Kuishi jirani na wazaaramo/Wandengereko utakoma!

Kuishi jirani na wazaaramo/Wandengereko utakoma!

ARCHBISHOP

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2012
Posts
271
Reaction score
488
Dah! Ndugu zangu, tumefundishwa kuvumiliana, japo kinachoendelea hapa jirani ni matatizo, Kuna nyumba ya Wazaramo wamemwoza kijana wao, bibi harusi ni mdengereko, aisee!!...., tokea jana mida ya saa kumi unapigwa mziki mpaka sasa hawajazima. Ni mwendo wa taarabu, singeli...., Mtaa mzima hatuelewani!! Dah!
 
Tangu jana? Hapana, ninavyojua Mangu aliacha onyo la muziki mwisho saa sita usiku ndiyo maana vurugu za mzee Maulana na ukoo wake siku hizi zimepungua
 
Pole usiombee ukute ngoma inaaza Alhamis kuisha j2 ukiacha Fujo mtaani Ila wana afya zao za kukesha. Pole mtoa Mada wazoee watani Zangu.
 
Tangu jana? Hapana, ninavyojua Mangu aliacha onyo la muziki mwisho saa sita usiku ndiyo maana vurugu za mzee Maulana na ukoo wake siku hizi zimepungua
Hawa wamemshinda. Nimwendo wa viduku
 
Tangu jana? Hapana, ninavyojua Mangu aliacha onyo la muziki mwisho saa sita usiku ndiyo maana vurugu za mzee Maulana na ukoo wake siku hizi zimepungua
Naomba kumtambua mzee maulana mkuu
 
Naomba kumtambua mzee maulana mkuu
Ukifika Mwananyamala kwa Kopa, mwambie Bodaboda yeyote akupeleka kwa mzee Maulana chaukucha, akisema hapajui, mwambie mjukuu wake alicheza kwenye wimbo wa AT unaitwa vifuu tundu
 
Jaman acha hyo miziki ,enzi zetu za ujana mitaa ya Ilala tulikua tunakesha nayo,siku hizi eti mwisho saa sita duh.
 
Acha kuwasema wazaramo na wandengereko, kwa waafrika kalele hazijawahi kuwa tatizo la jamii, labda kama uliwahi ishi ulaya ndo utaona ni tatizo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom