Kuhusu shambulio la Fr. Kitima

Kuhusu shambulio la Fr. Kitima

Okay, isipokuwa tambua tu kwamba
CCM imepoteza kabisa mvuto!
CCM imepoteza kabisa ushawishi!
Njia pekee kwa CCM kuendelea kuwa hai na kuendelea kushika madaraka katika Utawala wa nchi hii ni kwa kupitia kwenye kufanya Siasa za Propaganda za Vitisho Kama hizi za kuteka watu, kuua Watu, kuwashambulia na kuwapoteza wale Watu wenye ushawishi wanaokipinga Chama hicho. Nje ya Kuendesha Propaganda za Vitisho, kamwe CCM haiwezi kubaki salama na Wala haiwezi kuendelea kuwa hai, LAZIMA itakufa!

Utawala wowote ule uliofitinika na ambao upo mwishoni unakaribia kuanguka na kufa, huwa ni kawaida kabisa kutokea matukio mabaya Kama haya. Watawala huwa wanakuwa wameshikwa na kiwewe, wanaingiwa na hofu kubwa, kila Mtu mwenye Fikra mbadala na anayewakosoa au kuwapinga wanamchukulia kuwa ni Mhaini anayetaka kuwapindua.
Hali Kama hii pia iliwahi kumkumba aliyekuwa Rais wa Zaire (DRC) wakati huo akiwa madarakani, Hali ambayo ilimfanya amteke hata Mkuu wake wa Majeshi General Mahele na kisha kumuua kikatili Sana Kama nguruwe pori, Mobutu alimshuku Jenerali huyo wa Jeshi kwamba alikuwa anamsaliti na kuwaunga mkono Wapinzani wake wa kisiasa.
Kwa Hali halisi ya kisiasa na HAKI za binadamu iliyopo hivi Sasa hapa Tanzania, tutarajie kushuhudia kwa wingi sana Watu wengi sana wakikumbana na matukio mabaya kama haya ya kushambuliwa, kutekwa, kupotezwa na hata kuuawa kikatili.
Upo sahihi. Kuna hata kwenye vitabu vya Dini inasemekana kwamba, utawala dhalimu unapokaribia kufikia kwenye point ya mwisho kabisa huwa wanapofushwa macho, wanazibwa masikio yao na hivyo na hatimaye huweza kutesa mpaka kuua hata watu wake wa karibu. Inafika wakati hata mtoto wake anakuwa hamwamini. Kwa ujumla linakuwa kama gari lililopoteza mwelekeo. Litagonga kila kitu kilicho mbele yake.
 
Kitima ndo kanisa?mpumbavu toeni Udini wenu, Kibao hakua na dini? Waisalamu walidai kwamba uislamu ndo umevamiwa,
Tusio Waislamu tulilaani mauaji ya Mzee Kibao wakati wewe ulifurahia mauaji hayo. Lakini haiondoi kwamba Kibao hakuwa na Uongozi BAKWATA, ila Kitima ni Katibu wa Baraza la Maaskofu. Shambulizi moja ni personal, jingine ni institutional.
 
Kitima ndo kanisa?mpumbavu toeni Udini wenu, Kibao hakua na dini? Waisalamu walidai kwamba uislamu ndo umevamiwa,
We ni mbugila kinoma, kwahiyo mfano Mama Samia akishambuliwa anakuwa anakuwa aliyeumizwa ni Samia na sio Mwenyekiti wa CCM?

Kwamba kama alishambuliwa akiwa nje ya Ikulu inakuwa Raisi hajaumizwa?
 
Alishambuliwa kama Kitima personally au kashambuliwa kwa niamba ya kanisa? Acheni kuleta Udini katika hili suala tutapoteza lengo watanzania wangapi wameua na wana dini zao, mkileta Udini katika suala la no reform no Election tutapoteza wote kwasabb kila mtanZania ana dini yake.
Udhalimu hauishii hapo, hata wewe utakufuata tu.
 
Alishambuliwa kama Kitima personally au kashambuliwa kwa niamba ya kanisa? Acheni kuleta Udini katika hili suala tutapoteza lengo watanzania wangapi wameua na wana dini zao, mkileta Udini katika suala la no reform no Election tutapoteza wote kwasabb kila mtanZania ana dini yake.
Ok sawa tuseme kashambuliwa yeye kama yeye na siyo kwasababu ya Dini yake wala Kanisa lake.
1. Je waliomshambulia walilenga nn au
walifanya hivyo kwa lipi hasa??
2. Je akitoa maoni yake yeye kama yeye
iweje maoni yake binafsi yahusishwe
na Dini yake na Kanisa lake??

Ukweli wa shambulio lile liko wazi na Watz walio wengi sio wajinga. Wanafahamu ni nani waliopanga na ni nani waliotekeleza unyama ule. Mungu yupo ambae ni Hakimu wa kweli. Giza kamwe hiliwezi kushinda nuru.
 
Safari hii mmeyakanyaga, kanisa halitaacha hili lipite hivihivi
Yeah Tena hapa haitakuwa ukatoliki bali ukristo ni mbaya sn hii
Sijui waliwaza nn kabla ya kufanya haya!

Mi sio rc ila kati ya wakristo ambao hawayumbishwi Wala huwakuti tuition 🤣Kwa manabii huko ni RC
 
Back
Top Bottom