Kuhusu Video ya Liberian Girl ya Michael Jackson

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,416
6,577
Habari zenu wakuu...

Michael Jackson enzi za uhai wake alipata kutoa vibao mbalimbali mojawapo kikiwa ni Liberian Girl ambacho ndani yake kuna maneno adhimu ya lugha ya Kiswahili, Nakutaka pia, Nakupenda pia, Mpenzi wee! Sijui aliyapata wapi? Ila yalinogesha wimbo huo.

Ila kinachofurahisha katika video ile ni kuwa, MJ alitumia ubunifu mkubwa sana. Aliwaalika marafiki zake wa karibu kwa ajili ya kurekodi video rasmi ya wimbo huo.

MJ aliwahi sana eneo la kukutania kwaajili ya kushoot video (Aliwahi kabla ya muda uliopangwa), akajificha sehemu na kuanza kurekodi baadhi ya matukio ya watu wakiwasili eneo la tukio, huku akiwarekodi wengine waliokuwa wanafanya mazoezi ya kama sehemu ya maandalizi ya kwenda kushoot video husika.

Watu wote wakawasili na wakaanza kumsubiria MJ huku wengine wakikosa uvumilivu na kuanza kulalamika mbona MJ amechelewa sana? Wasijue kuwa MJ yupo anawarekodi tu muda mrefu.

Baadae MJ akajitokeza toka juu alipokuwa anawarekodi jamaa zake bila wao kujua,wengi walishangaa sana, na kutokana na ubora wa yale matukio aliyoyarekodi MJ akaamua vipande vile ndio vitumike kama Video rasmi ya wimbo wa Liberian Girl hivyo akawatangazia jamaa na marafiki zake waliojitokeza kwa wingi kurekodi video hiyo kuwa hakutakuwa na zoezi la kushoot tena video ya wimbo huo.

Huu wimbo ni dedication kwa Elizabeth Taylor, binti wa kiingereza na rafiki wa karibu wa MJ ambaye inaaminika walikuwa wapenzi, vyanzo vingine wakisema ni marafiki tu wakawaida.
 
mtoa mada " Utaniliza bure' namuelewa sana Mj " kifo chake kimeniachia kovu moyoni halitofutika kamwe" ulipoutaja huo wimbo ubongo wangu umesafiri faster na kuanza kuwaona wale characters waliohusika kwenye ile video " nimemuona mzee don king akiwa na yule sokwe wa Michael na Elizabeth Taylor mwenyew " dahhh alikuwa ni demu matata sana "... fikira zikanipeleka mpaka pale ambapo Michael anashuka kwenye crane akiwa na camera


gone too soon Michael Jackson
 
Kuna mzungu mmoja nlimwambia unajua kiswahili kipo juu sana nkamtajia wimbo huu kuwa ya maneno ya kwanza ni yakiswahili akashangaa sana hadi akawainterested kujua swahili
Hatuna hulka ya kujitangaza, AGT ya 2018 kuna kwaya ya kiswahili iliimbwa watu wakaipenda na hadi jaji mmoja alikuwa na shauku na kutaka kujua ile lugha (kama kumbukumbu zipo vizuri) ila sikuona hata mwanakwaya mmoja akidhubutu kuelezea na kupromote lugha.
 
mtoa mada " Utaniliza bure' namuelewa sana Mj " kifo chake kimeniachia kovu moyoni halitofutika kamwe" ulipoutaja huo wimbo ubongo wangu umesafiri faster na kuanza kuwaona wale characters waliohusika kwenye ile video " nimemuona mzee don king akiwa na yule sokwe wa Michael na Elizabeth Taylor mwenyew " dahhh alikuwa ni demu matata sana "... fikira zikanipeleka mpaka pale ambapo Michael anashuka kwenye crane akiwa na camera


gone too soon Michael Jackson
Pole sana
 
Back
Top Bottom