Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

Kuhusu Mwakyembe na Mwandosya this can be true kabisa!

Inaonekana ni ukristu zidi ya Uislamu maana kati ya walengwa sioni akina Zito na waislamu wengine ambao huwa mwiba kwa serikali inapovurunda.
Sasa nimeanza kumkumbuka Mwalimu juu ya udini na ile speech yake

didas masaburi on work...
 
dah, sasa polisi wameshindwa vipi kufanya kazi, mbona uchunguzi alishaumaliza mwenyewe, mengi yamesomeka, lakini hilo la DR kuamini uganga mhmmm, sasa unga gani unapumbaza. mungu akujalie upone Dr uje upambane mwenyewe maana inaonyesha na wewe una kikosi kama taarifa zote hizi umezipata.pole sana
 
alamsiki kaka, kilichokufanya ukaficha madudu ya serikali wakati unailipua richmond ndo matokeo yake haya kumbuka wenzio walisema 'hatukukutana barabarani' we kaa na uzalendo wako wa kinafki na huo ndio mshahara wake, alamsiki mkuu.

Mkuu, mimi naamini tatizo ni lako wewe na Watanzania walio wengi sana ambao wanaamini kuwa wajibu wa kuanzisha na kumalizia kampeni dhidi ya ufisadi nchini ni wa akina Mwakyembe, Sitta, Slaa n.k. ila sisi wengine tubaki tukipenyeza hoja za kejeli na vijembe vya rejareja kwenye JF.

Walipotufikisha akina Mwakyembe kwa ujasiri mkubwa sana katika mapambano haya, panatosha sana na sisi tuendeleze kwa ujasiri uleule. Ni haohao akina Sitta, Mwakyembe ambao wameonyesha ujasiri wa hali ya juu kukataa malipo kwa Dowans pamoja na kwamba wako serikalini na suala hilo likabadilika mwelekeo!

Mimi naamini leo hii akina Dk. Mwakyembe wakiulizwa ni nini walikiweka kiporo katika suala la Richmond/Dowans, nina uhakika wanaume hao wataweka hadharani. Naamini hawaoni haja kufanya hivyo kwa kuwa hatuko serious; hatuko focussed na hatuna msukumo wa dhati wa kulimalizia suala hilo!

Nakumbuka mwaka jana, mwanafunzi wa sheria wa mwaka wa tatu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam alinieleza kuwa walikuwa na Dk. Mwakyembe kwenye mhadhara maalumu wa somo la Katiba ambapo Dk. Mwakyembe aliwaelezea wanafunzi sababu zilizomfanya yeye na wenzake akina Selelii wasiseme yote.

Alisema Watanzania kwa ujumla wao ni watu waoga sana ambao kujitoa kwao kwa mapambano yoyote yale ni kwa bahati nasibu nasibu hivi. Ni rahisi sana kukuacha peke yako kwenye mataa halafu nwakakufuatilia kwa umakini kupitia MwanaHalisi au Raia Mwema! Hivyo Dk. Mwakyembe akasema mpambanaji yeyote makini lazima ajiwekee bima mwenyewe; ajitengenezee ulinzi wake mwenyewe ili mambo yakimgeukia na Watanzania wote wameangalia kwingine, ajinusuru kwa kuliweka lililobaki hadharani!

Hebu Human Rights Centre, Vyuo Vikuu, Vyama vya Wanasheria n.k. waiteni akina Mwakyembe watufafanulie haya! Msiseme watakataa, waliwahi kukataa lini? Mipango ya kuwaua hawa jamaa ipo kwa kuwa wanabeba siri nzito. Badala ya kuwa-engage intellectually, tunawakejeli huku tumevaa kanga kiunoni! Acheni vimbwanga hivyo jamani, havitufai watu wazima!
 
kwa maana hiyo we conclude HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI HAINA TIBA KWA'' MAGONJWA MAKUBWA AU HAINA TIBA KWA WAKUBWA TUU''
 
Huyu jamaa kama wakati huo aliweza kutoa maelezo ya kina kuhusu kuwindwa kwake kutaka kuuliwa, sipati picha hata kidogo iwe je kama kuumwa kwake kwa sasa hivi kuna mkono wa mtu ashindwe kutupa maelezo ya kina pia. Tena kwa maneno yake, ile pieee! kuanza kuwashwa ni takribani miezi mi3.

