Kuibuka kwa wananchi wakiwa na Mabango ya kero mbele ya Rais Magufuli. Je, ni Kushindwa kwa viongozi wa kisiasa na watendaji mbalimbali?

Freed Freed

JF-Expert Member
Jun 27, 2017
6,262
6,514
Kumekuwa na tabia iliyozoeleka Sasa ya wanainchi wakiwa na Mabango ya kero mbalimbali mbele ya Rais Magufuli. Hii ni Ktk ziara zake mbalimbali za kuwatumikia wanainchi.

Je, hali hii inamaanisha ni Kushindwa kwa viongozi wa kisiasa/ wawakilishi na watendaji/ watumishi wa umma katika kazi zao?
 
Kuonekena kwa mabango hayo ni kiashiria chanya kuonyesha nchi yetu it's a ONE show MAN,nchi inahitaji TAASISI imara zinazojitegemea na italeta hali ya utawala bora na sio kutegemea mpangaji mkuu wa pale Magogoni,generation iliyopo sasa ni mabingwa wa key boards ila itakayokuja itakuwa tofauti kabisa na hii ya kwetu muda huu.
 
Haya maigizo wanafanya ili anayejiita mtetezi wa wanyonge aonekane kweli anatetea wanyonge
Nadhani wale kina mama huwa wamepangwa, kama yule mchoma mahindi, mwenye mguu wa kuku kiunoni.
 
Niliwahi kufanya kazi katika kampuni moja ya kilimo ya wazungu mkoani Iringa. Unakuta shida ndogo tu ambayo mimi ningeweza kutatuta ila mwanakijiji anakwambia "sitaki kuongea na wewe, nipe number ya simu ya boss wako mzungu ndio atanisaidia"

Kwa hiyo sisi binadamu tuna hulka sana ya kupenda kupewa attention ya mamlaka za juu pamoja na watu wenye status kubwa ndani ya jamii.
 
Kumekuwa na tabia iliyozoeleka Sasa ya wanainchi wakiwa na Mabango ya kero mbalimbali mbele ya Rais Magufuli. Hii ni Ktk ziara zake mbalimbali za kuwatumikia wanainchi.

Je hali hii inamaanisha ni Kushindwa kwa viongozi wa kisiasa/wawakilishi na watendaji/watumishi wa umma ktk kazi zao?
KWA SABABU KAZI YAO IMEHAMA(WAMEACHA KAZI YA) KUTOKA KUHUDUMIA WANANCHI HADI KUMUABUDU NA KUMTUMIKIA RAIS
 
Niliwahi kufanya kazi katika kampuni moja ya kilimo ya wazungu mkoani Iringa. Unakuta shida ndogo tu ambayo mimi ningeweza kutatuta ila mwanakijiji anakwambia "sitaki kuongea na wewe, nipe number ya simu ya boss wako mzungu ndio atanisaidia"

Kwa hiyo sisi binadamu tuna hulka sana ya kupenda kupewa attention ya mamlaka za juu pamoja na watu wenye status kubwa ndani ya jamii.
Mkulima alikuwa sahihi kwa sababu Mzungu alikuajiri wewe uwasaidie Wakulima lakini ukawa huwasaidii kwa hiyo wakimpigia simu tu wakawa wanasaidiwa ndo maana wewe siyo mwajiriwa tena wa Mzungu, ulitumbuliwa. Vivyo hivyo wananchi wanamfuata Mteuaji na mabango kudai haki zao kwa sababu wateule wake aliowajaza huko kwao
hawawasaidii wapo tu wanangoja maagizo toka kwake ambayo hayaji na kama yatakuja siyo ya kutatua matatizo yao bali ya kusifia na kuunga mkono juhudi. Tofauti na yule Mzungu anayewasaidia Wakulima na kutumbua wafanyakazi wake wazembe, huyu licha ya watu maelfu na mabango wanaomfuata, atasaidiwa mmoja tu kwa kumgawia mamilioni au kununua jogoo mmoja tu kwa Sh. Laki moja kujionyesha badala ya kununua majogoo 10 ya wauzaji 10 kwa Sh. 10,000 kila jogoo angekuwa amesaidia familia 10. Wateule wake ni homeboys hawatenguliwi!
 
Ni kweli watendaji wa serikali wengi wao ni miungu watu sijui huwa wanawaza nn wakiwa maofisini jaman yaan unakuta shida ndogo tu au umepeleka barua inachuku mwenzi kupata majibu ya siku moja...hasa manispaa na wilaya.
 
Maigizo...niliwaona kule.Ushirombo wanayaandaa mahali kabla mkulu hajafika nika dharau..majuzi
 
Ni kweli watendaji wa serikali wengi wao ni miungu watu sijui huwa wanawaza nn wakiwa maofisini jaman yaan unakuta shida ndogo tu au umepeleka barua inachuku mwenzi kupata majibu ya siku moja...hasa manispaa na wilaya.
Ukweli mtupu
 
Funguka vizuri.
Sema ccm japo wako peke yao madarakani lkn wamekosa ushawishi kwa wananchi,

zaidi ushawishi wao unalazimishwa na matumizi ya bunduki
Kumekuwa na tabia iliyozoeleka Sasa ya wanainchi wakiwa na Mabango ya kero mbalimbali mbele ya Rais Magufuli. Hii ni Ktk ziara zake mbalimbali za kuwatumikia wanainchi.

Je, hali hii inamaanisha ni Kushindwa kwa viongozi wa kisiasa/ wawakilishi na watendaji/ watumishi wa umma katika kazi zao?
 
Mkulima alikuwa sahihi kwa sababu Mzungu alikuajiri wewe uwasaidie Wakulima lakini ukawa huwasaidii kwa hiyo wakimpigia simu tu wakawa wanasaidiwa ndo maana wewe siyo mwajiriwa tena wa Mzungu, ulitumbuliwa.
Nilitumbuliwa ndio maana nikaamua kuwa Taxi Driver. Karibu sana nikupe huduma
 
Back
Top Bottom