Meneja Wa Makampuni
JF-Expert Member
- Jul 7, 2020
- 6,328
- 8,246
Kuibadili gesi asilia yetu kuwa mafuta ya petroli na dizeli kunaweza punguza gharama tunazotumia kuagiza mafuta hayo kutoka mataifa ya nje
Ni hivi wakuu,
Gesi asilia imeundwa kwa kampoundi zinazoitwa methane (CH4). Kampaundi hizo zina kaboni moja na hydrojeni nne.
Petroli imeundwa kwa kampoundi zenye kaboni kuanzia 6 hadi 12.
Dizeli imeundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 12 hadi 20.
Mafuta ya taa yameundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 9 mpaka 16.
Mafuta ya ndege yameundwa kwa kampaundi zenye kaboni kuanzia 9 mpaka 16.
Wakati wa kuibadili gesi asilia kuwa mafuta, hapo kinachofanyika ni kufanya miungano ya kikemikali kuzibadili hizo kampaundi za methane zenye kaboni moja zilizomo ndani ya gesi asilia kutupatia kampaundi zenye kaboni kuanzia sita hadi 20 na zaidi ambazo zinapatikana kwenye mafuta.
Kisha kinachofanyika baada ya hapo ni kufanya utenganisho wa kikemikali kupata petroli, dizeli, mafuta ya taa, LPG, na prodakti zingine.
Hatua ya kwanza gesi asilia inabidilishwa kuwa kaboni monoksaidi na hydrojeni gesi.
Hatua ya pili monoksaidi na hyrojeni ziaungana kutengeneza kampaundi zenye kaboni nyingi na hydrogeni nyingi.
Hatua ya tatu kampaundi zenye kaboni nyingi na hydrojeni zilizotengenezwa zinatenganishwa kutoa petroli, dizeli, mafuta ya taa, mafuta ya injini, nk.
Njia nyingine niya kutengeneza petroli moja kwa moja.
Hapa hatua ya kwanza gesi asilia inabadilishwa kuwa koboni monoksaidi na hydrojeni.
Hatua ya pili kaboni monoksaidi na hydrojeni zinaunganishwa kutengeneza methanol.
Hatua ya tatu methanol inabadilishwa kuwa petroli.
Hivi ndivyo wenzetu CHINA, SOUTH AFRICA, na mataifa mengine wanavyoibadilisha gesi asilia kutengeneza mafuta.
Hii ndio tunaita natural gas value chain to get valueble products. Au Natural Gas utilization.
Kwenye Tanzania Natural Gas Utilization Master Plan ya Wizara ya Nishati 2016 hadi 2045 hivi viwanda vyote vipo. Na hesabu zilishapigwa kilichobaki ni utekelezaji tu.