Kijakazi
JF-Expert Member
- Jun 26, 2007
- 6,525
- 9,172
Baada ya utetezi huo, Watoto wako wansoma shule gani?
ijabahatika kuwa naye bado!
Unajua kwenye historia ya Lugha zamani nchi nyingi za ulaya kama Uingereza & Co. walikua wanatumia kilatini, na sababu hasa za wazungu wakiwemo waingereza kuacha kutumia kilatini ni kwamba kilatini ni lugha nyingine kabisa na haina uhusiano wowote na kiingereza kwa hiyo ilibaki kuwa lugha ya watu wachache tu "elite" na watu wa kawaida ambao walikuwa ndio wengi waliachwa nyuma (kama ilivyo Afrika leo), wakafanya mapinduzi yaliyoanzishwa na Martin Luther aliyetafsiri Biblia kwenda kijerumani na baada ya hapo mapinduzi yakaja na waingereza nao wakatafsiri kwa lugha yao "King James Bible", wakatoa kilatini na ndio maana unaona sehemu kubwa ya kiingereza na lugha nyingi za ulaya zina maneno ya kilatini, sasa wazungu wanalijua hilo na ndio maana wanakampeni sana kwa propaganda nyingi kwamba nchi za kiafrika zitumie lugha zao kwa maana wanajua zitabaki kueleweka na elite wachache ambao watawatumia kwa manufaa yao na waliobaki wengi kubaki kuburuzwa tu na elite wachache!
Duniani hamna jipya mambo yanakwenda yanajirudia hata hizo nchi zoote za kiafrika (Mungu atuepushe Tz) zinazotumia kiingereza/kifaransa/kireno ipo siku wakija kujitambua watafanya mapinduzi na kurudi kule kule wanakokupinga sasa hivi na nakuhakikishia haitakuwa kazi rahisi lakini ni lazima itafanyika!