Haya maisha niliyaona kwa Wanigeria wakikaribishana London. Wanaishi chumba kimoja kaka, shemeji, mtoto na mgeni. Inabidi shemeji atafutiwe kazi ya usiku, wakati anarudi kaka na shemeji wanatoka na mtoto anaenda shule. Hali ni ngumu lakini kuliko ndugu yako alale barabarani inabidi umsaidie.
Mgeni inabidi awe na akili za ziada, weekend kama wote hawaendi kazini, mgeni analala kwenye sofa. Ukienda bafuni unabeba vifaa vyote unavyohitaji kubadili. Baada ya chai lazima uelewe hawa ni wana ndoa, toka kazuge mtaani unarudi jioni.
Msiishi hivyo kwa muda mrefu, mgeni akipata mshahara wa kwanza anatafuta chumba chake.