Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Wamasai, watu wanaovutia na wanaofuga wanyama, wanaishi katika pori la Bonde Kuu la Ufa nchini Kenya na Tanzania huku Afrika Mashariki. Wao bado huishi kama vile mababu wao wa kale walivyoishi zamani. Watu hao hawajali saa, bali hufanya kazi zao kuanzia mapambazuko hadi machweo, na kwa kufuatana na majira.
Wamasai wana ustadi unaohitajika kuishi katika pori la Bonde la Ufa. Wao hutembea mbali sana kutafuta malisho na maji kwa ajili ya mifugo yao, nao huchunga mifugo miongoni mwa makundi ya kongoni, punda-milia, twiga, na wanyama wengine wanaoishi katika pori hilo.
Wamasai wanaamini kwamba ng’ombe wote duniani ni mali yao. Imani hiyo inatokana na hekaya inayosema kwamba hapo mwanzoni Mungu alikuwa na wana watatu, naye alimpa kila mmoja zawadi. Yule wa kwanza alipokea mshale wa kuwindia, yule wa pili alipokea jembe la kulimia, na yule wa tatu alipokea fimbo ya kuchunga ng’ombe. Inasemekana kwamba yule mwana wa mwisho alikuwa babu wa kale wa Wamasai. Ijapokuwa watu wa makabila mengine wanafuga ng’ombe, Wamasai wanaamini kwamba ng’ombe hao ni mali yao.
Nyumba za Wamasai hujengwa na wanawake, nazo hujengwa kwa matawi na nyasi na kisha hukandikwa kwa samadi ya ng’ombe. Nyumba za Wamasai ni zenye umbo la mstatili nazo huzunguka boma ambamo ng’ombe hulala usiku. Nje ya nyumba hizo kuna ua wa matawi yenye miiba unaowalinda Wamasai na ng’ombe zao dhidi ya fisi, chui, na simba wanaowinda usiku.Wamasai ni watu warefu, wembamba, na wenye sura nzuri. Wao hufunga mashuka yenye rangi nyangavu nyekundu na samawati. Wanawake hujirembesha kwa kuvalia mkufu mpana wenye shanga, na mapambo ya vichwani yenye rangi nyingi. Nyakati nyingine mikono na miguu hukazwa kikiki kwa nyaya nyingi nene za shaba. Wanawake na wanaume hurefusha masikio yao kwa kuvaa mapambo na vipuli vizito vyenye shanga. Madini mekundu yaliyosagwa huchanganywa na mafuta ya ng’ombe nayo hutumiwa kupamba mwili.
Vijana wanapokuwa wakubwa, wao hujifunza mila na sherehe wanazohitaji kupitia ili wawe watu wazima. Miongoni mwa mila ambazo wao hujifunza ni zile zinazohusu magonjwa, bahati mbaya, ndoa, na kifo. Wamasai huamini kwamba wasipofuata mila hizo watapatwa na balaa.
Wazazi wa msichana Mmasai wanaweza kupanga ndoa yake akiwa kitoto. Msichana huyo huposwa na mwanamume aliye na mifugo ya kutosha kulipa mahari ambayo babake atatoza. Mara nyingi wasichana huolewa na wanaume walio na umri mkubwa kuliko wao, ambao tayari wana wake wengine.
Mila za pekee na utamaduni wa Wamasai unatoweka kwa haraka siku hizi. Katika maeneo mengine, Wamasai hawawezi tena kuhamahama na mifugo yao ili kutafuta malisho bora. Sehemu nyingi za nchi yao ya zamani zinafanywa kuwa mbuga za wanyama, au kutumiwa kwa ajili ya ujenzi wa nyumba, na ukulima. Wamasai wengi hulazimika kuuza ng’ombe zao wapendwa kwa sababu ya ukame na hali mbaya ya kiuchumi. Wamasai wanapohamia miji mikubwa, wanakumbwa na matatizo yaleyale yanayowapata watu wengine siku hizi