Watu watajaribu kueneza uvumi mwingi tu ila mwisho wasiku misemo hii ya kiswahili ita simama, "mficha uchi.......na kuna mficha ugonjwa ........." mtanisaidia kujaza.
 
Mkuu Kapela, nakupongeza kwa hoja iliyokwenda shule. Hoja nyingi za JF siku hizi hazitofautiani na za akina nanihii wakisukana nywele!
 
Huyu jamaa kama wakati huo aliweza kutoa maelezo ya kina kuhusu kuwindwa kwake kutaka kuuliwa, sipati picha hata kidogo iwe je kama kuumwa kwake kwa sasa hivi kuna mkono wa mtu ashindwe kutupa maelezo ya kina pia. Tena kwa maneno yake, ile pieee! kuanza kuwashwa ni takribani miezi mi3. Watu watajaribu kueneza uvumi mwingi tu ila mwisho wasiku misemo hii ya kiswahili ita simama, "mficha uchi.......na kuna mficha ugonjwa ........." mtanisaidia kujaza.

Mkuu, kama huyu jamaa huko awali aliwahi kutoa maelezo ya kina (tena yenye ushahidi kamili) hayakufanyiwa kazi. Unataka leo tena, akiwa na dripu mkononi akutumie maelezo ya kina kuhusu ugonjwa wake, ili iweje?
 
Ole wao kama wanaifananisha vita hii na dini, kama ni uislamu juu ya ukristo ,Mungu na awaonyeshe yeye ni nani. Na kwa damu ya Yesu nawafunika wote , watakuwa wazima hadi hao wauaji na wafadhili wao watakapoteketea na kutoweka kwenye uso wa dunia...can sombody say amen?????
 
Mwakyembe1.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam juzi.
 
Mkuu, kama huyu jamaa huko awali aliwahi kutoa maelezo ya kina (tena yenye ushahidi kamili) hayakufanyiwa kazi. Unataka leo tena, akiwa na dripu mkononi akutumie maelezo ya kina kuhusu ugonjwa wake, ili iweje?


Mkuu mwenza angeweza kuweka hata kwa ajili ya records tu. Huoni hayo maelezo ya huko nyuma watu wanayatumia kwa reference. Imekuwa tabia ya wanasiasa wetu kutoa visingizio ambavyo hawawezi kuvithibitisha wanapotakiwa kufanya hivyo. Hatuja sahau ya DR Slaa na kuchakachuliwa kura.
 
kwa maana hiyo we conclude HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI HAINA TIBA KWA'' MAGONJWA MAKUBWA AU HAINA TIBA KWA WAKUBWA TUU''
Labda kuna hisia kwamba hapo muhimbili atakaye takiwa kumchoma sindano ni rahisi kumnunua achome sindano ya sumu
 
Nawasilisha maeleoz yote bila kuficha namba wala majina ya watu. Mwenye kujua namba ya haya magari atusaidie ni ya kina nani?

Katika barua hiyo ya 9 Februari 2011, iliyobebwa na kichwa kisemacho, “Taarifa ya njama za kuondoa maisha yangu na ombi kwa jeshi la polisi kulinda haki yangu ya kikatiba ya kuishi,” Dk. Mwakyembe anataja watu wengine mashuhuri wanaotishiwa kuuawa.

Hao ni mfanyabiashara mashuhuri nchini, Reginald Mengi, waziri wa Maji na Umwagiliaji, Profesa Mark Mwandosya, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe na mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Melecela.
Dk. Mwakyembe anasema katika barua yake, “Pamoja na kwamba taarifa hii ni mpya yenye matukio ya takribani mwezi mmoja tu, naamini kwa dhati kuwa msingi wake – kwa maana ya wahusika na maudhui – hautofautiani na ule wa matukio mengine ya awali ambayo baadhi yake yalisharipotiwa polisi na vyombo vingine vya usalama kwa lengo la kuchunguzwa.”

Anasema pamoja na hayo, bado ana imani kubwa na jeshi la polisi kuwa litaifanyia kazi taarifa hiyo bila kujali nguvu ya ukwasi na ya kisiasa ya watuhumiwa.

