu mzima na shemeji kisa kakorofishana na mkewe ambaye ni dada yako.

Tata why so many people think in that way?..Nadhani ni kuwavunjia heshima wakwe..i bet hata kama mtu umekosana na binti huwezi kutukana ukoo wake!!..unless the reason ya tatizo iwe ndugu wenyewe..which also is rare as most problems kwenye ndoa zinakuwa inflicted na infedility..
 
Last edited by a moderator:
Mhhh SnowBall kun amambo ambayo kweli huwezi kufanya na kuna mipaka ya kuka akwa dada
Sijaona faida wala la maana kwa kaka mztu mzima kukaa kwa dada yako awe ameolewa au hajaolewa
na sio mbaya kwa dada kumlea kaka yake
Ila je uhuru wako au uhuru wake ukoje
Tuseme ameolewa yuko na mumewe hapo hapo home
Huoni kama unamyima raha kufanya kile ambacho angefanya kwa mkewe
Maana yeye anajua amemuoa dada yako na ana uwezo wa kumkiss na kufanya utundu wowote na mkewe
Sasa akiwa anafanya huo utundu wewe kaka yake unafeel vipi
Na je kama hajaolewa uhuru wake wa kuja na mwanaume wake ukoje huoni kama unamuingilia na hayuko huru
Maana pale ni kwake yuko huru kuja na mwanaume wake maana ni nyumba yake
Na je wewe nawe kama mwanaume unaweza kuja na gal wako pale na dada yako anakuonaje
na sio mmoja tuu kama kaka mtu anawabadilisha kama nguo hapo ikoje kwa dada
Kwenye nyumba dada najiamini anatoka na kanga moja maana yuko kwake mkakutana kwenye corridor hapo inakuwaje
Ahh mambo mengine sio ya kuombea au kuzungumza mkuu

Mkuu Rocky amenisemea yote, lakini pia jamii ina mchango mkubwa sana katika kuliweka hili jambo kuwa kama kitu kisichopendeza.................
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Rocky amenisemea yote, lakini pia jamii ina mchango mkubwa sana katika kuliweka hili jambo kuwa kama kitu kisichopendeza.................

Mkuu Mtambuzi hapo kwenye red ndio nilitaka upasemee bro..come on buddy!
 
Last edited by a moderator:
Tata why so many people think in that way?..Nadhani ni kuwavunjia heshima wakwe..i bet hata kama mtu umekosana na binti huwezi kutukana ukoo wake!!..unless the reason ya tatizo iwe ndugu wenyewe..which also is rare as most problems kwenye ndoa zinakuwa inflicted na infedility..

Mheshimiwa haya mambo ya kutukanwa ukoo mzima yapo sakwa makosa ya mtu mmoja yapo sana. Nimeyashuhudia kwenye kesi za mashemeji. Kwa kiasi kikubwa yanatokana na mila na desturi zinazohusianisha tabia fulani fulani na kurithi kwenye ukoo. Ndio maana zamani watu walikuwa wanafuatilia historia ya ukoo wa binti au bwana kujua tabia potofu (kama wizi sugu, ulevi sugu, mauaji etc.) au magonjwa (kama sickle cell, asthma etc.) ambayo yanaweza kurithiwa ikiwa mtaingia kwenye mahusiano ya ndoa. Sasa wengine wanatumia hiyo knowledge kuwadhalilisha wenzi wao.
 
Mkuu Rocky amenisemea yote, lakini pia jamii ina mchango mkubwa sana katika kuliweka hili jambo kuwa kama kitu kisichopendeza.................

Mtambuzi kuna watu wanasemea haya mambo ya extended family sijui wakati wa kusoma na mambo kama hayo
Ila nayo yana muda wake bana
Huwezi kusema kusaidiana unakaa na kaka yake anafanya kazi ila bado anaishi kwako kisa extended family
Huwezi kuendelea kukaa na kaka yako ambaye amemaliza masomo na hujaona juhudi zake za kutafuta kazi kisa tuu ni kuwa unataka umsaidie
Kuna mipaka na umri pia
Usitake kuniambia kaka yako ana miaka 30 bado yuko kwako unazidi kumsaidia kisa extended family au sijui kwenu kuna matatizo
Duh kuwe na mipaka bana
 
Last edited by a moderator:
Hizo exceptional cases zipo nakubali.

Ila kuna watu ambao wala hawajaribu.

Tena wakiwa na maisha mazuri hata kwao huko vijijini hawakanyagi kwa kuwa ndugu zake ni wa chini sana yeye ni matawi. Na ukute kaoa familia bora ndio kabisaaaa. Hata watoto hawatakaa wakanyage kwa bibi na babu...yani mtu anajitenga na familia.

