1. Kanisa litafakari kwa kina na kuchukua hatua kali zaidi dhidi udhalimu. Hapa tatizo si kushambuliwa kwa Fr. Kitima na wengineo bali UDHALIMU ulioota na unaoendelea kuota mizizi kwa kasi zaidi kuliko wakati mwingine wowote ule.
2. Kanisa liwaunganishe Watanzania wote kupinga udhalimu katika Nchi hii kabla hali haijawa mbaya zaidi. Tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Hakuna aliye salama kwa sasa. Ni uovu mtupu.
3. Kanisa litumie vyombo vyake kuhamasisha jamii kupinga udhalimu huu.
Okay, isipokuwa tambua tu kwamba
CCM imepoteza kabisa mvuto!
CCM imepoteza kabisa ushawishi!
Njia pekee kwa CCM kuendelea kuwa hai na kuendelea kushika madaraka katika Utawala wa nchi hii ni kwa kupitia kwenye kufanya Siasa za Propaganda za Vitisho Kama hizi za kuteka watu, kuua Watu, kuwashambulia na kuwapoteza wale Watu wenye ushawishi wanaokipinga Chama hicho. Nje ya Kuendesha Propaganda za Vitisho, kamwe CCM haiwezi kubaki salama na Wala haiwezi kuendelea kuwa hai, LAZIMA itakufa!
Utawala wowote ule uliofitinika na ambao upo mwishoni unakaribia kuanguka na kufa, huwa ni kawaida kabisa kutokea matukio mabaya Kama haya. Watawala huwa wanakuwa wameshikwa na kiwewe, wanaingiwa na hofu kubwa, kila Mtu mwenye Fikra mbadala na anayewakosoa au kuwapinga wanamchukulia kuwa ni Mhaini anayetaka kuwapindua.
Hali Kama hii pia iliwahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Zaire (DRC) wakati huo akiwa madarakani, Hali ambayo ilimfanya amteke hata Mkuu wake wa Majeshi General Mahele na kisha kumuua kikatili Sana Kama nguruwe pori, Mobutu alimshuku Jenerali huyo wa Jeshi kwamba alikuwa anamsaliti na kuwaunga mkono Wapinzani wake wa kisiasa.
Kwa Hali halisi ya kisiasa na HAKI za binadamu iliyopo hivi Sasa hapa Tanzania, tutarajie kushuhudia kwa wingi sana Watu wengi sana wakikumbana na matukio mabaya kama haya ya kushambuliwa, kutekwa, kupotezwa na hata kuuawa kikatili.