Msingi mkuu wa yeye kuamua kuvitaarifu vyombo vya dola, anasema Dk. Mwakyembe, ni taarifa alizozipata kutoka Songea, 22 Januari 2011 zinazolihusu kundi la watu saba lililoingia mjini humo usiku wa 21 Januari 2011 wakitumia gari linalodaiwa kuwa la wizara yake.Gari hilo aina ya Land Cruiser lilikuwa na namba za usajili STK 6868, lakini baadaye namba ilibadilishwa na kusomeka STK 6869.Gari hilo liliwateremsha “abiria” hao saba sehemu iitwayo Madaba na kisha kuchukuliwa na gari jingine Land Cruiser hardtop, Na. T 768 BDU hadi baa ya Top Inn mjini Songea.

Anawataja baadhi ya abiria waliokuwamo katika gari hilo kuwa ni raia wawili wa Somalia, Hafidh na Faraj, “kijana mmoja wa Kichagga” kwa jina Mustafa a.k.a “Master” Mkusa ambaye imeelezwa kuwa ni ofisa wa idara ya usalama wa taifa na mwingine aliyejulikana kwa jina moja la Ramika kutoka Tanga, ambaye inadaiwa ndiye “mtaalamu” wa kukaba watu.
Dk. Mwakyembe anaeleza katika barua yake kwa IJP, kwamba aliyepokea genge hilo la wahalifu mjini Songea, ni mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Songea Vijijini, Rajabu Mtiula akiongozana na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Manya.

“Usiku wa Jumamosi 22 Januari 2011, kundi hilo lilielekea Mbunde, wilayani Namtumbo kwa gari aina ya Defender STK 2654, likiendeshwa na Zuberi Komba kwa lengo la kukutana na ‘mganga’ Majungu (kabila Mdendeule) ambaye anaishi ndani ya mbuga ya wanyama (Selous Game Reserve with impunity,)” anaeleza Dk. Mwakyembe katika barua yake.
Anasema, “Defender hiyo iligeuza kurejea Songea siku mbili baadaye na kuwaacha wageni hao kwa mganga ambako walikaa siku saba wakitengenezwa. Walirejea Songea 29 Januari 2011 na kesho yake, 30 Januari 2011 wakaanza safari kurejea Dar es Salaam.”

Anasema kutoka Songea hadi Mafinga, watuhumiwa wa njama za kuua walitumia gari Na. T 768 BDU ambalo walilitumia awali kutoka Madaba hadi Songea. Anasema walifika Mafinga saa mbili usiku na kukuta magari mawibili yakiwasubiri. Moja, Hilux Mayai ya kampuni ya Vodacom na Defender iliyowaongoza hadi Morogoro.

Akiandika kwa kujiamini, Dk. Mwakyembe anasema, “…walipofika Morogoro walipokelewa na askari mmoja anayemtaja kwa jina la Sabasita. Hapo kundi likagawanyika: Watu wanne wakiwemo wale wasomali wawili wakaingia kwenye Nissan Patrol T 845 ADH mali ya kampuni ya Caspian, na wengine wakabaki Morogoro.”

Kampuni ya Caspian ni mali ya Rostam Aziz, mfanyabiashara, mbunge wa Igunga (CCM) na wakala anayejitaja kuwakilisha kampuni ya kufua umeme ya Dowans ya Costa Rica. Gazeti lilipomtafuta, hakuweza kupatikana.

Anamwambia Mwema kuwa, Mganga Majungu mwenyewe, ambaye wapelelezi wake wanaweza kuongea naye kama walivyofanya waliompa taarifa hizi, aliwapa masharti ya kutotumia silaha za moto ila njia nyingine kumuua kwanza Mwakyembe, baadaye Dk. Slaa na wengine.

Anasema mganga huyo “ametengeneza dawa ya kuwapumbaza waliohukumiwa kifo na kuwa mfano wa mbwa mbele ya chatu” ili kukimbia hasira za wananchi pale mpango wa mauaji utakapotekelezwa.

