MchunguZI
JF-Expert Member
- Jun 14, 2008
- 4,006
- 2,166
Ktk mchango wa Mh. Wenje kwa hotuba ya bajeti ya wizara ya Elimu, amewaeleza wabunge na mawaziri wote waache UNAFIKI wa kuweka sera ya elimu inayotaja wazi kwamba lugha ya kufundishia kwa shule za msingi ni Kiswahili, huku wao wabunge na mawaziri wakiwapeleka watoto wao shule zinazotumia Kiingereza.
Binafsi naomba niseme kwamba ni aibu mawaziri, wabunge, wakurugenzi, Rais, makatibu wakuu n.k hawaamini kwamba Kiswahili ni lugha inayowafaa watoto wao. Pamoja na imani hiyo wengi wanakuwa wanafiki kwa kusema lugha hii itumike ktk shule zetu zote. Tena wengine wanakwenda mbali na kutaka itumike hadi vyuo vikuu.
Nahisi wanasiasa wanataka kiingereza kibaki kuwa ni privilege yao na familia.
Tuache unafiki kama alivyosema Mh. Wenje, Tuseme ukweli kwamba wote tunahitaji kiingereza kuliko Kiswahili. Shule zetu zirudishe Kiingereza ili hata mtoto wa maskini aweze kutumia Kiingereza.