Kuhusu ukweli

Shayu

Platinum Member
May 24, 2011
608
1,653
Wale wanaopenda ukweli hawaangalii nani kauongea, ana umaarufu kiasi gani, ana cheo kiasi gani au ana kiasi gani katika akaunti yake benki. Ukweli ni ukweli hata ukiongewa na mtu mwenye viraka kwenye nguo zake una baki kuwa ukweli. Ingawaje watu wanadharau maneno yatokayo kinywani mwa mtu asiye maarufu au asiye na cheo au asiye na utajiri. Hii ni illusion ambayo tunayo.

Jiangalie kwa ukaribu usije ukawa mnafiki. Usimpe sifa mtu asiyestahili kisa cheo chake au fedha zake au kwasababu unataka kitu kutoka kwake. Sikiliza kila mtu . Usimpambe speak the truth always.

Je Kipi kinachofuatwa? neno au nani aliyelisema neno?

Neno linabaki kuwa neno liwe limetoka kinywa kwa maskini au tajiri kwa mtu maarufu au siye maarufu. Ni lile lile neno.

Lakini kushabikia neno la kipuuzi kisa limetoka kwa mwenye cheo, maarufu au tajiri ni upumbavu wa hali ya juu.

Usitafute nani kasema neno nenda deep angali mantiki ya neno. Judge it liweke kwenye mizani. Tafuta ukweli kuhusu neno na likuongoze .
 
Back
Top Bottom