Dk. Mwakyembe anamueleza IJP Mwema, kwamba awali mkakati wa kumuua Dk. Slaa ulipangwa kutekelezwa katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, lakini ulisitishwa kwa hofu ya kuingiza nchi katika machafuko.
“…utabiri wa Sheikh Yahya Hussein mwaka jana kuwa mmoja wa presidential candidates (wagombea urais) atakufa, ulimlenga Dk. Slaa ambaye alidaiwa kubebwa na makinisa. Utabiri huo haukutimia kwa kuogopa kuiingiza nchi kwenye machafuko makubwa ya kisiasa/kidini ambayo yangewaweka pabaya hata wafadhili wa mpango wenyewe,” anasema.
Wiki mbili zilizopita, Sheikh Yahaya alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kutatokea vifo vya watu kadhaa mashuhuri wakiwamo wanasiasa na mwandishi mmoja wa habari mashuhuri nchini. Wakati Shekh Yahaya anatoa utabiri wake, Mwakyembe alikuwa katika wiki ya tatu tangu awasilishe malalamiko yake polisi.

MwanaHALISI lilipowasiliana na Sheikh Yahya ili kufahamu iwapo utabiri wake unatokana na kutumiwa na watu maalum waliomlipa fedha ili kufanikisha mkakati huo wa mauaji, mnajimu huyo alisema, “Watu wasubiri matokeo.”
Alisema anachokifanya yeye ni unajimu na tayari amefanya hivyo katika matukio kadhaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuwako kwa serikali ya umoja wa kitaifa Zanzibar.

“Nilitabiri Raila Odinga kuunda serikali moja na Mwai Kibaki Kenya. Yametimia. Nilitabiri CCM itapata msukosuko baada ya uchaguzi mkuu, imekuwa hivyo. Sasa hapo unahoji nini?

“…Sijataja jina la mtu, hivyo watu wasijihisi kwa utabiri wangu, ila wao wasubiri matokeo. Halafu ninyi MwanaHALISI mnafanya kazi nzuri. Ipo siku nitawaita hapa kuzungumza nanyi. Ila nayi msihofu, msubiri matokeo.”
Naye Dk. Slaa alipoulizwa kuhusu mpango huo, kwanza alicheka, kisha akauliza: “Nani kakuambia?” Alipoelezwa kuwa ni taarifa zilizothibitishwa na jeshi la polisi, Dk. Slaa alisema, “Basi nadhani wao ndiyo wanajua wanaohusika katika suala hilo.”
Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kijana mmoja anayefahamika kwa jina la Hassani alitumwa kutoka Dar es Saalam kwenda Dodoma, 5 Februari mwaka huu kwa “maandalizi” ya kikosi cha mauaji. Amesema tayari kikosi hicho kimefanya utambuzi wa nyumba yake aliyopangiwa kuishi na serikali.

Anasema, “Tarehe 6 Februari 2011, mnamo saa nne usiku, kikosi hicho cha mauaji kikiwa na watu watano kiliondoka Dar es Salaam kwenda Dodoma kwa gari aina ya Land Cruiser nyeupe ya mkonga (T 360 AKU). Waliokuwa kwenye kikosi hicho ni wasomali wale wawili, mgeni mmoja wa kiume kutoka Uganda, Mustafa a.k.a ‘Master’ na kijana mmoja ambaye tarehe 19 Januari 2011 aliwabeba wasomali hao kutoka Morogoro kwa gari aina ya VX Lands Cruiser T 656 APF. Kijana huyo ana shepu ya Kitusi na anaongea Kifaransa.”

Jijini Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anasema, “Wahitimu hao wa Profesa Majungu walifikia Kiwalani karibu na Kiwanda cha Mohammed Enterprises. Jirani na kiwanda hicho kuna jengo la ghorofa, chini ni msikiti wa Waarabu unaoitwa MALKAZ na juu ni sehemu ya kuishi.”

Anaeleza kuwa tarehe 5 Februari, wageni wawili zaidi waliwasili kwa ndege kutoka Uganda. Mwanaume mmoja (aliyechanganya rangi) na mwanamke mmoja (mweusi vilivyo). Anaripoti kuwa walipokelewa kwa magari mawili: moja la polisi, PT 0288 – polisi ujenzi na la pili lenye namba za kibalozi T 69 CD 82 aina ya RAV 4. Anasema, jioni wakawa na mazungumzo ya kina na raia wawili wa Somalia ambao inadaiwa ni kutoka kundi la Al-Shabaab.