Kusaidia ni muhimu sana ingawa najua msaada unabidi uwe ndani ya uwezo wako na si kuitesa familia na watoto.

Nina aunt yangu ni mwalimu wa primary lakini amesomesha wadogo zake na sasa ni maofisa; na wengi walikuwa wanakaa kwake mpaka wameanza kujitegemea. Wanaume hawanaga roho mbaya ila ni sisi wanawake hatutaki saidia ndugu zetu. Mume anayekupenda hawezi chukia ndugu zako.

nyumba kubwa ngoja nikuambie kitu
Kuna watu ambao wanasaidiwa na hawajui thamani ya msada unaowapa
Kuna watu wanashauriwa ila hawajui thamani ya huo ushauri wala hawausikilizi
Kuna watu wanapewa hadi mitaji kwa ajili ya kujiendeleza au kupewa elimu ila bado anarudi kwako bila kuwa na lolote la kumsaidia maishani mwake
Sio kwamba watu hawapendi kukaa na ndugu ila mazingira yanayosababishwa na wale ambao hawajui thamani hiyo ndio yanayowafanya watu wadoubt
 
acha tu nipite.....

maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...

hivyo acha nisonge mbele.....

chukua zangu tano.....
 
Hizo exceptional cases zipo nakubali.

Ila kuna watu ambao wala hawajaribu.

Tena wakiwa na maisha mazuri hata kwao huko vijijini hawakanyagi kwa kuwa ndugu zake ni wa chini sana yeye ni matawi. Na ukute kaoa familia bora ndio kabisaaaa. Hata watoto hawatakaa wakanyage kwa bibi na babu...yani mtu anajitenga na familia.

Kusaidia ni muhimu sana ingawa najua msaada unabidi uwe ndani ya uwezo wako na si kuitesa familia na watoto.

Nina aunt yangu ni mwalimu wa primary lakini amesomesha wadogo zake na sasa ni maofisa; na wengi walikuwa wanakaa kwake mpaka wameanza kujitegemea. Wanaume hawanaga roho mbaya ila ni sisi wanawake hatutaki saidia ndugu zetu. Mume anayekupenda hawezi chukia ndugu zako.

nyumba kubwa katika vitu ambavyo napenda watoto wangu wakue wakivijua ni kuwa kuna kijiji ambacho mimi nimetokea au mama yao ametokea
So mara kwa mara nawapeleka huko wakakae na babu na bibi zao na ikiwezekana na watoto wa pale kijijini waone maisha ya kijijini yakoje
Huo ni ulimbukeni mkubwa sana kujitenga kisa umefanikiw akimaisha au uko matawi ya juu kuwasahau ndugu zako na ulikotoka
Nakubaliana na wewe kusaidia ndugu kuwe na limit na umri pia
Sio ndugu amefikia umri wa kuoa bado anakaa kwa sister haileti hata picha bana
 
Last edited by a moderator:
Mi najua tatizo ni kuiga western culture huku tunasahau kuwa kwa wenzetu serikali zina mfumo wa kuhudumia watu wasio na uwezo/ wasio na kazi na wazee.

Tamaduni zetu za kibantu zinakufa wakati context ilotufanya tuwe na hizi tamaduni haijabadilika...umasikini

Ona Kenyans wanavyotoka. Kuna dada nilikuwa nae huku ugahibuni ananmbia anasomeshwa na ukoo.

Watu wanashindana ili koo zao zisiwe nyuma...sisi tukitoka tunafanya juhudi kuhakikisha hakuna wa kutukaribia ili tuendelee kusujudiwa.

Mtambuzi kuna watu wanasemea haya mambo ya extended family sijui wakati wa kusoma na mambo kama hayo
Ila nayo yana muda wake bana
Huwezi kusema kusaidiana unakaa na kaka yake anafanya kazi ila bado anaishi kwako kisa extended family
Huwezi kuendelea kukaa na kaka yako ambaye amemaliza masomo na hujaona juhudi zake za kutafuta kazi kisa tuu ni kuwa unataka umsaidie
Kuna mipaka na umri pia
Usitake kuniambia kaka yako ana miaka 30 bado yuko kwako unazidi kumsaidia kisa extended family au sijui kwenu kuna matatizo
Duh kuwe na mipaka bana
 
acha tu nipite.....

maana sidhani kama kuna mtu anapenda kuishi kwa dada au kaka yake au ndugu yoyote....
nadhani ni ugumu na matatizo ya dunia....
sema kwa vile mtu hatembei na bango la matatizo yake mtu huwezi kuona wala kujua zaidi ya kunyoosha vidole...

hivyo acha nisonge mbele.....

Well spoken mkuu,nimependa busara zako
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom