Kuhusu Tamasha La Anti- Virus- Utetezi Wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kuhusu Tamasha La Anti- Virus- Utetezi Wangu

Discussion in 'Entertainment' started by maggid, Dec 5, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Dec 5, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Usiku huu nime-google jina langu ndipo nimekutana na habari hii; ' Maggid Mjengwa ana virus?

  Nimejadiliwa katika angle hiyo kwa kile kilichodaiwa na mwanzisha mada kuwa Mjengwablog haikurusha picha za tamasha la anti virus.

  Ukweli habari na mjadala huo umeniburudisha na kunipa elimu pia. Ama hakika, ishi ujionee na ujifunze kutoka kwa wanadamu wenzako.

  Kwamba nimeshambuliwa binafsi kwa kuwa Mjengwablog haiku-post picha za tamasha la Anti- Virus. Na ni jana tu hapa Iringa nimenunua kitabu cha Mr. Sugu kuhusu maisha yake- From Streets to The parliament.

  Ndugu zangu,
  Mie naishi na kufanya kazi Iringa. Ni mahali ambapo hata mtandao wa intaneti wakati mwingine ni wa shida. Na kublogu huku tunajitolea tu. Hata matangazo ya maana kwenye blogu wengine sisi hatuna. Ukweli tumeamua kuwa ' suguz'. Watu tuliojitolea kwa miaka mingi, kuwa tutapambana hadi risasi ya mwisho. Ndio maana, tunatumia senti za mifukoni mwetu kuendesha blogu zetu. Na mimi kazi ya kublogu naifanya nikiwa na wakati ziada.

  Tena siku hizi nina mwanafunzi wangu aliye Dar na anayejitolea wakati mwingine kuifanya kazi hiyo. Kuhusu picha za tamasha hilo linalosemwa nami niliziona zimetundikwa kwenye Mjengwablog na mwanafunzi wangu huyo.

  Niwahakikishie, kuwa Mjengwablog ni blogu huru. Haijapata kununuliwa na haitakuja kununuliwa kufanya kazi za kishabiki. Na mimi kama mmiliki wa blogu ndivyo nilivyo. Sijapata kununuliwa na sitakuja kununuliwa nimfanyie mtu kazi ya kishabiki na isiyo na maslahi ya kitaifa.

  Pamoja na yote hayo. Niseme tu, kwa hata mabaya yaliyoandikwa hapa juu yangu, sina kinyongo na mtu. Na nirudie, niliyosoma hapa usiku huu yameniburudisha pia. Nimebaki nikicheka mwenyewe kuona jinsi watu wanavyonifikiria, kunituhumu na kunihukumu, bila hata kunipa nafasi ya kunisikiliza.

  Nawatakia usiku mwema.

  Maggid,
  Iringa.
  .
   
 2. K

  Kuntakint JF-Expert Member

  #2
  Dec 5, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 1,111
  Likes Received: 468
  Trophy Points: 180
  pole sana
   
 3. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #3
  Dec 5, 2011
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,084
  Likes Received: 7,312
  Trophy Points: 280
  Bado hujani- convince!!!
   
 4. Mwakalinga Y. R

  Mwakalinga Y. R Tanzanite Member

  #4
  Dec 5, 2011
  Joined: Oct 22, 2008
  Messages: 2,718
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Hilo la kwamba pande za Iringa Internet ni taabu sizani kama lina ukweli . Nadhani wewe kama mmiliki wa blog unapaswa kupitia mara kwa mara kuona nini vijana wako wanapost ,kwa hilo inaelekea wewe haupo makini kwani ipo siku vijana wako watapost vitu ambavyo sivyo.Nadhani ulichokiona hapa jf kama ni mtu makini ufunguke kwani wengi wao ndio wanaokufuatilia na kukubali kwenye kazi zako za uandishi,huwa ni watu wachache sana ambao wanawezafanya tathnini yakinifu ya madhara ya hii mitandao ya kijamii.Mfano watu ambao hawakuwa wanajua na kufuatilia makala zako pindi watakapo ona thread kama ile,ni dhahiri wataanza kukufuatilia lakini kwa mtazamo hasi ambapo sio. MTAZAMO
   
 5. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #5
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Mkuu kweli uungwana ni vitendo, umetumia haki yako ya kiasili ya kujitetea, Binafsi nimekuelewa na utetezi wako nachukulia kwamba utachukulia hili kama changamoto ili siku nyingine usipate sintofahamu isiyokuwa na sababu.

  Licha ya kwamba wewe ni mwandishi huru na ambaye huna bei, yaani ununuliki lakini hawa maharamia clouds fm wamefanikiwa kulihujumu lile Tamasha la Anti Virus lisipate wadhamini kwa sababu mameneja masoko karibu wote ni connection ya Ruge, sasa wakati huo huo tukiona Blogu yako nayo imerusha Picha za Tamasha la clouds peke yake basi hapo jibu linakuwa kama kusoma hujui basi hata picha huoni?
  Nakutahadharisha humuangalie vizuri huyo mwanafunzi wako huenda alipewa bahasha na Kusaga.
   
 6. m

  maggid Verified User

  #6
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Mwakalinga,

  Sijui unaishi wapi. Tunaoishi Iringa tunajua kuwa mtandao wakati mwingine ni wa shida sana. Kwa nini niongope? Unasema mimi sio makini. Asante sana, nitajitahidi kuwa makini.
  Maggid,
  Iringa.
   
 7. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  Iringa ulipataje picha za virus ukashindwa kupata picha za ant-virus?
  Mwanume akiguna ina maana kakubali kosa. kwa kuwa umeguna tumekusamehe.
  Mimi binafsi kama figganigga nakuomba uwaunge mkono wasanii wetu wa Bongo fleva(vinega) katika halakati za kujikomboa. Je mikakati yako ni ipi ya kuwasaidia kuhakikisha sanaa ya Bongo inasonga mbele na wasanii kupata mafanikio? ni hayo tu. Mia
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Ameshaanza kwa kununuwa kitabu cha Sugu cha Muziki na Maisha, kuna paragraph muhimu sana mule kwenye kile kitabu kwa kijana ambaye amekata tamaa yaani mambo hayaendi. nitajitahidi niweke kwenye soft copy tufanye share ring kidogo.
   
 9. Mwita25

  Mwita25 JF-Expert Member

  #9
  Dec 6, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 3,840
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hukuwa na haja ya kuomba msamaha mkuu. Sidhani kama kulikuwa na kosa hapo.
   
 10. g

  goodlucksanga Senior Member

  #10
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Iringa hakuna internet.......we ndo entertainer kweli umechemka aiseee..!!
   
 11. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #11
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Huu ni utetezi wake, yeye yuko media house hawezi kuwa na akili za shake well before use half empty glass, na ndio maana anatumia jina lake halisi, na kukosolewa ni sehemu ya kujifunza.
  Neno samahani lina heshima kubwa sana ambapo clouds media wameshindwa kulitumia baada ya kujipatia pesa kwa njia za udanganyifu kwa kuwalaghai Watanzania kwamba DMX angeperform siku ile huku wakijuwa si kweli na wanawadanganya watu.
   
 12. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #12
  Dec 6, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Walitaka Sugu akose watu.
   
 13. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #13
  Dec 6, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  From palament to striti...!!! to meki a shoo...
  (((((((((((((((((lakini badoo))))))))))))
   
 14. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #14
  Dec 6, 2011
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  JF ina watu wa ajabu sana!
   
 15. Domenia

  Domenia JF-Expert Member

  #15
  Dec 6, 2011
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 462
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We Kibunango wa CCM Nani wa ajabu!!?
   
 16. Mzee Wa Rubisi

  Mzee Wa Rubisi JF-Expert Member

  #16
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,754
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Pole mkuu
   
 17. UmkhontoweSizwe

  UmkhontoweSizwe JF-Expert Member

  #17
  Dec 6, 2011
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 2,968
  Likes Received: 240
  Trophy Points: 160
  Kweli mkuu, na huo ndo uhuru wa kutoa maoni.
   
 18. Faru Kabula

  Faru Kabula JF-Expert Member

  #18
  Dec 6, 2011
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 10,640
  Likes Received: 2,872
  Trophy Points: 280
  Vipi, wewe hawajakuchomea moto baa yako?

   
 19. N

  Noboka JF-Expert Member

  #19
  Dec 6, 2011
  Joined: Nov 12, 2011
  Messages: 1,144
  Likes Received: 136
  Trophy Points: 160
  :tongue:Maggid kama binadamu ana mapungufu yake kama tulivyo wengi lakini mnaoshambulia mmejiangalia na nyie mapungufu yenu? mwenzenu amekiri kuwa matusi hayo ameyachukua kama funzo sasa mnataka afanyeje tena? naanza kuwa na wasiwasi na uwezo wa kufikiri wa baadhi yenu
   
 20. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #20
  Dec 6, 2011
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,272
  Trophy Points: 280
  Na ile Mzalendo.net ina watu wa namna gani? mabwabwa?
   
Loading...