Dk. Mwakyembe anasema katika maelezo yake kwamba amepata picha ya kwa nini wapiganaji wa kikundi hicho wameingizwa nchini.

Anasema, “Nimeweza kukusanya taarifa zinazodai kuwa awali walifikiriwa kuletwa wapiganaji kutoka Rwanda, lakini wazo hili lilikataliwa na wafadhili wa mpango huu ambao walitaka wanaharakati wa aina hiyo watoke Somalia. Ndipo kikundi hicho kikashawishiwa. Mimi na wenzangu hao watano tumejengewe hoja kuwa maadaui wa Uislamu tunaotumiwa na makanisa, hivyo hatuna budi kukatishwa maisha yetu.”

Katika barua yake kwa IJP, Dk. Mwakyembe anasema kila siku hupata taarifa za ziada kutoka kwa raia wema kuhusu suala hili; anazitoa taarifa hizo kwa jeshi la polisi ili ziwasaidie katika upelelezi.

Kwanza, taarifa zinaonyesha raia hao wa kisomali waliingia nchini kutokea Kenya na walikwenda Dodoma kupitia njia ya barabara kwa kutumia gari aina ya RAV 4 (new model- T 816 AQS) tarehe 08 Januari 2011.
Pili, Dk. Mwakyembe anasema walipofika Morogoro walipokewa na askari Sabasita wa jeshi la polisi mkoani humo, ambapo walikaa katika hoteli mbili tofauti – Hillux Hotel na Top Life. Anamtaja aliyewafanyia booking wageni hao ni mmiliki wa Morogoro Hotel aliyemtaja kwa jina moja la Kari.

Tatu, Dk. Mwakyembe anasema magari waliyotumia wakiwa Morogoro, ni RAV 4 T 816 AQS, VX Land Cruiser STK 1287, Mercedez Benz (Station Wagon) T 874 BDT, Toyota Mark II GX100 nyeupe T 218 BKR na wakiwa Dar es Salaam wametumia magari VX Land Cruiser T 656 APF na Nissan patrol T 845 ADH.

Wakiwa Dar es Salaam, Dk. Mwakyembe anataja watu waliokuwa na mawasiliano na waliotumwa kuchukua roho yake kuwa ni “Masuhe wa Central Police Station (polisi kati), Fred Lowassa ambaye inadaiwa aliwapelekea mbuzi watatu huko Kiwalani tarehe 04 Februari 2011 na hata kuwatafutia gari VX Land Cruiser T 656 APF.

Anasema walipokuwa Dar es Salaam, tarehe 13 na 14, Januari wabaya wake walifikia nyumba Na. 551, Mtaa wa Chakechake, Upanga.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Vijijini, Rajab Mtiula, hakupatikana juzi kuzungumzia kuhusishwa kwake katika mikakati hiyo.

Gazeti lilipowasiliana na Fred Lowassa kueleza juu ya kuhusishwa katika maandalizi ya kifo cha Dk. Mwakyembe na wenzake alijibu, “Kaka katika mazingira ya kawaida tu, hilo jambo ni very serious (hilo jambo zito). Kuua ni tuhuma nzito.
Alisema, “Siku hizi kuna teknolojia ambako ukifanywa uchunguzi, itaonekana tu. Mimi nimekutana na mambo magumu sana maishani, lakini siwezi kufikia hatua ya kuua au kuhusika kuua.”

Fred ambaye ni mtoto wa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa alisema, “Yakinipata magumu, mwokozi wangu ni Mungu. Naomba Mungu, halafu huwa nasamehe. Siku zote huwa sipendi kuingia kwenye malumbano,” alieleza.
Lakini Dk. Mwakyembe katika barua yake kwa IJP Mwema anasema, “Pamoja na kwamba sina imani na ushirikina au nguvu za giza, kutajwa kwa jina langu na fursa ya pekee niliyokuwa nayo ya kujua kilichokuwa kinafanyika, kukanipa ari, nguvu na shauku ya aina yake kutaka kulielewa zaidi suala hili ili ikibidi, niwataarifu wenzangu nao waelewe.”
Taarifa zinasema kila aliyetajwa kuuawa amejulisha taarifa hizo na Dk. Mwakyembe kama ambavyo ameeleza katika maelezo yake polisi.
 
Mwakyembe1.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam juzi.
Jakaya Mrisho Kikwete ni mtu anaye jali sana utu na ni muungwana sana.
 
Mwakyembe1.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam juzi.


Kuhudhuria Misiba, Mazishi, vipaimaira, Harusi, Ngoma, Majando, Kutembelea wagonjwa na mambo yasiyo na tija Mkwe.re anayapenda sana.
 
Stori za kupikwa bwana!!! Huyo mganga ana dawa huko Selous ya kuogopewa zaidi ya mungu? Labda uranium poisons Mwakyembe ni msanii tangu alipoichunguza Richmond bila ya kudeclare yeye mwenyewe mwanahisa katika kampuni ya ufuaji umeme wa upepo mie nimetokea kutomwamini kabisa mwanasiasa huyu. Labda tu ameathirika na dawa fulani (kwani Exfoliative Dermatisis) sometimes inasababishwa na dawa ikikudhuru (medicine allergy) but hili la conspiracy kutaka kumuua mh naona kama ni hadithi za kusadikika.

Kwahiyo mkuu unasubiri afe ndo uamini?

Suala la richmond na afya yake ni vitu viwili tofauti. Hata mimi sikuridhika to some extent kwa kile alichodai kuficha baadhi ya findings za tume yake kwa maslahi ya serikali ya chama chake. Lakini hiyo haimaanishi kwamba kila atakalosema haliaminiki.

Aliwahi kupata ajali, akashuhudia kwamba kuna watu wanamtafuta, watu kama wewe wakabisha. Badae mwaka huu mwanzoni akatoa taarifa za kufuatiliwa ili auwawe bado watu mnabisha, pamoja na ushahidi wa magari na watumishi wa serikali wanaotumika kutaka kumuua kuwekwa wazi lakini bado tu mnabisha. Kuna mbunge aliwahi kunaswa na kamera za bunge akitaka kumfanyizia lakini bado tu mnabisha.

Nadhani kimoyo moyo mnamuombea afe, si bure!
 
Napata taabu sana moyoni! MWANDOSYA NA MWAKYEMBE wapo kambi tofauti na mkuu wa nchi ndio maana hata Mbeya mkuu wa kaya bado hakubaliki kwa sababu ya mawaelewano yake mabaya na hawa jamaa 'si-mnakumbuka Mbeya walimpiga mawe mkuu wa nchi?'

Sasa wakali hawa wawili wote wapo India hospital moja (Apollo) wakiwa wanaugua magonjwa ya kutisha! Nakumbuka hata Kimaro (yule mbunge wa wazamani wa Vunjo) baada ya kuwashambulia mafisadi (mkuu wa kaya included) aliugua nusu ya kufa! Kwa nini wapambanaji wa ufisadi ndani ya CCM wanaugua namna hii?

Anywayz tumwachie Mungu.
 
Mwakyembe1.JPG


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali Naibu Waziri wa Ujenzi, Dkt.Harrison Mwakyembe wakati alipomtembelea nyumbani kwake Kunduchi Mtongani, jijini Dar es Salaam juzi.

kwa hiyo hapa Mkuu alikwenda kuangalia/kuhakiki kama kazi imefanyika vyema?
 
Fanya editing kidogo ya habari yako, uweke na paragraphs, hii inakuwa ngumu sana kuisoma mpakaa mwisho.
mkuu sio ngumu kuisoma wewe ndo mvivu wa kusoma.ina tatizo gani.?mbona inasomeka vizuri.?kama unaona ngumu kuisoma just itengenezee paragraph mwenye.alafu unasema eti "hii inakua ngumu sana kuisoma mpaka mwisho"ndo nyie mnakuja kukurupuka na kuandika upupu simply because hamjasoma mpaka mwisho kwa ajili ya uvivu wenu.mkuu tulia read btn the line,huku ukitafakari unachosoma sio kwenda kwenda tu ka bendera.kama ukipoteza the meaning the word above while unasoma at the end of the story hutaelewa .any way unawakilisha watanzania wengine ambao ni wavivu kusoma hata walichoandikiwa.
 
Back
Top Bottom